Huyu jamaa nilikuwa namheshim sana kipindi kile yuko tume ya katiba nashangaa nini kimempata leo hii haipiganii tena rasimu ile alitumia nguvu kushiriki kuiandika na kuitangaza.
Juzi kwenye mahojiano anadai eti rasimu ya warioba inafanyiwa kazi na magufuli tayari sasa najiuliza maoni kma wabunge wasiwe mawaziri limetekelezwaje na magufuli, muundo wa muungano,tume huru, maadili na miiko ya uongozi,kupunguza majimbo na nguvu za rais pia kufuta post kma za ukuu wa wilaya hizo zote zinatekelezaje ndani ya katiba ya sasa???
Hivi kweli polepole anaamini kwenye fikra wa mtu mmoja sio mfumo?? Sasa ikitokea magufuli kastaafu na kaja rais mwingine kipi kitamfunga wakati katiba mpya haipo kiuhalisia ila ipo kwenye FIKRA TU ZA MAGUFULI PEKE AKE??
Hivi kweli ina maana polepole hajui katiba ingesaidia mambo muhim ya nchi yapewe muongizo tayari ili hta aje rais dhaifu vp atabanwa tu afuate muongozo ule???
sasa nashangaa mtu aliyeamini katiba ingemdhibiti rais leo hii anaamini rais ndio anaitekeleza katiba isiyoonekana this is so low na offcially nimemfuta polepole kma mzalendo wa kweli na role modal kwenye harakati hizi za mageuzi ya kudai katiba mpya huyu amekuwa msaliti wa ndoto za mamilion ya watanzania waliotoa maoni yao kwa tume hii.