Wanajeshi wa Rwanda wanawahudumia wanajeshi wa Kongo wanaokimbilia Rwanda, ambao ni majeruhi wa vita. Jana, walipewa chakula, maji, na juisi. Licha ya yote, hawaonyeshi hasira wala kinyongo kwa kile ambacho serikali yao imewaambia.
Rwandan soldiers are treating Congolese soldiers fleeing to Rwanda, who were casualties of the war. Yesterday, they were provided with food, water, and juice. Despite everything, they show no anger or resentment toward what their government has said about them.
View attachment 3216496
Huu vita ni mtaji mkubwa kwa watawala mafisadi wa Afrika .
Kagame ndiye mwenye nia njema ya kulinda watu wa Kongo na Rasilimali zao .
Iko hivi Wazungu wapo Kongo kuiba mali na rasilimali za Kongo .
Wezi hao wa nchi za magharibi wanasaidiana na marais mafisadi kulinda wizi huo kwa kupeleka Majeshi Kwenda kulinda hao majizi toka ulaya .
Kongo ni eneo la dili la watawala wasioweza kutunza majeshi yao kwenye nchi zao hivyo wanawapeleka Kongo kwa ajili ya kwenda kupata fedha za kuendesha maisha ya wanajeshi . Hali hiyo haiwezi kumaliza vita Kongo kwa sababu kuna mzunguko wa uhalifu .
Wazungu wanaiba dhahabu na kugawa bunduki kwa waasi . Waasi wanashambulia wananchi . Wananchi wanataka kuchimba dhahabu na kwenda kuuza nchi jirani ya Randa na Uganda kama ilivyokua Tanzania wakati wa Tanzanite waliuza Kenya na India kwa sababu ya soko zuri.
Sasa Wahuni wanaoiba rasilimali za Kongo adui zao wakubwa tangu enzi za Mfalme Leopard ni Wananchi wa Kongo na sio Kagame wala Randa wala Watusi wala wahutu ,wanatoa pesa UN na kwenye hizo nchi za Afrika vibaraka wa wazungu majuzi kupeleka majeshi kuwalinda dhidi ya wananchi wa Kongo wanaotaka kwenda kuchimba madini .
Iko hivi vita hii itaisha siku Kongo itakapopata Rais mzalendo na kuwafukuza wanajeshi wote toka UN na Wale wanaotoka nchi nyingine kama Tanzania na Afrika kusini . Hao wanaenda Kongo kama mradi wa mabeberu kuiibia Kongo .
Wakati fulani waasi waliwashambulia UN wazungu wakatishia kuacha kutoa silaha kwa waasi ili wakamatwe . Waasi wakapiga magoti kwa mabeberu . Ndio ikagunduliwa kuwa waasi na mabeberu la ni moja ila adui yao ni wananchi wanaotaka kuchimba madini yao na kuuza wanakotaka. Sasa Kagame amekua mzalendo ili waafrika wafaidi rasilimali zao wenyewe na sio kuwapa wazungu kwa malipo ya risasi na bunduki za kuuana.
Serikali ya Kongo inaungana na Majizi kuwauaa raia wake wanaodai haki zao kwa kuwaita waasi kwa sababu tu inataka kuwahamisha ili iwape wazungu ardhi ya madini wakaneemeshe nchi za ulaya .
Ili vita iishe waafrika wakatae kupeleka majeshi Kongo na UN waondoke Kongo ili wezi wa madini walipe Kodi na wananchi wapate maendeleo Kongo ikae meza moja na Rwanda kulinda nchi zao wananchi wake na kuruhusu biashara ya dhahabu kuuzwa kwenye soko zuri Rwanda na kwingineko sio kuwaachia wazungu uporaji kwa damu za watoto wa maskini huku wakiwabagua wakongo wenye asili ya kinyarwanda.
Hata hapa Tanzania wapo wa mtanzania wenye asili ya kinyarwanda na Kikongo pia ambao kuna wakati walifanya uhalifu mkubwa sana kule Kagera na mpaka sasa wapo kule Kigoma kwenye ziwa Tanganyika . Chaa ajabu uhalifu Kagera umeisha ila kule Kagera ambapo UN wapo uhalifu ni mkubwa sana . Mkitaka uhalifu uiishe dawa ni kufunga shughuli za UN . Hapo ndipo kuchaka cha uhalifu kinapojificha na wanapopata silaha kirahisi kwa kujifanya ni wakimbizi .
Waafrika amkeni kupinga unyonyaji unaofadhiliwa na mawakala wa ubeberu waliojificha kwenye madaraka bila kujali maisha ya wanyonge