Miami magnificent humu ndani! Ila zamani nilikuwa na "access " jf kwa sumu yangu ya techno 360, nilikuwa navutiwa sana na mijadala ya humu na mala nyingine nilikuwa natamani sana kuwa mchangiaji wa baadhi ya maada bahati mbaya simu yangu ilikuwa ndogo! Nakumbuka Luna siku nilishinda njaa nikitaka kuwa na account jf kwa simu yangu ndogo nakashindwa na baadaye nikaenda kwa jama yangu mwenye smartphone anifungulie account kwa simu yake aliniambia kuwa tayari nimefungua lakini nikitaka log in siioni nilihuzunika sana ! Luna muda nilianza kuwa na mahaba makubwa sana juu ya member wa jammiiforums, nikawa najiuliza maswali mengi sana; Hivi hawa watu wanafananaje mtaani? Na jee wanaishi haswa wapi?mbona wanajua mambo mengi sana? Any way hadi sasa sijawahi kumuona member ata mmoja mwenye icon ya Jf ! Ila nawaza sana juu ya udugu ulioko jf. Pia ningependa kama hamtajali, member tuwe na ishara zetu mtaani ili tuupanue udugu! Na pia kama hamtojali tuwe na sherehe yetu wana jf ambayo itategemea mipango yetu! Nawapenda sana wanajf