Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo: Waagizaji hawakupaswa kuleta mchele wa Msaada kutoka Marekani kwani Tanzania ina hazina ya mchele

Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo: Waagizaji hawakupaswa kuleta mchele wa Msaada kutoka Marekani kwani Tanzania ina hazina ya mchele

Tanzania inakuwaje maskini jeuri ? Umeshaambiwa kuwa ni mchele wa msaada ...sasa unachagua jinsi gani yule anayekusaidia (kukupa bure) akusaidie ????

Huna kitu anatokea mpita njia anakupa buku ,unaikataa ukitaka akupe elfu kumi kwa kuwa buku tayari unayo mfukoni.
 
Bashe ameendeshwa na hisia na maoni ya wazalendo uchwara katika hili
Kwa uwezo wako wa kufikiria, unadhani tz tunahitaji msaada wa mchele, maharage n mafuta?? Vipi wasomali, palestines, Nigerians, Ukrainians...
Kwa fikra zako kwa stories za kuambiwa, kujisomea n uwezo wako wa kufikiria, unadhani America wana mapenzi hayo kweli ya dhati kwa watz?? Tukirudi kwenye historia, America amewahi kulisaidia taifa gani bila kuwa na agenda yeyote iliyojificha??
Hivi hujui uko Palestine kila kukicha sio chini ya watu 40 wanakufa kwa njaa? Kwanini asipeleke chakula chake kwenye taifa lenye uhitaji anatuletea uku ambapo tunategemewa na mataifa jirani tuwauzie mazao yetu ya ziada? Hatuna maendeleo kama yao, ila wasituone sisi maboya kiasi hiki.
 
 
Kwa uwezo wako wa kufikiria, unadhani tz tunahitaji msaada wa mchele, maharage n mafuta?? Vipi wasomali, palestines, Nigerians, Ukrainians...
Kwa fikra zako kwa stories za kuambiwa, kujisomea n uwezo wako wa kufikiria, unadhani America wana mapenzi hayo kweli ya dhati kwa watz?? Tukirudi kwenye historia, America amewahi kulisaidia taifa gani bila kuwa na agenda yeyote iliyojificha??
Hivi hujui uko Palestine kila kukicha sio chini ya watu 40 wanakufa kwa njaa? Kwanini asipeleke chakula chake kwenye taifa lenye uhitaji anatuletea uku ambapo tunategemewa na mataifa jirani tuwauzie mazao yetu ya ziada? Hatuna maendeleo kama yao, ila wasituone sisi maboya kiasi hiki.
Mkuu umeshatembea huko vijijini ukawaona watoto wanavyoteseka na njaa na walivyodumaa. Lishe duni ni tatizo kubwa Tanzania. Kama wewe na watoto wako mnajitosheleza hapo ulipo shukuru Mungu, kuna watu huko hawajui mchana watakula nini. Cha msingi hapo Serikali ijiridhishe usalama wa hicho chakula kama Kipo Sawa mm sioni shida. Mchele na chakula kilichopo tz ni Kwa wanaojiweza Tu.
 
Mkuu umeshatembea huko vijijini ukawaona watoto wanavyoteseka na njaa na walivyodumaa. Lishe duni ni tatizo kubwa Tanzania. Kama wewe na watoto wako mnajitosheleza hapo ulipo shukuru Mungu, kuna watu huko hawajui mchana watakula nini. Cha msingi hapo Serikali ijiridhishe usalama wa hicho chakula kama Kipo Sawa mm sioni shida. Mchele na chakula kilichopo tz ni Kwa wanaojiweza Tu.
Sehemu chakula kinapotoka lishe ni duni. Shida ni elimu sio uhaba
 
kitu muzuri sana H.e Bashe. Babu yangu anaeleza alikula ugali ya njano ilikuwa hakuna Vitamini.
 
Swali jee utafiti umefanywa kuhakikisha hivyo virutubisho ni vizuri kwa watoto wetu, visine kuwa na Virutubisho vya kujenga marekebisho ya JINSIA ya Vijana kuwa vinginevyo. Maana siku hizi kuna hila za kupunguza idadi ya watu, haswa barani Africa
 

MKOA wa Ruvuma unaoongoza kwa udumavu​

Tarehe Ya Kuwekwa: May 16th, 2019

1710641677373.png


MKOA wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa mitano nchini inayoongoza kwa udumavu. Mkuu wa Wiaya ya Songea ndugu Pololet Mgema ameongoza kikao cha Kamati ya Lishe katika Manispaa ya Songea ambacho kimezungumzia changamoto mbalimbali za lishe ikiwemo udumavu kwa watoto. Fuatilia makala haya ili kujua changamoto ya udumavu kitaifa na kimataifa.

TANZANIA ni miongoni mwa nchi 10 zinazokabiliwa na changamoto ya kuwa na watoto wenye udumavu, ugojwa ambao unachangiwa kwa kiwango kikubwa na lishe duni wanazozipata watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi yamekuwa yakihangaika kuhakikisha kuwa changamoto hii inapungua kama si kutoweka kabisa hapa nchini.

