Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Ndugu wana Jf nyote ni mashahidi namna ndugu Humphrey Polepole alivyozunguka hii nchi na rais JPM kunadi na kuuza porojo kuwa kwa awamu ya tano ilani ya Ccm imetekelezwa kwa kasi na kwenye sekta ya viwanda viwanda zaidi ya 8477 vimejengwa kwenye mikoa 26 ya Tanzania.
Nimeshangazwa na kauli ya ndugu Polepole akiwa bungeni kuwa anatoa ushauri eti mawaziri wa viwanda na biashara wakae na kuangalia namna gani uzalishaji wa mafuta unakua wa kukidhi mahitaji ya sasa. Maana mpaka sasa viwanda vya ndani haviwezi kukidhi mahitaji ya ndani. Sababu kubwa ni kuwa viwanda vya ndani vinazalisha lita laki mbili wakati mahitaji ni laki tano.
Sasa huyu ndugu Polepole alipokuwa anamwaga swaga zake majukwaani kuwa hii Tanzania ya viwanda imepatikana baada ya ilani ya chama kutekelezwa kwa kasi wamu ya tano alikuwa na maana gani? Kama hata mafuta hatuwezi kuzalisha ya kutosha hii Tanzania ya viwanda ipo wapi?
Ni wazi kuwa Polepole alidanganya umma juu ya mambo mengi ili Ccm ishinde kimazabe.