Huna marafiki wa kweli, tusidanganyane

Huna marafiki wa kweli, tusidanganyane

Urafiki ni kitu kizito sana na urafiki sio ukisema ndio na yeye aseme ndio. Urafiki sio kukubaliana kwa kila kitu bali kuambiana ukweli hata kama unamkera mwenzio kwa sababu unachojali ni maendeleo yake zaidi kuliko atajihisije.

Urafiki ni kufurahia maendeleo ya mwenzako genuinely hata kama anakupita

Urafiki ni kujitoa, urafiki ni kutokuhesabiana fadhila, urafiki ni bond kubwa kwa mtu ambaye hamna uhusiano wa damu.

Ukipata rafiki kwa maisha haya ni achievement kubwa japo ni kheri usiwe nao kuliko kuwa nao ambao si sahihi

Urafiki upowa kweli upo ila ni nadra kuupata
Na kwanini inakuwa ni nadra kuupata?
 
Tena ambao hawana shughuli ya kufanya. Huwezi kaa masaa yote hayo hospitali eti kisa urafiki, hata kama mmeshibana kiasi gani utaondoka kwenda kufanya shughuli zako huku ukiendelea kumjulia hali.
Inategemea na mifumo yako ya uchumi ulivyoi-set wapo amabao ata wasipokuwepo kwenye ofisi zao pesa zinaendelea kujizalisha, mfano 'youtubers'
 
 
Na kwa nini uwe wa utotoni tu, huku ukubwani ni nini kilichowabadilisha?
 
Urafiki siku hizi ni wa mchongo
Kabisa,lets meet nipe dili za mahela upite hivi

Urafiki wa sikuhizi ni wa kuliana wake 🤣🤣🤣

Wazazi wetu walikuwa wanakaribishana nyumbani na kutambulisha wake zao...ila sikuhizi DAAAH...wanapeana namba mchezo umeisha
 
Kabisa,lets meet nipe dili za mahela upite hivi

Urafiki wa sikuhizi ni wa kuliana wake 🤣🤣🤣

Wazazi wetu walikuwa wanakaribishana nyumbani na kutambulisha wake zao...ila sikuhizi DAAAH...wanapeana namba mchezo umeisha
Ni kuwa makini tu,marafiki uua
 
Kwa marafiki ulionao sasa, leo hii uko hospitali una miezi mitatu umelazwa ni yupi atakayekuwa bega kwa bega na wewe?
Ninae mmoja, naamini atafanya hivyo lakini sio kwa kukesha na mimi hospitali maana ana kibarua chake lazima mambo mengine kwa upande wake yaendelee.

Mwanaume kama huna mke wa kukutunza usitegemee ndugu zako au marafiki zako waje wakuhudumie hospitali. So hawa kataa ndoa ingawa wanayo hoja wasikilizwe wanatakiwa kuwa na hela ya kutosha incase wameugua waweze kuajiri mtu wa kuwasafisha na kuwabadilisha diapers.

Kwa upande wa wanawake hakikisha una watoto wa kike wa kukuhudumia.
 
Back
Top Bottom