Kwa nyakati tofauti, jitihada zimekuwa zikichukuliwa katika kuhakikisha kuwa afya inaimarishwa kwa kila mtu, ambapo zimekuwa zikiungwa mkono na taasisi mbalimbali za dini.

Lakini bado hali ni tete kwa watoto ambao ndio wanaokumbana na tatizo hili la udumavu na ukondefu unaosababishwa na kukosa lishe bora.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha kuwa kila siku zaidi ya watoto 270 walio chini ya umri wa miaka mitano nchini Tanzania hupoteza maisha kwa lishe duni, huku zaidi ya watoto 2,700,000 wakikabiliwa na udumavu unaotokana na utapiamlo.

Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 40 ya vifo hivyo hutokea katika mwezi wa kwanza wa maisha ya watoto hao.

Huku takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa kwa shabaha ya kuwasaidia watoto duniani UNICEF, zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 42 ya watoto wote wa Tanzania waliochini ya umri wa miaka mitano wamedumaa kutokana na kukosa lishe bora.

Chanzo cha ugonjwa huu wa udumavu kinaelezwa kuwa ni utapiamlo unaosabibishwa na lishe duni kwa mtoto ambapo huchangia mtoto kuwa na kimo au urefu mfupi usioendana na umri wake.

Japo kumekuwapo na dalili za kupungua kwa kiwango cha udumavu nchini kwa asilimia 30, kati ya mwaka 1994 hadi 2014 japo idadi ya watoto waliodumaa ikiwa imeongezeka kutoka milioni 2.4 hadi 2.7 katika kipindi hicho.

Sababu nyingine ya udumavu ni kutokana na kuugua mara kwa mara katika miaka mitatu ya mwanzo ya makuzi yake.



Sababu nyingine ni afya na lishe duni kwa wanawake kabla ya ujauzito, wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua.

Pia kutopangilia uzazi yaani kuzaa karibu karibu na tatizo la wasichana kubeba mimba wakiwa katika umri mdogo.

Taratibu duni za ulishaji watoto, ikiwamo kutonyonyeshwa maziwa ya mama pekee katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa na kupewa chakula cha nyongeza kisichokidhi mahitaji yao ya lishe pale wanapotimiza umri wa miezi sita.

Watoto kupewa kiasi kidogo cha chakula au kisichokuwa na ubora au mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya chakula pia ni sababu nyingine zinazodumaza watoto.



Athari


Mtoto kuwa na udumavu huchangia kupata athari zisizoweza kurekebishika katika maisha yake hata kama kwa hapo baadaye atapewa lishe bora, mwili wake tayari utakuwa umedumaa na hivyo kushindwa kupokea marekebisho.

Kushuka kwa maendeleo ya akili ya mtoto pia ni moja ya athari za udumavu, hatua hii humfanya mtoto kushindwa kufanya vizuri hata kwenye masomo yake.

Kuwa na uzito mkubwa, kiriba tumbo na kukumbwa na magonjwa yasiyoambukiza kama moyo, kiharusi, shinikizo la damu na hata kisukari.



Namna ya kukabiliana na ugonjwa huu

Ni wazi kuwa mpango wa WHO kwa Tanzania ni ifikapo mwaka 2025 walau idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano waliodumaa iwe imepungua kwa walau asilimia 40.

Hata hivyo, malengo haya yatafanikiwa tu iwapo Watanzania watazingatia lishe bora kwa watoto na mjamzito kulinda afya yake katika kipindi chote cha ujauzito na kuzingatia unyonyeshaji pindi anapojifungua.

Ni muhimu kwa akina mama kunyonyesha watoto wao maziwa hadi watakapofikia miaka miwili, hapa wanawake wajitahidi kutowaachisha watoto wao nyonyo mapema.

Inashauri kwa mama kumnyonyesha mtoto wake ziwa lake kwa kipindi cha miaka miwili
 
Dar es Salaam. Saa chache baada ya kuibuka kwa mjadala katika mitandao ya kijamii juu ya mchele ulioongezwa virutubisho ulioletwa Tanzania kutoka nchini Marekani, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amefunguka akisema waagizaji hawakupaswa kuleta mchele huo kutoka nje, kwa kuwa Tanzania ina hazina ya mchele.

Akaongeza kuwa kama ni virutubisho, bado shirika lililoagiza mchele huo lingenunua mchele wa ndani na kuwaomba wafadhili wao wauongezee virutubisho hapahapa nchini, huku kila mtu akiona kuliko kuagiza kutoka nje ya nchi.

