Huna Wajibu wa kumtunza au kumhudumia Mzazi wako akiwa chini ya miaka 60 kama haumwi

Huna Wajibu wa kumtunza au kumhudumia Mzazi wako akiwa chini ya miaka 60 kama haumwi

Unajua kusoma sana siyo kuelimika. Naweza kusema mleta mada kasoma lakini inaonekana hajaelimika Bali kaathiriwa na vyeti vya darasani.

Kipi kinakufanya uache kumhudumia na kumtunza mtoto wako akishakua?
Watu kama nyie huwaga najua hamwezi kujenga hoja kutetea upande mliopo.
 
Soma vizuri mkuu unielewe.
Sijasema mtu asisaidie kwao au wazazi.
Afanye kwa hiyari au mapenzí kwa wazazi ambao hawajazeeka.

Kuna wazazi wanatumia vibaya uzazi wao kudhulumu haki za watoto.
Kama ilivyo kuna watoto wanatumia utoto wao kudhulumu haki za wazazi wao
Kukuelewa itakua ngumu sabab wanahisi huo ni wema na baraka.

Kwanza kumsaidia mtu yoyote ni muhimu kama unaweza kufanya hivyo ila siku hiz kuna huo ukiritimba wazaz wananguvu ya kudanya kazi na kujitafutia lakini wanamtegemea mtoto,mfano kuna jirani yangu hapa yeye umri mdogo lakini ataki kufanya kazi anasema amezaa watoto wa kazi gani.Bahati mbaya watoto hawajajipata lakini mzazi kutwa kutaka marejesho hii hata mungu anaikataa.

UMEONGEA VIZURI SANA ILA HUWEZI KUELEWEKA SABAB TULIO WENGI MIOYO NDO HUFANYA KAZI SIO AKILI
 
HUNA WAJIBU WA KUMTUNZA AU KUMHUDUMIA MZAZI WAKO AKIWA CHINI YA MIAKA 60 KAMA HAUMWI.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mada hii inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya Watu. Lakini nitakachojadili hapa ni Haki, kweli, akili na upendo kama ilivyo kwa Watibeli wote.

Kama ilivyo kwa mzazi hana wajibu wa kukutunza na kukuhudumia pindi ufikishapo umri wa kujitegemea yaani kuanzia miaka 21 hivi kwa sisi Watibeli. Na kwa sheria za dunia ni miaka 18. Basi ndivyo hivyohivyo kuwa mtoto hana wajibu wa kumtunza na kumhudumia mzazi au mlezi ambaye yupo chini ya miaka 60 ambaye HAUMWI(hana tatizo la kiafya).

Kuna kijitabia fulani cha kinyonyaji, dhulma, uvivu, na ukandamizaji ambao unafanywa na wazazi kwenda kwa watoto wao. Ambapo mzazi anazaa watoto idadi fulani anawapa na kuwatunza(wajibu wake) alafu wakishafikisha miaka 20 tuu wakaenda kujitafutia basi inakuwa nongwa. Mzazi hata miaka 50 haujui, miaka 60 ndio kabisa hatarajii leo wala kesho kuifikia. Mzazi ananguvu kabisa lakini kutwa kusumbua watoto na kuwatia watoto katika shinikizo isivyostahili.

Sio jukumu la mtoto kukulea na kukutunza ukiwa na umri huo. Wewe bado upo umri wa kujitegemea na kujihudumia. Kwa nini umpe mtoto mzigo? Kwa nini umdhulumu mtoto haki zake?
Kama sababu ni kuzaa na kumtunza hata yeye atazaa na kutunza watoto wake.

Kama ishu ni wajibu basi subiri muda ukifika mtoto atekeleze wajibu wake. Na kama atakutunza au kukuhudumia iwe kwa uwezo na mapenzi yake kwako na shukran na sio shinikizo.

