Huruma, upendo na msaada wa Mungu ndiyo msingi wa mafanikio yako kisiasa, kijamii na kiuchumi

Huruma, upendo na msaada wa Mungu ndiyo msingi wa mafanikio yako kisiasa, kijamii na kiuchumi

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Historia ya maisha yako ya zamani tangu kuzaliwa, malezi na makuzi yako kiroho, kimwili, kielimu, kisiasa kijamii na hata kiuchumi ni Huruma ya Mungu tu.

Na hata hapo ulipofikia hivi sasa ni Upendo wa Mungu tu

Na unapoelekea ni pekee Msaada wa Mungu ndiyo wa kukufanikisha. Jifunze kua na shukrani.

Kifupi tulikotoka kama wanadamu ni huruma ya Mungu tu, na tulipo ni upendo wa Mungu, na huko tuendako ni kwa msaada wa Mungu tutafika salama.

Neema na Baraka za Mungu ziambatane na kuandamana nawe katika kazi zako za kisiasa, kijamii na kiuchumi daima.

Mshukuru Mungu kwa kila Jambo

Mungu Ibariki Tanzania 🐒
 
Historia ya maisha yako ya zamani tangu kuzaliwa, malezi na makuzi yako kiroho, kimwili, kielimu, kisiasa kijamii na hata kiuchumi ni Huruma ya Mungu tu...
Si kweli wanasiasa na wafanyabiashara waliofanikiwa asilimia 95 ni walogaji, walonzi na wanafanya vitu vya ajabu hudhanii.

Watu wa kati na wa chini ni watu waungwana sana wengi wao wanamtegemea Mungu kweli.
 
Dreams , Knowledge, Hard Work , Perseverance.

Mungu ni Mungu , naye alisema, Mvivu na Mzembe ni rafiki wa umasikini ( kutokufanikiwa).

Mawazo yako mtoa mada, ndio yanakufanga kujipendekeza Kwa CCM kiasi mpaka Unamchukiza Mungu ukitegemea kupata kanafasi.

Kwa Sasa CCM ni Chaka la wajinga, wavivu ,wanaotumia janjajanja kuishi.

Binafsi nmethibitisha hapa Tanzania, na Duniani Kwa ujumla, mwanadamu yoyote mwenye Akili nzuri kabisa hawezi kufurahia ujinga na upuuzi na uozo na ufisadi, na upuuzi wa aina yoyote unaofanywa na VIONGOZI.
 
Si kweli wanasiasa na wafanyabiashara waliofanikiwa asilimia 95 ni walogaji, walonzi na wanafanya vitu vya ajabu hudhanii..
Watu wa kati na wa chini ni watu waungwana sana wengi wao wanamtegemea Mungu kweli.
kuamini au kutokuamini ni uamuzi na hiyari yako. Mimi nimetekeleza wajibu wangu, sidaiwi chochote siku ya mwisho 🐒
 
Dreams , Knowledge, Hard Work , Perseverance.

Mungu ni Mungu , naye alisema, Mvivu na Mzembe ni rafiki wa umasikini ( kutokufanikiwa)...
sidaiwi chochote, na yeyote katika hili,

kwa hiyari yangu nimetekeleza wajibu wangu katika kushuhudia Neema na Baraka za Mungu katika maisha ya kila moja wetu bila kujali, dini wala chama cha siasa..

Ni hiyari yako kuamini Mungu, au au kuendekeza ushirikina 🐒
 
Back
Top Bottom