Huna marafiki wa kweli, tusidanganyane

Hata Ndugu au Marafiki wanaweza kufanya hivyo 🤣
Ata undugu siku hizi ni wamchongo tu 😀 ; ndio maana wazee wakizungu wanatafuta vijana wadogo wakiafrika ili waoane na kumalizia maisha yaliyobaki.
 
KATAA NDOA WANAKUJA
 
Wengine wameoa na kukimbiwa na wake walipokuwa wagonjwa na hela zimekata. Wengine wamezaa watoto lakini wametelekezwa na watoto wao.

Hii dunia ina mambo ya kustaajabisha.
 
Wengine wameoa na kukimbiwa na wake walipokuwa wagonjwa na hela zimekata. Wengine wamezaa watoto lakini wametelekezwa na watoto wao.

Hii dunia ina mambo ya kustaajabisha.
Ni kweli inatokea lakini mara chache. Wanawake wengi huwatunza waume zao. Na watoto wengi wa kike huwatunza mama zao katika hali ya ugonjwa.
 
Ni kweli inatokea lakini mara chache. Wanawake wengi huwatunza waume zao. Na watoto wengi wa kike huwatunza mama zao katika hali ya ugonjwa.
Tunahitaji marafiki, ndugu na watoto. Unaweza kulazwa hospitali na una mke lakini asiweze kukuhudumia sababu yulo kwenye wodi za wanaume. Watoto vile vile. Na ugonjwa wa muda mrefu mke hawezi peke yake.
Sisi wifi yetu aliugua mwaka mzima sisi ndio tulikuwa tunamhudumia, na hata akahamia kwa dada yangu maana mume asingeweza peke yake.
Dada yangu vile vile tulikuwa tunamhudumia maana watoto walikuwa shule. Mume yupo lakini hakuweza kumhudumia wodini.
Kaka yangu alihudumiwa na sisi maana mke wake alitanguliq kufa na watoto wako mbali na hospitali ya Muhimbili.
 
Upo sahihi. Mume akiwa wodini inakuwa vigumu mke kumuhudumia ingawa atakuwa anafanya shughuli nyingine kama kuleta chakula. Pia inategemea na wodi, kama ni private basi mke anaruhusiwa maana mgonjwa anakuwa peke yake.

Pia kama ni ugonjwa wa muda mrefu mgonjwa atakuwa nyumbani.
Haya mambo hayatabiriki lakini kwa mmazoea tunavyoona wanawake ndo wanaolea wagonjwa zaidi.
 
Na kwanini inakuwa ni nadra kuupata?
1. Nimekuja kujua kuwa watu wengi tu hawana roho nzuri na wenye roho nzuri za kujitoa huwa wanachukuliwa kama mazoba au boring kuwa kwenye kampani yao. Hivyo, watu wengi wanachagua wale wanaoona wapo na vibe haswa za kutoka na si ajabu mmoja akiharibikiwa, anaekuja kumsaidia ni yule wanaemuona kapoa, ana Mungu sana au kazubaa. Ila wengi ndo huwa wana moyo mzuri. Hivyo ukiona mtu kama huyu hata kama hamuendani hobby, muweke pembeni kwa sababu wengi wao huwa loyal sana.

2. Unless umepata rafiki wa kitambo hicho hamjui hata kutafuta pesa na mkaendana kwa vingi hadi mkatengeneza bond kubwa. Huku ukubwani ni ngumu kutengeneza hizo bonds aidha ni kazini au bar kwa sababu kila anaekusogelea, huwa ana maslahi yake kichwani hivyo anatumia urafiki fake ili kuendelea kufaidika na wewe kirahisi. Ila, siku ikifika muda wao wa kukusaidia huwa wanayeyuka. Na hii ubaya ipo popote ikiwepo mahusiano..


Kwa hiyo kama unatafuta rafiki ukubwani, tafuta mtu mwenye huruma na watu. Yani kuna wale watu ambao huwa ni wema, wana hekma, wasiri na huwasaidia watu bila kutaraji chochote in return. Hao ndio watu wanaweza kuwa na utu wa kukupenda wewe kama binadamu na sio kwa sababu unawafaidisha kwa kitu fulani

Kwa hiyo tafuta bond nao, iwe kwa kazi au social activities lakini kikubwa na wewe uwe real, sio unatafuta urafiki ambao binafsi huwezi kuutoa. Kuwa real, tafuta mtu mwema. Hapo urafiki utamea
 
Wengine wameoa na kukimbiwa na wake walipokuwa wagonjwa na hela zimekata. Wengine wamezaa watoto lakini wametelekezwa na watoto wao.

Hii dunia ina mambo ya kustaajabisha.
Wengi wasichokijua ni kuwa uhalisia wa vitu huwafika watu pale jambo linapowakuta. Sio kwa hizi story story

Kuna watu wanaugua lakini wanatelekezwa kiasi wanatunzwa na majirani na marafiki

Kuna wengine walikimbiwa na marafiki Ila mke na watoto wakasimama. Na kuna wengine walitengwa na kila mtu. Hakuna watoto, ndugu au marafiki

Ndio zile unaenda msibani majirani wanalalamika kuona msiba wa kifahari Ila muhusika alifariki peke yake ndani bila msaada wowote. Dunia hii ni kumuomba Mungu tu
 
Inategemea na tafsiri yako katika huo urafiki, na kipimo ulichojiwekea.
Siwezi kuupima urafiki kwa mtihani ambao hata mzazi wangu anaweza kufeli. Mfano kuna mdau hapo kaongelea suala la figo, hilo ni jambo kubwa ambalo hata wazazi/watoto wanaweza kufeli( ndio maana watu wanakufa kiss figo wakati wana watoto/wazazi)

Kwangu Mimi urafiki wa kweli ni wakutakiana kheri na sio Shari. Rafiki wa kweli hana husda wala roho ya kukunja. Rafiki wa kweli hana fitna wala uongo. Mengine ni madhaifu ya kibinadamu tunasameheana.
Mimi ninaye Rafiki wa kweli. Kwangu Mimi ni kawa zaidi ya Rafiki.
Dear E, kama upo hapa, tambua ninakupenda na kukuthamini. Wewe ni rafiki wa kweli. Pokea maua yako.
 
Kuna cha kujifunza hapa
 
Watu wanaongea kinadharia lakini uhalisia mambo hayako hivyo
 
Hivi kumbe kuna wanaume wapo bizy kutafuta marafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…