Ni laana kubwa kumhudumia mtu isivyo halali. Kuhudumia mzazi kwa kushinikizwa yaani kunyonywa na kudhulumiwa ni laana ambayo wengi inawatafuna.

Sio ajabu unakuta Watu wengi tangu wakiwa vîjana wanateseka kuhudumia wazazi isivyostahili wakifikiria ndio baraka lakini miaka inaenda maisha yao hayabadiliki zaidi ya kuzidi kuwa maskini na fukara zaidi.

Ni sawasawa na mzazi amuone mtoto keshafikia umri wa kujitegemea alafu bado awe anamhudumia na kumtunza huo ni umaskini wa akili na roho. Lazima kizazi hiki kiwe fukara.

Ninajua ndoa nyingi zilizoharibika na familia nyingi kuanguka kisa wazazi kushinikiza huduma. Ni laana tupu. Wakati huo wazazi wananguvu kabisa.
Ninajua mabinti wengi wanaoteseka kwenye ndoa kisa wazazi wao wamewashinikiza watoto wao wabaki kwenye mateso ili wao wanufaike au walishanufaika na kumuuza binti yao.

Wengine huwashinikiza binti zao waolewe na wanaume wenyewe pesa hata kama hawapendwi na binti zao kwa kulenga kuhudumiwa na pesa za mkwilima wao.

Wapo vibinti vya kazi za ndani wanalipwa mishahara kiduntu kama elfu 30 mpaka 60 na bado wazazi wanataka gawiwo licha ya kuwa wazazi hao bado kiumri wanauwezo wa kufanya kazi na kujitafutia.

Wapo wazazi kiumri ni wadogo lakini wanawakosea watoto wao haki kwa kuwashinikiza watoto wao kwa matusi na kejeli kuwa hawafanyi kazi huko mjini kisa tuu hawatumiwi pesa. Jambo ambalo sio Haki na sio Upendo.
Wapo watoto wanajitutumua kuhakikisha wanahudumia wazazi wao kiugumuugumu, kwa kujikamua, na malalamiko ya nafsi wazazi kwa ubinafsi wao huona ni sahihi lakini sio sahihi kabisa.

Acheni watoto wakiwa na umri wa kujitafutia watafute na kujitegemea alafu wao kwa roho ya upendo wawatumie kwa hiyari yao na sio kuwadhulumu maisha na nguvu zao.

Watoto pia, acheni kudhulumu nguvu za wazazi wenu huku mkujua kuwa tayari mmefikia umri wa kujitegemea na sio kuwapa wazazi wenu mzigo, kuwanyonya na kuwakatili.
Mzazi asifurahie utu uzima wake aanze kukufikiria mtu mzima na ndevu zako kisa ati ni mtoto wake. Hiyo sio HAKI

Kumhudumia mzazi wako aliyemzee sio hiyari yako wala sio mapenzi yako kwake. Hiyo ni lazima, wajibu.
Bahati nzuri wazee hawana mahitaji mengi kama ilivyo kwa watoto.

Lakini kuhudumia mzazi aliyechini ya miaka 60 na haumwi hiyo ni hiyari na mapenzi tuu na sio lazima/wajibu. Unaweza ukafanya au usifanye na hakuna lolote litakupata.

Kumhudumia mtu anayeweza kujitegemea ni laana na kurudisha nyuma kizazi na ukoo wenu.
Lazima Watu wafanyekazi na wawajibike kwa maisha yao na ya wale wanaowahusu.

Huo ndio Utibeli. Ukweli, haki, upendo na Haki
Mimi nimemaliza, mwenye maswali anaweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mkuu nimesoma uzi kwa makini nimeona una hoja usipuuzwe,,
Miaka 60--50 sio mzee kwwnn uwe tegemezi?

Point ya mleta mada ilikuwa ni kuwapa alert call wale wazazi wote ambao hawajafikia umri wa kuchoka na hawajishughulishi kutafuta pesa wao kazi yao ni vizinga na kusumbuwa watoto wao..

