Humphrey Polepole: "Hatuwezi kuwa nchi inaendeshwa kama idara ya 'Fire'

Humphrey Polepole: "Hatuwezi kuwa nchi inaendeshwa kama idara ya 'Fire'

Si kaongoka sasa!

Kwani mtume Paulo ilikuwaje?

Litesi na liuaji maarufu la wafuasi wa Yesu na sasa ndiye baba wa Enjili!

Kuwahi kuwa sehemu ya tatizo haikatazwi mtu kujitambua, kujuta na kubadilika.

Mungu kusamehe makosa yetu, inamaanisha sisi ni wakosefu, tunatubu na sasa tunamrudia yeye na yeye anatusamehe.

Nimetoa mifano ya kiimani kama angalizo kumhusu mtu mbaya kwa namna anavyoweza kubadilika na kuwa mtu tegemeo anayefaa sana!

Tusimhukumu kwa yaliyopita kama ameamua kutubu na kuyakana maovu aliyokwisha kuyatenda, tumpokee na sasa tusikilize mantiki ya maudhui yake tu.
Wenye akili timamu pekee ndo wataelewa!
Binafsi napenda sana disruptors! Mara zote wanatufanya tufikirie upya!
 
Tangu miezi mitatu iliyopita tumesoma humu Habari za kila aina
Mara mwezi ujao kuna mtu anatuaga, mara ooh kuna habari mbaya sana mwezi wa Saba
Hata mwezi wa nane waliandika kuwa mambo mengi yatatokea.
Ila hakuna anaejua kesho
Na hili Acha tusubiri nchi isimame maana siku zinaenda mbio sana
Mkuu mbona yote yametoka au upo ulimwengu gani???
 
Wakuu!

Humphrey Polepole amesema alijiuzulu Ubalozi wa Cuba ili awe huru kuzungumza kwamba kuna tatizo kubwa katika Taifa letu na sio dhambi kujirekebisha.

Sasa leo saa 2:00 usiku usikae mbali nami hapa nitakuletea kila atakachokizungumza.

Updates... Polepole

Utamaduni, desturi na katika ya Chama cha Mapinduzi Rais Samia hatakiwi kupeperusha bendera ya CCM kipindi hiki kwa msingi kuwa amekuwa Makamu wa Rais, Mungu akampromote kuwa Rais, tunapokwenda kubadilisha awamu tunakwenda kusema tumewaletea hawa, tutakimbia kwa mwendokasi huu.

"Hatuwezi kuwa nchi inaendeshwa kama idara ya 'Fire', tunataka mtu ambaye anchukizwa na ulegelege huu"

, Salamu ya 'Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.... Kazi iendelee!' inamkiuka Mungu

"Ni Haki ya kila mmoja kugombea lakini haipendezi kwenye mchakato wa Ubunge ni Watu wa Familia za Viongozi."


Nampenda sana Rais Paul Kagame, hacheki na nyani kama huyu, ndio maana shamba lake la mahindi liko salama na anaendeleza nchi fasta kuliko sie wote Afrika Mashariki na Kati. Hauhitaji kuwa na PhD kujua ni nini mnafiki kama huyu PK angemfanya nini libaki kuwa fundisho kwa wengine dizaini yake.

Ila na yeye HP asimchukulie mama poa sana. Ajue naye ana familia, ana ndugu jamaa na marafiki wanaoteseka kwa kumdhihaki waziwazi hivi. Mama anaweza akampuuza ila kuna mtu anaweza kujitokeza akamjibu kwa niaba ya Mama.

Halafu, kimtu kama hiki kina impact gani katika nchi hii? Nina ushahidi kwamba aliptimuliwa nafasi ya Uenezi CCM makao makuu (alishaastukiwa kuanzia hapo) walifanya tafrija kushukuru mnafiki mwenye roho mbaya huyu kuondoka. Naambiowa Mtafute DC wa Kisarawe Magoti (alikuwa msaidizi wake) akupe za ndaaaani za nyani huyu ambaye yeye kazaliwa kupinga kila kitu na mbishi. Yaani hapo alipo anaweza akabisha kabisa kuwa yeye si Humphrey Polepole! Yaani anajiona kama ndiye Socrates wa Tanzania! Yaani anajiona yeye ana akili kuliko kiumbe yeyote nchini...

Sinema hapa iko hivi: Baada ya Polepole na genge lake (tuliite Team 2025) kushindwa kumyumbisha Magufuli, wakarudisha mpira kwa kipa na kukubaliana waacha mashambulizi hadi miaka mitano ipite, ndipo warudi kushambulia.

