Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Wengi tunaamini wale watu wanaotuzunguka katika mazingira yetu ya kila siku ndio marafiki wa kweli; iwe tunakutana nao maeneo ya starehe kama bar, sehemu za miziki, harusini, au sherehe yoyote; iwe tunakutana nao makazini, idarani, chamani n.k; iwe tunakutana nao misibani, mahospitalini n.k, iwe tunakaa mtaa mmoja, majirani n.k
Ila ukweli wale sio marafiki, bali ni watu wakubadilishana nao tu mawazo kutokana na mazingira mliopo. Watu wengi hukosea na kuamini watu wanaokutana nao katika mazingira hayo wanaweza kuwa marafiki wa kweli; ila ukweli unakuja kugundulika baada ya kuangukia pua, pale utakapowahitaji na hawatakuwepo, zaidi ya wewe mwenyewe kupambana na hali yako na haijalishi uliwekeza kiasi gani kwao.
Kwa kifupi kupata rafiki wa kweli, ni mchakato mrefu sana zaidi ya unavyotafuta mchumba; ambaye mtafanana mitazamo, ambaye wewe ukisema ‘yes’ naye atasema ‘yes’ akisema ‘no’ naye atasema ‘no’.
Na hii itapelekea kuwa na umoja wenu kutokana na idadi mliopo, mfano; ‘the big three’, ‘the big five’ n.k
Kuna video moja ilirekodiwa hospitali moja huko nje, jamaa amelazwa hospitalini anapumulia oxygen, marafiki zake wamekuja kumuona hapo hospitalini, wahudumu wakawa wanawaambia muda wa kumuona mgonjwa umeisha mnatakiwa muondoke; wale marafiki zake walikataa, wakasema tutakaa naye hapa hapa mpaka dakika ya mwisho na hatutaondoka, kama kuna mahitaji yoyote yanatakiwa yapatikane, yatakuja wao wakiwa pale pale.
Je hao wasaka tonge wako ulionao, wataweza kuwa kama hao marafiki wa jamaa?