Humu ndani kuna babu na bibi zetu tuheshimiane

Humu ndani kuna babu na bibi zetu tuheshimiane

Wakuu habari na poleni na hili janga la COVID-19.

Jana mimi kama Mchimba Chumvi niliweka tangazo humu la kuuza sim yangu na nilifanikiwa kwa asilimia 1000.

Sasa bwana jioni nilifanikiwa kupokea simu ya mtu analiedai hii anaitaka hii simu kiukweli hakua na mengi zaidi ya kunielekeza alipo tuonane anununue simu tofauti na wengine.

Leo asubuhi nikamuibukia mpaka eneo hilo,kiukweli ninavyoongea nae kwa simu alisound kama father fulani hivi .
Nilivyofika eneo la hilo nikampigia akaniambia bado hajafika eneo hilo nimsubiri, punde akanipigia aisee kugeuka nikamuona nilipigwa na butwaa ni mzee sana kama +65yrs hivi anyway tukafanya biashara .

Vijana hasa sisi early 20's humu tupo na zaidi ya wazazi wetu humu,tuheshimiane hata kama usimheshimu mtu kwa I'd yake, nimestaajabu sana kumuona huyu mzee ambaye kaniambia alijiunga jf 2010 na vile tunavyojibizana humu.

Shikamoo mkuu japo hujanitajia I'd yako ikiwa yangu unaijua.
Heshimu kila mtu you never know.

Uzi tayari.
Kama hao babu na bibi wakiwa wajingawajinga basi wataoga matusi kama kawaida...
 
Back
Top Bottom