POTOSHI Hushpuppi aliachiwa kwa muda kutoka gerezani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya Davido

POTOSHI Hushpuppi aliachiwa kwa muda kutoka gerezani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya Davido

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na hiki kipande cha video kikimuonesha Hushpuppi akiwa amehudhuruia kwenye sherehe y Davido na anagawa pesa.

Taarifa hiyo inaeleza pia kuwa Hushpuppi alipewa ruhusa ya kuwa nje ya gereza kwa muda ili aweze kuhudhuria sherehe hiyo.
1755066929051.png

 
Tunachokijua
Agosti 11, 2025 Davio pamoja na mkewe Chiomma walifanya white wedding (ndoa ya kidini) huko nchini Marekani na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Madai

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa nyakati tofauti walichapisha kipande cha video video kikimuonesha aliyekuwa mwanamitandao maarufu na mragabishaji, Ramon Olorunwa Abbas maarufu kama Hushpuppi, Hush, Ray Hushpuppi, The Billionaire Gucci Master akiwa amehudhuria kwenye sherhe (White Wedding) ya Davido na mkewe Chioma. Tazama hapa na hapa

Kipande hicho cha video kinamuonesha Hushpuppi akitunza fedha huku ikielezwa kuwa amepewa mapumziko mafupi na gereza kwa ajili ya kuhudhuria ndoa ya hiyo.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kina na kubaini kuwa Si kweli kuwa Hushpuppi alihudhuria sherehe hiyo.

Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao na nyenzo za kidigitali ikiwemo google reverse image search, JamiiCheck imebaini kuwa video hiyo si hivi karibuni (Agosti, 2025) na badala yake imekuwepo mtandaoni kwa muda mrefu kabla ya sherehe hiyo.

Mathalani vyanzo mbalimbali vilichapishataarifa hiyo mwaka 2020 wakati Hushpuppi akiwa kwenye harusi ya Adewele Adeleke na Kani iliyofanyika Dubai. Adewele ni kaka yake Davido na sherehe hiyo ya Adewele ilifanyika Februari 2, 2020 Dubai baada ya ndoa ya kimila iliyofanyika huko Cross river Disemba 13, 2019.

Hivyo JamiiCheck imejiridhisha kuwa video hiyo imesambazwa tena hivi karibuni kwa lengo la kupotosha kwani Hushpuppi bado anatumikia kifungo chake miaka 11 gerezani baada ya kuhukumiwa jela Novemba, 2022 nchini Marekani kwa makosa ya ulaghai wa fedha.
Back
Top Bottom