Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi kukosa Kura zote za Zanzibar za Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) inafikirisha sana. Haki ya Wazanzibar kuchagua iko Wapi?

Unataka kutuambia karatasi ziliandikwa majina ya wapiga Kura?
 
Si uanzishe uzi wako mbona unatuconfuse??
 
Hivi wazenj mtakubali lini kuwa Zenj sio nchi ? Ni kanda maalum tu ya tz
 
Miongoni mwa sababu kubwa inayowafanya Wazanzibar wauchukie Muungano ni huu ubabe na njia zinazotumiwa kuulinda.Tunavyofahamu kuungana ni lazima kuwe na vinavyounganishwa aidha zaidi ya kimoja kuungana na kingine.Hapa ziliungana Nchi mbili huru yaani Tanganyika na Zanzibar kwa makubaliano maalum(Makubaliano na Hati ya Muungano),iweje tunashindwa kujadiliana namna bora za kuuendesha?
Kwa nini CCM wanakataa mjadala kuhusu Muungano?Je,Hiyo ni aina gani ya utawala?Wazanzibar wakiulizwa kwa njia ya kidemokrasia wataamua kuchagua Muungano kwa namna mnavyowafanyia?Tusijigeuze wakoloni weusi kwa ndugu zetu,tutengeneze Muungano unaoendana na mahitaji yetu ya sasa huku tukihifadhi kwa wivu mazuri ya historia yake.
Tuandike Katiba ya Tanzania Mpya kwa ajili ya Watnzania wote bila kujimilikisha michakato kama tulivyofanya 2014 enzi za Bunge la Katiba.Fursa hiyo ikatekwa na wanasiasa kwa ubinafsi wao.Hatuna jinsi nyingine zaidi ya kurejelea ule mchakato,kwa sababu kazi ile kubwa iliyofanywa na Watanzania haiwezekani ipotee bila kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa hoja nyepesi za Watawala wa CCM ya kuwa Katiba siyo kipaumbele chao.
Katiba ni kipaumbele cha Watanzania,kama CCM inashindwa kulifanyia kazi suala hili nyeti kwa ufanisi,wasiwazuie Watanzania kutimiza hitaji la Katiba Mpya ya Watanzania,watupishe lifanywe na wengine.
Watanzania wenzangu,tunatakiwa kufanya maamuzi magumu ili tuijenge nchi yetu tuliyopewa na muumbaji wa dunia.Hapa tutaishi mara moja tu na tunatakiwa tuijenge kwa pamoja,baadaye tuwarithishe vizazi vijavyo nchi bora tuitakayo.
 
Kumbuka aliyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuhusu Serikali tatu alizotaka Maalifu Seif akiwa Waziri Kiongozi Zanzibar.
"Sera ya Serikali tatu si sera ya CCM, naomba kadi yangu ya CCM"
Maalifu Seif alimrudishia Mwalimu Kadi ya CCM, na baada ya hapo aliamuru atoke nje.
Kwa sababu hakuwa mwanachama wa CCM tena, alivuliwa nyadhifa zote na airudi Dar kwa Basi.
Ni kweli kuwa mafisadi wa huko walitumia pesa nyingi kutaka kuweka mtu wao kwenye Urais kwa kuwalipia watu fomu za kuomba nafasi ya Urais na kwa namna yoyote wajumbe wa Zanzibar watakuwa walininuliwa na kundi hili.
Tunapoongea swala la Zanzibar kiutawala na hasa kuhusu Srikali na Chama yukumbuke kuwa CHAMA ni cha Muungano na hakuna chama cha Zanzibar peke yake. Lakini kuna Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano ya Tanzania.
Maamuzi ya kamati kuu ya CCM hayana ubara na Unzanzibari.
Mjumbe wa Zanzibar ambaye anafikiri kuwa hakubaliani na mfumo wa CCM basi akaanzishe chama chake.
kumbuka, katika bunge letu la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wakati wanachaguliwa wabunge wa Bunge la Afrika mashariki, wabunge wawili wanawake hawakuwa chaguo la Chadema , waliwaweka tu ili kutimiza swala la genda issue.
Kwa sababu wabunge wa CCM ni wengi, waliamua kuwapa kura hawa wanawake na wakashinda ubunge.
Kura za Chadema zilienda kwa watu wao na hawakushinda kwa sababu ya uchache wao.
Kwa hili hatuwezi kusema CCM waliwachagulia Chadema wabunge.
 
CCM ni NGO ya Mwenyekiti
 
Ok sawa kwa imani uliyonayo
 
CHADEMA ipo kwenye mioyo ya watz wkt ccm ipo kwenye mioyo ya polisi na tume ya uchaguzi.....
Ndio maana ccm wanaogopa time huru, wanaogopa katiba ya wananchi, hawataki chadema wafanye siasa, lkn wanaogopa hata uchaguzi wenyewe maana wanajua hapa tulipo hakuna mkulima, mfanyakazi, mfanyabiashara au mwanafunzi anaweza kuipigia kura ccm.....

Wanahofu sn jamaa
 
Kama Wazanzibar wengi hawaridhii muungano ni swala la muda tu, ipo siku tutagawana fito.
Kwa taarifa yako Wazanzibar wanafaidi muungano kuliko Wabara. Angalia Wapemba walivyojaa Bara wakifanyabiashara na kumiriki hadi ardhi wakati wabara hawaruhusiwi kumiliki ardhi huko Zanzibar. Hivyo raia wa kawaida hawawezi kuvunja muungano labda hao wanasiasa uchwara!
 
Watz wapi hao? Chadema acha ijifie nyenyewe wala msilaumu CCM tabia za viongozi wa Chadema ndiyo shida!
 
Watz wapi hao? Chadema acha ijifie nyenyewe wala msilaumu CCM tabia za viongozi wa Chadema ndiyo shida!
MNAOGOPA NINI?

CHADEMA ipo kwenye mioyo ya watz wkt ccm ipo kwenye mioyo ya polisi na tume ya uchaguzi.....
Ndio maana ccm wanaogopa time huru, wanaogopa katiba ya wananchi, hawataki chadema wafanye siasa, lkn wanaogopa hata uchaguzi wenyewe maana wanajua hapa tulipo hakuna mkulima, mfanyakazi, mfanyabiashara au mwanafunzi anaweza kuipigia kura ccm.....

Wanahofu sn jamaa
 
Mimi nasema hivi: Zanzibar wataendelea kuchaguliwa marais na Tanganyika hadi watakapojitambua na kudai uhuru wao kutoka kwa mkoloni wao mweusi (Tanganyika). Lakini ili koloni hili la Tanganyika lipate uhuru kamili, lazima wazanzibar waudai, hata ikibidi kwa kutumia mtutu wa bunduki. Vinginevyo, watabakwa mpaka Yesu atakaporudi. Ikiwa mbakwaji hapigi kelele maana yake ni kwamba amenogewa na mashine, mwacheni ashughulikiwe tu hakuna namna.
 
Utavunjwa tu(ni muda tu ndio utaongea), hakuna mzanzibar anayetaka MUUNGANO ,hauna faida kwao zaidi ya kuwanyonya tu!!
Hata huku bara hauna fAIDA, wao ndio wanatunyonya.........1 2 3, waende kwao uone jinsi wameziba nafasi za wa-Tanganyika.............muda utasema tuu
 
Inatakiwa kuwe na ushahidi, tutaaminije?
 
Sisi wa Zanzibar hatutarusu Muungano uvunjike kwakua unafaida kubwa kuliko hizo siasa mnazo abudu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…