Mjadala wa mchele huo ulianzia katika mtandao wa X, baada ya ukurasa wa Ubalozi wa Marekani kuweka picha iliyokuwa ikionyesha viroba vya mchele huo, huku ikiambatisha na ujumbe uliosomeka:

"Chini ya mpango wa 'Pamoja Tuwalishe', Wizara ya Kilimo ya Marekani, kwa ushirikiano na Jumuiya za Kimataifa, imetoa msaada wa kwanza wa mchele ulioongezwa virutubisho, maharage na mafuta ya alizeti kutoka kwa wakulima wa Marekani moja kwa moja hadi shuleni katika eneo la Dodoma nchini Tanzania."


Ujumbe huo uliendelea kueleza kuwa msaada huo unalenga zaidi kutoa milo yenye lishe kwa wanafunzi wa shule zaidi ya 300 zinazoshiriki, huku ukieleza kuwa mbali na mchele huo, pia wataanzisha bustani za shule na kufunza mbinu za kuvuna.

Alichosema Bashe

Akizungumzia suala hilo wakati akielezea miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan na yale aliyoyafanya katika sekta ya kilimo, Bashe amesema Tanzania inazalisha mchele na maharagwe kwa kiwango cha kutosha.

"Tumewaambia ile NGO, waambieni Wamarekani kuwa mchele upo maharagwe yapo nchi hii, zile fedha wanazotumia kuwapa wakulima wa Marekani wawape Watanzania. Tununue mchele kutoka Tanzania, maharage kutoka hapa Tanzania, halafu hivyo virutubisho mnavyotaka kuweka muwekewe hapahapa Tanzania wote tunaona," amesema Bashe na kuongeza kuwa ameieleza NGO hiyo kuwa Tanzania inajitosheleza kwa chakula.

Maoni mtandaoni

Elisha Mbise alitoa maoni yake katika ujumbe ulio katika ukurasa wa Ubalozi wa Marekani akiandika: "Tanzania tuna chakula cha kutosha...mchele umejaa kila mahali. Walete vitu vya maana, wajenge maabara, walete vifaa vya hospitali, vifaa vya kufundishia, vyuo vya ufundi. Hivi ndivyo vitu vinavyoweza kugusa elimu na afya kama kweli wana nia na kusaidia hayo maeneo.’’

Naye Dani Zayumba aliandika: "Tanzania hatuhitaji chakula cha misaada bali tunahitaji mabadiliko ya mitalaa ya elimu, ili tuweze kujilisha wenyewe. Mnaweza kufananisha mchele wa Mbeya na Marekani kweli?’’

Credit: Mwananchi digital

View attachment 2936741

Hapo awali Balozi wa Marekani ukiandika kwenye Mtandao wa X Kwamba, "Chini ya mpango wa 'Pamoja Tuwalishe', Wizara ya Kilimo ya Marekani, kwa ushirikiano na Jumuiya za Kimataifa, imetoa msaada wa kwanza wa mchele ulioongezwa virutubisho, maharage na mafuta ya alizeti kutoka kwa wakulima wa Marekani moja kwa moja hadi shuleni katika eneo la Dodoma nchini Tanzania. Zaidi ya kutoa milo yenye lishe, wanafunzi katika shule zaidi ya 300 zinazoshiriki, pia wataanzisha bustani za shule, na kujifunza mbinu za kuvuna maji ya mvua. Ikiwa ni mfano kamili unaoweza kuigwa, programu hii inaakisi ahadi na dhamira ya dhati ya Marekani ya kukuza afya, elimu, na fursa kwa watoto kote ulimwenguni."
View attachment 2936743View attachment 2936744
Nyie mnataka mchele wa msaada kwani kuna ukame nchini? Hebu tuondoleeni hii aibu. Kwani mchele na mboga zimeletwa kabla ya makubaliano? Mbona mmewapa exemption ya Kodi meaning mlijua ni bidhaa ya msaada.
 
Kiburi chanini wakati watoto wetu wanaanguka njaa mashuleni huku walimu wakipepesuka kwa njaa??

Wizara ipime kama Mchele hauna shida upelekwe mashuleni, Mchele wenyewe bei ghali shule gani inaweza kununua ikalisha watoto wake???

Waziri anakaa Dar anaamini watuwote tunakula Kila tunapojiskia...huku vijijini kunawatoto hupigwa kipigo kikali kisa kudokoa wali kutokana na njaa kali waliyonayo. Tunakula mlo mmoja tuu labda siku ya bahati ndiyo tule milo miwili.

Msiweke kiburi kisa ninyi mnakula mnashiba na kuvimbiwa, chamuhimu Mchele unaenda liwa shule ambamo hawawezi nunua Mchele wetu ambao bei ni yajuu.

Nilini tutapata viongozi wazalendo wenye akili nzuri na wanaojua nchi yao na watu wake wanavyoumia hasa huku vijijini??
Hopeless leaders kabisa!!
 
Magufuli angewatimua watu fulani saa saba usiku kwa sababu ya mambo ya kipuuzi kama haya.
 
Back
Top Bottom