Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi, ilikuwaje ukawa Mbunge wa Mkuranga, mkoa wa Pwani, na sasa unaenda kugombea urais Zanzibar?

Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi, ilikuwaje ukawa Mbunge wa Mkuranga, mkoa wa Pwani, na sasa unaenda kugombea urais Zanzibar?

Ni Mtanzania.

Hilo siyo jibu sahihi......!!!
Issue hapa siyo Utanzania baali Uzanzibari na Uzanzibara.
Uzanzibari- Uunguja na Upemba.
Uzanzibara- Utanganyika.
Sijawahi sikia Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar akawa Mtanganyika..........ila Rais na au M/Rais wa Tanganyika aweza kuwa Mpemba au Muunguja but not the opposite!
 
Ngoja nikuambie kitu mkuu.

Hivi unajua kuna wazanzibari waliozaliwa bara? Na unakubaliana na mimi kwamba kuna wasukuma waliozaliwa zanzibar? Na unajua kwamba kuna wamakonde waliozaliwa Musoma? Hao je tunawaitaje? Kuzaliwa kwao Musoma au Kagera kunawatoa umakonde wao?

Kama jibu ni sio hiyo ndiyo case ya Hussein Mwinyi pia. Hivi unajua kwamba hata baba yake aliwahi kuwa mbunge wa Mkuranga ? Mkuranga inaweza kuwa sehemu yake tu aliyoianzia siasa lakini kama asili yake ni Zanzibar basi alirudi nyumbani
Yaani hao wanao jiita wanzibar ni wamakonde na wasukuma mixer nyamwezii wale walivushwa na mabwenyenye ya kiarabu Kwa ufanyanywa utumwa[emoji16][emoji16] , sasa Ajabu Nikwamba wanakataa asili Yao haoo. Ukikutana na watu wa kulee waambie we kabila gani ? Uwasikie vizurii [emoji23] yaani hawana kitu wanajua aisee, wanajaribu kutafuta identity ambayo waowenyewe hawaijui ....!
 
Hili suala linachanganya, na ninahofia wahafidhina wa Kizanzibari watalitumia kutusumbua kwenye kampeni.

Je, Hussein Mwinyi ni Mtanganyika au ni Mzanzibari? Ilikuwaje akagombea Mkuranga, mkoa wa Pwani?

Hii siielewi, anayeelewa anifahamishe
Sisi ni watanzania hatuchagua kiongozi kwa kuangalia alikozaliwa. Tuna wabunge wengi wanaongoza majimbo ambayo sio kwao kwa kuzaliwa na wanaongoza vizuri sana. Kuna Wazanzibari wengi wanaishi bara na hakuna anayewauliza wanashikiri shughuli zote za kisiasa na kiuchumi wakiwa huru. Lakini kwa baadhi ya wenzetu WANASIASA UCHWARA KILA KUKICHA WANATAFUTA SABABU YA KUTUGOMBANISHA KWA KUTENGENEZA TOFAUTI FEKI ILI TUCHUKIANE NA TUGOMBANE.
NAJUA NDUGU ZETU WANZANIBARI HAWATALIKUBALI HOJA DHAIFU KAMA HIZO. WANASIASA WENGINE WANATAKA KUWAAMINISHA WATU KUWA UZAO WA SULTAN SEIYED SAID NDIO WENYE HATI MILIKI YA ZANZIBARI WAKATI NI WAVAMIZI KTK KARNE YA 13
 
chinembe,
Kwani sheria inasemaje kuhusu kugombea ubunge? Wa bara agombee bara na wa visiwani agombee visiwani?
Ili kuondoa Tanganyika kuimeza Zanzibari, wao wana ruksa kugombea Tanzania bali Watanganyika hugombea Tanzania Bara tu. Kadhalika ile sheria ya kumtaka mgombea huko Visiwani kuwa na kitambulisho cha mkazi kwa muda ambao wameuweka inawatoa Wabara katika kugombea huko.
 
Una habari kwamba kwa Mwinyi ni Zanzibar na wana ardhi kubwa sana Zanzibar? Kama sio wazanzibari imekuwa je wakamiliki hayo maeneo?

Hivi huwezi kuishi Zanzibar ukafanyia kazi Dar. Mbona wabunge wengi wanaishi Dar na sio majimboni kwao?

Maana ya kuishi Zanzibar unaielewa vipi?

Huwa sishobokei maswali ya kiwango cha chini hivi, na sijui kama mada hii ni size yako!! Hayo maswali kawaulize wa level yako.

Nikukumbushe, swala la uraia ni nyeti sana kwa wazanzibari kulipo watanganyika. Kuwa mtanganyika aikifanyi uwe mzanzibari!! Wakati wewe unajua kuna mtanzania - wazanzibar wanajitambua kama wazanzibar na NEC haimtambui hata mzanzibar (achilia mbali mbara) ambaye hajakaa katika shehia husika miaka 5 kabla ya kupiga/kupigiwa kura)!! Hussein Mwingi alijithibitisha kuwa mbara pale alipogombea na kushinda ubunge wa mkuranga!! Hii haikumwondolea uzanzibari bala haki ya kuwa kiongozi wa kuchaguliwa zanzibar.

