Wakuu,
Habari za mida hii ! Leo napenda kuuliza juu ya elimu ya ndugu yetu Humphrey Polepole anayehudumu kama Muenezi wa CCM mpya, ambaye awali kabla ya kuja kwenye chama chetu alijizolea sifa kadhaa katika mchakato ule wa Katiba kwa misimamo yake thabiti mpaka kupelekea kuthubutu kutamka hadharani kwamba `` Uchaguzi ukiwa huru na wa haki CCM ijiandae kukabidhi Ikulu " .
Nnahitaji kufahamu elimu yake kama ambavyo miaka ile tulivyohoji elimu ya Mh Mnyika na akaja hapa jukwaani na kutudadavulia na tukaridhika japo hoja ilitoka kwa Nape na Ridhiwani lakini woote tulishiba majibu ya Mnyika. Nadhani ni wasaa mzuri kabisa nae Bw Polepole aje atufahamishe juu ya elimu yake ili kuondoa ile dhana kwamba aliishia kidato cha 6 na kuangukia pua.
Bw wewe Polepole uje hapa jukwaani tunasubiri majibu yenye tija na sio longolongo.
Nawasilisha!
Sent using
Jamii Forums mobile app