Bahati mbaya ama nzuri kikatokea kilichotokea. Mama akachukua timu. Muda ulipoenda Mama akanogewa ama akaona amalizie ngwe na kuweka nia ya kugombea. Kina Polepole na wenzie wakatahayari. Wakaanza fujo kwa mbaaaaali. Akapelekwa Malawi kisha akatupwa Cuba sababu yeye alikuwa kiwavi wao anayeuza ramani ya vita. Hivyo usishangae kumuona anaibuka sasa wakati mchakato umeshaanza na mashambulizi sasa ni kuhakikisha Mama haendelei na gemu. Timu yao ina kina Mpina, Gwajima (huyu kachukuliwa baada ya kujipendekeza kwao kwa kuona hatoboi tena kisiasa achilia mbali jimbo). Read the pattern.

Kama kuna mtu Team 2025 wanamchukia ni JK ambaye ndiye master mind wa kuua plani yao kwa kupendekeza na kukubaliwa Mama achaguliwe mapema pamoja na mgombea mwenza wake. Hapo team 2025 ya kina HP ikakuta CCM imepaki basi golini na hakuna ujanja hadi 2030 na penginepo hadi 2040 na hata 2050. Na hawana ujanja wala uwezo zaidi ya kubwabwaja mitandaoni.

JK, ambaye HP anamwita mstaafu mmoja, ni mtu ambaye anajuta kwa nini alimchomoa HP kwenye ki-NGO kimoja cha vijana wanaharakati alipomuona kule Ethiopia. Akamwita nyumbani akampa kazi na exposure. Ghafla tu huyu mnafiki asiye na shukurani kawa mjuaji kuliko Watanzania wooooooote, hususan wana CCM. Yaani anaongea as if yeye ndiye aliyeasisi TAA, TANU na CCM, ndiye aliyemfundisha hata Nyerere siasa! Yaani CCM wote hawajui ila yeye tu!

Nani? Huyu huyu Polepole aliyeokotwa na JK Ethiopia na kufadhiliwa leo ndio awe hivi??? Jiulize DAH!

Ama kweli Yuda wako hadi leo. Kwa ufupi wala mtu asihangaike. Huyo ni Team 2025 iliyokwama na ambayo inajua wakikosa mwaka huu ndio basi tena. Akitoka Mama, nani wa kumzuia Balozi kubeba timu? Nani? Polepole? Gwajima? Mpina? Au hao walio benchi lao la ufundi (muda ukiwadia nitawataja wote na ushahidi juu) wanaohaha.

Check the pattern...Mpina, Gwajima na sasa Polepole utakuta lugha yao ni moja. Hii Team 2025 wapo wengi wanasubiri muda wao, na wengine wameangukia pua kwenye mchujo wa uchaguzi wa ubunge na hata udiwani! Ila basi la CCM lililopaki golini inabidi sijui wafanye nini watoboe. So funny wakidhania vita mtandaoni inawafikia Watanzania wote. Cheki ripoti ya TCRA kuhusu wangapi wanamsikiliza, utaona. Hapo sijataja wangapi wana bando la kuusikiliza upuuzi wake...

Na picha kama hii inawauma kweli unaambiwa...

Watch this space
-Tarishi
IMG_5807.jpg
 
Pole pole ni mnafiki Sana. Huyu ndio alipambana kuiua CHADEMA kipindi Cha Magufuli, Sasa hivi anajifanya mwanademokrasia. Very stupid guy.
Kwa hiyo ulitakaje ndiyo akili zenu nyie Watanzania
 
Nampenda sana Rais Paul Kagame, hacheki na nyani kama huyu, ndio maana shamba lake la mahindi liko salama na anaendeleza nchi fasta kuliko sie wote Afrika Mashariki na Kati. Hauhitaji kuwa na PhD mnafiki kama huyu PK angemfanya nini libaki kuwa fundisho kwa wengine dizaini yake.

Ila na yeye HP asimchukulie mama poa sana. Ajue naye ana familia, ana ndugu jamaa na marafiki wanaoteseka kwa kumdhihaki waziwazi hivi. Mama anaweza akampuuza ila kuna mtu anaweza kujitokeza akamjibu kwa niaba ya Mama.

Halafu, kimtu kama hiki kina impact gani katika nchi hii? Nina ushahidi kwamba alioondolewa nafasi ya Uenezi CCM mamako makuu walifanya tafrija kushukuru mnafiki mwenye roho mbaya huyu kuondoka. Mtafute DC wa Kisarawe Magoti akupe za ndaaaani za nyani huyu ambaye yeye kazaliwa kupinga kila kitu na mbishi. Yaani hapo alipo anaweza akabisha kabisa kuwa yeye si Humphrey Polepole! Yaani anajiona kama ndiye Socrates wa Tanzania! Yaani ana akili kuliko kiumbe yeyote nchini...