Hivi bado uko katika mawazo kuwa umiliki wa kitu unaambatana na haki na uhalali?? Kwani mwizi hawezi kumiliki kitu alichoipa au kudhulumu??
 
Mleta mada somo la Uraia darasa la tatu alizungusha.

Yaani hata Civics ya form one nayo pia akalamba ziro.
 
Ni utaratibu wa kawaida tu ulioandaliwa na CCM na Tanganyika. Kwani haujasikia kuwa Jumbe alikuwa Rais wa Zanzibar baada ya muda wake akarudi Bara? Na Marehemu Hassan Moyo (Tanga), nk nk? Na hata Shein Disemba 2020 atarudi Bara kuishi maisha yake ya kawaida. Mwinyi atarudi tu Bara siku moja. Usiwe na wasiwasi.
Hili suala linachanganya, na ninahofia wahafidhina wa Kizanzibari watalitumia kutusumbua kwenye kampeni.

Je, Hussein Mwinyi ni Mtanganyika au ni Mzanzibari? Ilikuwaje akagombea Mkuranga, mkoa wa Pwani?

Hii siielewi, anayeelewa anifahamishe
 
Hili suala linachanganya, na ninahofia wahafidhina wa Kizanzibari watalitumia kutusumbua kwenye kampeni.

Je, Hussein Mwinyi ni Mtanganyika au ni Mzanzibari? Ilikuwaje akagombea Mkuranga, mkoa wa Pwani?

Hii siielewi, anayeelewa anifahamishe
Shida iko wapi? Mzanzibari yeyote ana haki ya kugombea nafasi yoyote Tanganyika. Na ndicho alichofanya Hussein Mwinyi.
 
Hili suala linachanganya, na ninahofia wahafidhina wa Kizanzibari watalitumia kutusumbua kwenye kampeni.

Je, Hussein Mwinyi ni Mtanganyika au ni Mzanzibari? Ilikuwaje akagombea Mkuranga, mkoa wa Pwani?

Hii siielewi, anayeelewa anifahamishe
Mgombea wa kukodi huyo, Wazanzibar hawana sifa ya kusimamisha mgombea u Rais kupitia CCM huko. Inasikitisha sana.

ITOSHE TU KUSEMA, MITANO YA UTAWALA WA IMLA/MKONO WA CHUMA SASA BASI..
 
Watasema ni Mtanzania na alikuwa mkazi wa Mkuranga. Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Temeke...
 
Zanzibar wasipotumia fursa ya Lissu na Seif katika uchaguzi huu CCM wakimtaka wanaweza kumpachika Uzanzibari hata Serukamba na kuwa Rais wa Zanzibar na Waunguja wasifanye kitu.
Tangu mwaka 1995 zanzibar haijawahi kukosea kupiga kura sema tuu ni vile wananyimwa haki yao kinguvu
 
Amekuwa mkaazi wa mkuranga hivyo alikuwa na sifa za kugombea huko. Sifa kuu ya kugombea zanzibar ni uwe mzaliwa kwa asili au uwe umekaa (kuishi zanzibar miaka 5 mfululizo).
Okay, kuwa na sifa Zanzibar unatakiwa uishi miaka mitano, na Mkuranga unatakiwa miaka mingapi???
 
Katiba ya Jamuhuri inamruhusu Mtanzania yeyote mwenye umri zaidi ya 21 anayejua kusoma na kuandika kugombea ubunge mahala popote katika Jamuhuri..na ndio maana unakuta wachaga wakiwa wabunge wa waarusha Kwa zaidi ya miaka 15 SASA. (katiba inaruhusu)
Eeeh!?!
 
Zanzibar wasipotumia fursa ya Lissu na Seif katika uchaguzi huu CCM wakimtaka wanaweza kumpachika Uzanzibari hata Serukamba na kuwa Rais wa Zanzibar na Waunguja wasifanye kitu.
CCM imejaza mabashite, hawezi kujitokeza mtu wa kujibu hili. CCM hawajitambui
 
Yaani hao wanao jiita wanzibar ni wamakonde na wasukuma mixer nyamwezii wale walivushwa na mabwenyenye ya kiarabu Kwa ufanyanywa utumwa[emoji16][emoji16] , sasa Ajabu Nikwamba wanakataa asili Yao haoo. Ukikutana na watu wa kulee waambie we kabila gani ? Uwasikie vizurii [emoji23] yaani hawana kitu wanajua aisee, wanajaribu kutafuta identity ambayo waowenyewe hawaijui ....!
ahahahahahaaaa . . .raha sana
 
Back
Top Bottom