Haiwezekani mzazi ana miaka 50 --60 anaona tayari ameshazeeka na anahitaji kuwa tegemezi kwa watoto wake..

Wazee wenzangu na wazee watarajiwa tunatakiwa tusibweteke wala kujiona tumeshazeeka kwenye umri wa miaka 50-60.

Tuendelee kupambana hadi kieleweke.,tufanye kazi Kwa bidii na tuandae maisha yetu ya baadae ili.kuepuka usumbufu kwa watoto wetu..

Mleta post ana kitu huyu asipuuzwe..
 
Kama watoto wenyewe ndiyo hawa akina Mtibeli alafu ndiyo tuwategemee waje watusitiri tukizeeka tuhesabu maumivu tu Wazee wenzangu.

Ndiyo maana nimefungua akaunti yangu ya Siri, najiwekea hela zangu ili kuepusha aibu ya kudharilishwa na Watoto tunaotegemea watupe Faraja Uzeeni.

Kama nitakufa mapema bora wale watu wa Benki tu 🥲
😁
 
Nashukuru sana kwa kunielewa mkuu.
Barikiwa
 
Hawa ni wale wa single mother/father kwa hiyo wamekuwa psychologically affected. Mzazi wako hata km ana pesa, kumpa vocha/pesa ya chakula au kumnunulia gari au zawadi yoyote ni kuongeza upendo na baraka. Uzungu anaozungumzia mleta mada awafanyie tu wazazi wake aache kurubuni na wengine.
Sijui kwanini wabongo sio waelewa, kumpa zawadi ni tofauti na kumuhudumia. Siku upo vizuri umejisikia tu ukamtumia muamala tigopesa ni tofauti na kumuhudumia. Labda nikupe mfano Mimi hapa mama angu hafanyi kazi namuhudumia mimi, nafanya yafuatayo
1. Nimemjengea nyumba anaishi hapo
2. Bills zote za hapo nyumbani nalipa mimi, umeme na maji
3. Pesa ya chakula hapo nyumbani mimi ndo mtoaji, nimemuwekea bajeti Kila mwezi namtumia almost laki 4.
Huko ndo kuhudumia, achana na zawadi unazotoa mara moja Kila baada ya miezi miwili au mitatu.
Sasa mtibeli anasema wajibu wa kumuhudumia mzazi kama hana changamoto ya kiafya basi ni kuanzia miaka 60.
 
Tatizo la watanzania ni kutojifanya hawaelewi wakati mambo yako wazi.
Kitu kinaeleweka lakini wanakifanya kionekane hakieleweki.
 
Achana na sheria ndugu, nenda kwenye uhalisia. Hujui wakati mwingine sheria humnyima mtu haki maana zinatungwa kwa malengo kuumiza wengi na kufurahisha wachache. Umewahi kuskia mtu kaua hadharani lakini kashinda kesi.

Achana na mambo ya kwenye makaratasi, nenda kwenye vitendo.
Sheria sio makaratasi ni mtindo wa maisha uliokubalika kutumiwa na wanajamii....
 
Nashukuru sana kwa kunielewa mkuu.
Barikiwa
Inaonekana wazee wengi humu JF kazi yao ni vizinga na kusumbuwa watoto wao hata kama umri wao wa kuchoka haujafika.

Tupambane na kutafuta maisha Mungu hajaweka limit ya umri wa kutoa riziki..
 
Kwanini wazazi wa Afrika ndo hupenda lelewa?
 
Nimesoma tu heading nikagundua mtoa mada ni mtu ambae hamnazo.!

Ni mtu ambae kila anachokifikiria kichwani kwake anakiona Cha kukileta mbele ya jamiii na kujiona genius.

Usipowapa furaha wazazi wako unataka kuwapa wakina nani.?? Maisha ni Nini kwako kama unajiweza na huku ukiwapa kisogo wazazi wako eti tu kisa wapo chini ya miaka 60.

saidia wazazi wako kwa kile ulicho nacho Wala hutapungukiwa chochote na zaidi baraka zitaongezeka katika utafutaji wako.!