Sinema hapa iko hivi: Baada ya Polepole na genge lake kushindwa kumyumbisha Magufuli, wakarudisha mpira kwa kipa na kukubaliana waacha miaka mitano ipite, warudi kushambulia. Bahati mbaya ama nzuri kikatokea kilichotokea. Mama akachukua timu. Muda uliopoenda akanogewa na kuweka nia ya kugombea. Kina Polepole na wenzie wakatahayari. Wakaanza fujo kwa mbaaaaali. Akapelekwa Malawi kisha akatupwa Cuba sababu yeye alikuwa kiwavi wao anayeuza ramani ya vita. Usishangae kaja sasa wakati mchakato umeshaanza na juhudi sasa ni kuhakikisha Mama haendelei na gemu. Timu yao ina kina Mpina, Gwajima (huyu kachukuliwa baada ya kujipendekeza kwao kwa kuona hatoboi tena kisiasa achilia mbali jimbo). Read the pattern.

Kama kuna mtu wanamchukia ni JK ambaye ndiye master mind wa kuua plani yao kwa kupendekeza na kukubaliwa Mama achaguliwe mapema pamoja na mgombea mwenza wake. Hapo team 2025 ya kina HP ikawa imepaki basi golini na hakuna ujanja hadi 2030 na penginepo hadi 2040 na hata 2050. Hawana ujanja wala uwezo zaidi ya kubwabwaja mitandaoni.

JK, ambaye anamwita mstaafu mmoja, ni mtu ambaye anajuta kwa nini alimchomoa HP kwenye ki-NGO kimoja cha vijana wanaharakati alipomuona kule Ethiopia. Akamwita nyumbani akampa kazi na exposure. Ghafla tu huyu mwanaharakati mnafiki kawa mjuaji kuliko Watanzania wooooooote, hususan wana CCM. Yaani anaongea as if yeye ndiye aliyeasisi TAA, TANU na CCM, ndiye aliyemfundisha hata Nyerere siasa! Yaani CCM wote ahawjui ila yeye tu!

Nani? Huyu Polepole aliyeokotwa na JK Ethiopia na kufadhiliwa leo ndio awe hivi??? DAH! Ama kweli Yuda wako hadi leo. Kwa ufupi wala mtu asihangaike. Huyo ni Team 2025 iliyofeli na ambayo inajua wakikosa mwaka huu ndio basi tena. Akitoka Mama, nani wa kumzuia Balozi kubeba timu? Nani? Polepole? Gwajima? Mpina? Au hao walio benchi lao la ufundi (muda ukiwadia nitawataja wote na ushahidi juu) wanaohaha.

Na picha kama hii inawauma kweli unaambiwa...

Watch this space
-TarishiView attachment 3426593
Wewe ndiye mjinga na chawa wako uliouandika humu,badala ya kujibu hoja unamuatack mtu
 
Pole pole ni mnafiki Sana. Huyu ndio alipambana kuiua CHADEMA kipindi Cha Magufuli, Sasa hivi anajifanya mwanademokrasia. Very stupid guy.
Wakati Ukuta, kila mtu hubadilika kutokana na wakati. Si Busara kumhukumu mtu na yaliyopita. Yaliopita huwa ni Mwalimu mzuri. Be always positive
 
Leo amtaje kabisa aliyemuua Ben saanane..maana siku hiyo na yeye alikuwepo..!!
Ila wabongo akili zetu sijui vp, yani mkuu watu bado wanauliwa hadi sasa ila wewe bado Ben tu?
 
Agenda yake kubwa ni CCM itafute mgombea mwingine badala ya Samia. Yaani Polepole anawachapa CCM viboko vya juu ya kiuno tu, wakishika kiuno anafuta anaanza upya. #KataaWahuni #NoReformsNoElection2025
Polepole anachekesha sana anapozungumzia maneno mengi lakini anashindwa kuzungumzia hata maneno machache tu yanayohusu madaraka makubwa aliyonayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🇹🇿 aliyopewa na Katiba iliyopo 😳 !

Kwa Akili yake anajidanganya ni Nani awezaye kumfunga paka kengele ??!

🤣🤣🤣🤣🤣🤣 !

Yaelekea jamaa amedata !
Kila mtu hapa ni muoga including yeye mwenyewe ndio maana anaitisha Press akiwa Ughaibuni 😳 !

Waswahili na misemo yao Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Farao 😄😄😄😅😅 !

Mukae kwa kutulia !! 😄 !
 
Ana nguvu kiasi gani aweze kusimamisha nchi ?
Ukweli ndio wenye nguvu kuliko jeshi lolote ukiupuuza una tabia ya kulipa kisasi. Siye tunamsikiliza na kupima hoja zake ambazo kimsingi zina mashiko.
 
Ila haya mambo ya kukaa watoto wa Viongozi kwenye nafasi za uongozi inaleta Sana ukakasi wakuu,
Pamoja na kuwa Wana haki kikatiba ila hili swala ni la kutazamwa Kwa Jicho Kali sana na sio swala la ku entertain kabisa, Leo Kuna Salma kikwete na Ridhiwani wamepita Bila Kupingwa kabisa na Mzee wao Kikwete anakuja hadharani na Kuzungumza uhalali wa hilo jambo Kitu ambacho sioni kama kina afya Kwa Taifa letu
 
Back
Top Bottom