Mimi na wewe tunakutana sehemu moja tu, kwenye kuchukia tawala ya kifisadi ya serikali ya ccm.
Ila kimtazamo tunatofautiana sana. Mfano:
Wewe unamuona Magufuli alikuwa hafai kabisa, yaani alikuwa Rais muovu, ila mimi namuona Magufuli km ni kiongozi aliyekuwa na uzalendo uliotukuka.
Pia wewe Unamuona km Lisu ni kiongozi bora ila mimi simuoni Lisu km kiongozi bora, nnamashaka na uzalendo wake. Namuona Lissu km mwanasiasa mchangamfu na mwenye uwezo wa kujieleza.
1: Alipambana kumsafisha Lowasa waliyemchafua wao wenyewe kwa kumuita fisadi papa.
2: Alishiriki kuvunja katiba ya CDM kwa kulazimisha Lowasa awe Mgombea kinyume na katiba ya chama.
3: Badala ya kumsaidia Magufuli alimpinga wazi wazi kwa kushirikiana na kina Amsterdam kwenye marekebisho ya mikataba ya madini. (Tutashitakiwa MIGA)
Kwa maana hiyo, mimi na wewe ni wapinzani wa CCM ila tunatofautiana mitazamo.