Huna marafiki wa kweli, tusidanganyane

Huna marafiki wa kweli, tusidanganyane

Wengi tunaamini wale watu wanaotuzunguka katika mazingira yetu ya kila siku ndio marafiki wa kweli; iwe tunakutana nao maeneo ya starehe kama bar, sehemu za miziki, harusini, au sherehe yoyote; iwe tunakutana nao makazini, idarani, chamani n.k; iwe tunakutana nao misibani, mahospitalini n.k, iwe tunakaa mtaa mmoja, majirani n.k

Ila ukweli wale sio marafiki, bali ni watu wakubadilishana nao tu mawazo kutokana na mazingira mliopo. Watu wengi hukosea na kuamini watu wanaokutana nao katika mazingira hayo wanaweza kuwa marafiki wa kweli; ila ukweli unakuja kugundulika baada ya kuangukia pua, pale utakapowahitaji na hawatakuwepo, zaidi ya wewe mwenyewe kupambana na hali yako na haijalishi uliwekeza kiasi gani kwao.

Kwa kifupi kupata rafiki wa kweli, ni mchakato mrefu sana zaidi ya unavyotafuta mchumba; ambaye mtafanana mitazamo, ambaye wewe ukisema ‘yes’ naye atasema ‘yes’ akisema ‘no’ naye atasema ‘no’.

Na hii itapelekea kuwa na umoja wenu kutokana na idadi mliopo, mfano; ‘the big three’, ‘the big five’ n.k

Kuna video moja ilirekodiwa hospitali moja huko nje, jamaa amelazwa hospitalini anapumulia oxygen, marafiki zake wamekuja kumuona hapo hospitalini, wahudumu wakawa wanawaambia muda wa kumuona mgonjwa umeisha mnatakiwa muondoke; wale marafiki zake walikataa, wakasema tutakaa naye hapa hapa mpaka dakika ya mwisho na hatutaondoka, kama kuna mahitaji yoyote yanatakiwa yapatikane, yatakuja wao wakiwa pale pale.

Je hao wasaka tonge wako ulionao, wataweza kuwa kama hao marafiki wa jamaa?​
Hivi kwa mfano uko wapi nikupe bia 5 za faster kwa kuongea ukweli..... kwa wastani unaweza kuwa na marafiki wa kweli lakini hawawezi kuzidi 3
 
98% of the people in our life comes for reasons eg your work mate school mate
1% for season eg certain projects
1% for life time eg family

Think twice.
 
Kwa mazingira hayo, rafiki wa kweli anaweza kupatikana vipi?
 
Marafiki wa kweli wanatengenezwa kipindi tukiwa wadogo tuliosoma nao primary school tuliokuwa nao mtaa mmoja kiufupi real friends comes from nothing they are not interested in what we have money education status quo etc.
 
Inategemea na tafsiri yako katika huo urafiki, na kipimo ulichojiwekea.
Siwezi kuupima urafiki kwa mtihani ambao hata mzazi wangu anaweza kufeli. Mfano kuna mdau hapo kaongelea suala la figo, hilo ni jambo kubwa ambalo hata wazazi/watoto wanaweza kufeli( ndio maana watu wanakufa kiss figo wakati wana watoto/wazazi)

Kwangu Mimi urafiki wa kweli ni wakutakiana kheri na sio Shari. Rafiki wa kweli hana husda wala roho ya kukunja. Rafiki wa kweli hana fitna wala uongo. Mengine ni madhaifu ya kibinadamu tunasameheana.
Mimi ninaye Rafiki wa kweli. Kwangu Mimi ni kawa zaidi ya Rafiki.
Dear E, kama upo hapa, tambua ninakupenda na kukuthamini. Wewe ni rafiki wa kweli. Pokea maua yako.
Ni dalili ya mtu mwenye gubu na entitled. Figo kabisa ye kuweza? Anatafuta kulaumu watu tu.
 
Wengi tunaamini wale watu wanaotuzunguka katika mazingira yetu ya kila siku ndio marafiki wa kweli; iwe tunakutana nao maeneo ya starehe kama bar, sehemu za miziki, harusini, au sherehe yoyote; iwe tunakutana nao makazini, idarani, chamani n.k; iwe tunakutana nao misibani, mahospitalini n.k, iwe tunakaa mtaa mmoja, majirani n.k

Ila ukweli wale sio marafiki, bali ni watu wakubadilishana nao tu mawazo kutokana na mazingira mliopo. Watu wengi hukosea na kuamini watu wanaokutana nao katika mazingira hayo wanaweza kuwa marafiki wa kweli; ila ukweli unakuja kugundulika baada ya kuangukia pua, pale utakapowahitaji na hawatakuwepo, zaidi ya wewe mwenyewe kupambana na hali yako na haijalishi uliwekeza kiasi gani kwao.

Kwa kifupi kupata rafiki wa kweli, ni mchakato mrefu sana zaidi ya unavyotafuta mchumba; ambaye mtafanana mitazamo, ambaye wewe ukisema ‘yes’ naye atasema ‘yes’ akisema ‘no’ naye atasema ‘no’.

Na hii itapelekea kuwa na umoja wenu kutokana na idadi mliopo, mfano; ‘the big three’, ‘the big five’ n.k

Kuna video moja ilirekodiwa hospitali moja huko nje, jamaa amelazwa hospitalini anapumulia oxygen, marafiki zake wamekuja kumuona hapo hospitalini, wahudumu wakawa wanawaambia muda wa kumuona mgonjwa umeisha mnatakiwa muondoke; wale marafiki zake walikataa, wakasema tutakaa naye hapa hapa mpaka dakika ya mwisho na hatutaondoka, kama kuna mahitaji yoyote yanatakiwa yapatikane, yatakuja wao wakiwa pale pale.

Je hao wasaka tonge wako ulionao, wataweza kuwa kama hao marafiki wa jamaa?​
Rafiki wa kweli ni njaa ambaye anani beep kwenye shida
 
Back
Top Bottom