Humphrey Polepole uliwalaghai Wananchi kuichagua CCM?

Humphrey Polepole uliwalaghai Wananchi kuichagua CCM?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Ndugu wana Jf nyote ni mashahidi namna ndugu Humphrey Polepole alivyozunguka hii nchi na rais JPM kunadi na kuuza porojo kuwa kwa awamu ya tano ilani ya Ccm imetekelezwa kwa kasi na kwenye sekta ya viwanda viwanda zaidi ya 8477 vimejengwa kwenye mikoa 26 ya Tanzania.

Nimeshangazwa na kauli ya ndugu Polepole akiwa bungeni kuwa anatoa ushauri eti mawaziri wa viwanda na biashara wakae na kuangalia namna gani uzalishaji wa mafuta unakua wa kukidhi mahitaji ya sasa. Maana mpaka sasa viwanda vya ndani haviwezi kukidhi mahitaji ya ndani. Sababu kubwa ni kuwa viwanda vya ndani vinazalisha lita laki mbili wakati mahitaji ni laki tano.

Sasa huyu ndugu Polepole alipokuwa anamwaga swaga zake majukwaani kuwa hii Tanzania ya viwanda imepatikana baada ya ilani ya chama kutekelezwa kwa kasi wamu ya tano alikuwa na maana gani? Kama hata mafuta hatuwezi kuzalisha ya kutosha hii Tanzania ya viwanda ipo wapi?

Ni wazi kuwa Polepole alidanganya umma juu ya mambo mengi ili Ccm ishinde kimazabe.
 
Wanasema vimejengwa viwanda 8,000+, halafu waziri Mkuu anasema hakuna ajira vijana wajiajiri.

Uchaguzi uliopita ccm hawakutangazwa washindi kutokana na kuhubiri sera,bali madaraka ya urais yanayotumika vibaya ndio yamefanya ccm kutangazwa washindi.
 
Duh...!
 
Hakuna Mkweli ndani ya hicho Chama ni Unafiki uliopitiliza
 
Serikali ya CCM inatakiwa kuwawezesha wananchi wa taifa hili kwanza,ndio hao watafungua aina za viwanda vidogo hadi vikubwa,kwa speed kubwa.
Serikali za China,Marekani Uingereza n.k zinafanya hivyo kuwawezesha wananchi wao na kuwalinda tokana na majanga.
Shida kubwa ndani ya serikali ni watu wasio na uzoefu,na mara nyingi wanalinda ajira tu.
Labda ushauri kwa Mjomba Magu asidharau uwezo wa binadamu.Kila binadamu ana mchango wake katika maisha.
 
Good point.
 
Huyo atakua "Mnadhimu Mkuu Wa Kambi Ya Wanafiki" huko akhera na siku ya kiama.

Nchi hii hakujawahi kuzaliwa kiumbe kiongo na kinafiki na kizandiki, kama hicho. Akifa mwili wake upelekwe "MAKUMBUSHO YA TAIFA" ili vizazi vijavyo vijionee.
Chakubanga ni kizandiki, kinafiki na kilafi mno, ndio sababu kimedumaa kama NDIMU.
 
Back
Top Bottom