Usisubiri mzazi afe ili uje kuonyesha fahari katika mazishi mbele ya jamii na marafiki WA kazini kwako

Note.
Maisha ni mafupi sana Miaka inaenda kama upepo siku si nyingi na sisi tutakuwa wazee kama walivyo wazazi wetu. Tusaidie ndugu na jamaa zetu

Nb.taikon WA fasihi ni mtoto mdogo Ambae hajui maisha yanataka nini. Yeye anajua mtu ukishapata Hela basi imeisha unafanya unavyoweza.kumbe sio kweli Kuna sehemu Hela na umaarufu havifiki

Be humble mzee sio Kila kitu Cha kuandika mtandaoni ' WE zombie.
Alichoandika naona hujakielewa pengine urudie mstari kwamstari

Yuko sahihi unamuhudumiaje au kumtunza dingi au motheri Yuko chini ya miaka 60 nyie ndio mnafanya jamii iwe ya kivivu tamalaki na hawaumwi

Labda kidogo miaka 60+ napo liwe jukumu la gvt zetu
 
Mimi napenda Haki, ukweli, akili na upendo.

Huwezi elewa ninachoandika mpaka uongozwe na hayo mambo manne.
Unachoandika makes sense lakini you are making an assumption ya familia zote kuwa Sawa which is not correct ! Kwa familia nyingi za kiafrika kumsomesha mtoto mpaka aanze kufanya kazi familia inakuwa imeuza kuku, mifugo na mazao ili kumuwexesha mtoto kusoma hivyo huo unakuwa aina ya uwekezaji!! Na unapowekeza you expect return on your investment.! Hivyo watoto kuwasaidia wazazi wao irrespective of their age ni wajibu wao.
 
Nimesoma tu heading nikagundua mtoa mada ni mtu ambae hamnazo.!

Ni mtu ambae kila anachokifikiria kichwani kwake anakiona Cha kukileta mbele ya jamiii na kujiona genius.

Usipowapa furaha wazazi wako unataka kuwapa wakina nani.?? Maisha ni Nini kwako kama unajiweza na huku ukiwapa kisogo wazazi wako eti tu kisa wapo chini ya miaka 60.

saidia wazazi wako kwa kile ulicho nacho Wala hutapungukiwa chochote na zaidi baraka zitaongezeka katika utafutaji wako.!

Usisubiri mzazi afe ili uje kuonyesha fahari katika mazishi mbele ya jamii na marafiki WA kazini kwako

Note.
Maisha ni mafupi sana Miaka inaenda kama upepo siku si nyingi na sisi tutakuwa wazee kama walivyo wazazi wetu. Tusaidie ndugu na jamaa zetu

Nb.taikon WA fasihi ni mtoto mdogo Ambae hajui maisha yanataka nini. Yeye anajua mtu ukishapata Hela basi imeisha unafanya unavyoweza.kumbe sio kweli Kuna sehemu Hela na umaarufu havifiki

Be humble mzee sio Kila kitu Cha kuandika mtandaoni ' WE zombie.
mi simuelewagi sana huyu jamaa,ujinga wowote unaokuja kichwani anauandika tu
 
Kama watoto wenyewe ndiyo hawa akina Mtibeli alafu ndiyo tuwategemee waje watusitiri tukizeeka tuhesabu maumivu tu Wazee wenzangu.

Ndiyo maana nimefungua akaunti yangu ya Siri, najiwekea hela zangu ili kuepusha aibu ya kudharilishwa na Watoto tunaotegemea watupe Faraja Uzeeni.

Kama nitakufa mapema bora wale watu wa Benki tu 🥲
Usitegemee watoto wakupe furaha, wewe ndio unatakiwa kuwapa furaha watoto
 
Back
Top Bottom