BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Hatimaye hukumu ya mwizi nguli mitandaoni ambaye ni raia wa Nigeria, Ramon Abbas (39), maarufu Hushpuppi imesomwa jana Alhamisi, Novemba 3, 2022 na Jaji Otis Wright wa Mahakama ya Wilaya huko California ambapo Hushpuppi amehukumiwa kifungo cha miaka 11 gerezani.
Hata hivyo kwa kuwa tayari Hushpuppiameshakaa jela nchini Marekani kwa takribani miaka 2 tangu mwezi Juni mwaka 2020 baada ya kukamatwa huko Dubai na kisha kuhamishiwa Marekani, anatajwa kutumikia kifungo chake kwa miaka 9.
Sanjali na hilo, kurasa zake za mitandao ya Kijamii ikiwemo wa Instagram uliokuwa na followers zaidi ya Milioni 2.8 imefungwa.
SNS