Tony 254, nchi inapokumbwa na njaa kali hadi kusababisha vifo, maana yake ni kwamba, kuna watu wengi hawana uwezo wa kupata chakula, hii haimaanishi chakula hakipo mchini tu, bali ni kwamba wananchi wengi hawana uwezo hata wa kununua chakula kama kipo, wakati mwengine hata ukiwapa chakula, hawana uwezo hata wa kupika hicho chakula kwa kukosa kuni au fuel ya kupikia, ndiyo sababu katika hali hiyo, watu hao hupelekewa vykul vya kwenye makopo ambavyo hawahitaji kupika.
Kenya pamoja na kununua mahindi toka Mexico/South Africa, bado jamii za wafugaji wa Turkana, Pokot, Wajir na kwengneko walihitaji kupewa vyakula vya bure kwasababu hawakuwa na uwezo hata wa kununua nusu lita ya mafuta ya kupikia, hivyo wasingeweza kununua mahindi ya Mexico. Kenya ulilazimika kuomba na kupokea msaada wa mahindi ili kuwapa bure bila malipo famili nyingi zilizokua hatarini kufa kwa njaa.