Hushpuppi adaiwa kutakatisha zaidi ya USD 400,000 akiwa bado Gerezani

Hushpuppi adaiwa kutakatisha zaidi ya USD 400,000 akiwa bado Gerezani

Billy the Goat

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2013
Posts
566
Reaction score
353
Aliyekuwa Gwiji wa utakatishaji fedha aliyejipatia umaarufu mitandaoni hasa Instagram, anayejulikana Kwa jina la Hushpuppi amefunguliwa mashtaka mapya na waendesha mashitaka wa Marekani wakimtuhumu kufanya ulaghai na kutakatisha zaidi ya dola za marekani 400,000 (zaidi ya Tsh Milioni 900) akiwa gerezani.

Siku ya Jumatano, waendesha mashtaka wa Marekani waliwasilisha hati mbele ya Mahakama huko California ya Marekani wakiwa na ushahidi mpya unaoonyesha kuwa Hushpuppi alifanya ulaghai na utakatishaji fedha haramu katika gereza analoshikiliwa huko Marekani, wakati akisubiri hukumu ya kesi yake ya kutakatisha fedha inayokadiriwa kufika Dola millioni 24 (Sawa na Shilingi Bilioni 55)

Hati hizo zilisema Hushpuppi alihusika katika ununuzi na ufujaji wa kadi za benki za Malipo wanayopewa raia wa Marekani kutoka Serikali Yao ili kuwapunguzia makali ya Athari za Kiuchumi zilizosababishwa na janga la COVID19.

Kulingana na waendesha mashtaka, wafungwa wanaruhusiwa kutumia simu pamoja na mtandao wa internet bila kufuatiliwa ili kulinda haki zao za faragha.

Hata hivyo, kati ya Januari 28 na Machi 4 2022, maafisa wa gereza analoshikiliwa Hushpuppi walibaini kuwa alikuwa amevuka mipaka ya matumizi ya intaneti, ambapo waliripoti kwa FBI, ambao walitoa kibali cha kurekodi shughuli matumizi yake ya simu pamoja na internet kwa wiki moja.

Ilibainika kuwa Hushpuppi alikuwa amenunua kadi 58 za benki za malipo ya athari za kiuchumi kutoka kwa soko la wahalifu wa mtandaoni zenye thamani ya $429,800.

Pia, Soma;

1). Hushpuppi afikishwa Marekani, asomewa mashtaka ya utakatishaji pesa. Atuhumiwa kutapeli club moja ya EPL £100M

2). Hushpuppi kabambikiwa kesi kwa sababu ya ushamba pamoja na Mwafrika kuchukiwa akiwa na maisha ya juu

20220317_155838.jpg
20220317_155842.jpg
20220317_155845.jpg


=====

UPDATES;

=====

Habari hii imekanushwa.

Zaidi soma;

1). Fake News: US says Hushpuppi didn't commit fraud in prison
 
Back
Top Bottom