Kwa nini na kigezo ni kipi?Mkuu,
Tukubali kutokubaliana kwa hili. Hiki hakiwezi kuwa ni kigezo cha umaskini.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa nini na kigezo ni kipi?Mkuu,
Tukubali kutokubaliana kwa hili. Hiki hakiwezi kuwa ni kigezo cha umaskini.
Double standard Government hizi ni mbinu za kutuondoa kwenye mijadala ya Kitaifa na kutulisha habari za kijinga, wakati haya ni matukio ya kila siku kwenye barabara zetu. Why Sharo is so special?
Usisituke mkuu, kusema kweli ni jambo la kawaida marehemu kuibiwa kwenye ajali na ndo maana halisi ya ule msemo kufa kufaana. Na mbaya zaidi sometime hata majeruhi huwa wanamaliziwa ili kupoteza ushahidi. Kuna jamaa yangu ilibidi awambie vibaka, ''Jamani msiniibie mimi bado ni mzima''
Kwa nini na kigezo ni kipi?
We are heading to the promised land, sema grace period ya kufika huko ndo issue. It gonna take us 100 years.God forbid. Sijui kama taifa tunaelekea wapi.
Mkuu wa Wilaya amesema watu warudishe mali za SHARO ikiwemo ngu alizovaa na kwa kuwa wanajulikana waliochukua?!!! Hivi wale waliochukua bag na camera ya Mwangosi si wanajulikana maana walimuua na kuondoka na kila kitu chake? Wamechukuliwa hatua gani kisheria? Niliona familia inakusudio kuidai serikali au niseme Jeshi la polisi!!! Watafanikiwa?? Maovu yamezidi na mbaya zaidi hata vile vyombo vy usalama tunavyoviamini tunaviogopa kama ukoma sasa!!
Mkuu,
makosa ni makosa tu. Hatuwezi kuharalisha kosa kwa kufanya kosa.
Mkuu sijahalalisha kosa ile nimeandika kimafumbo kidogo kuwa vile vya marehemu Mwangosi ilijulikana wazi kabisa vilichukuliwa na nani na hivi pia!! So ni vema fair justice ifanyike!!!
Hili ni jambo la kawaida sana ajali inapotokea.Nakumbuka nilikuwa natoka Dar - Arusha tyre ya mbele ya gari tulilokuwa tukisafiria lilipancha maeneo ya Maili kumi [Korogwe] gari likaacha njia likaingia maporini bahati nzuri halikupinduka ndani ya dakika 5 tulikuwa tumezungukwa na vibaka kama hatukuwa na silaha tungekoma tukapiga risasi moja hewani wakatawanyika.Sasa pata picha Sharo alikuwa mwenyewe,keshakufa ana vitu vizuri nguo,fedha,simu na nk.
Unashangaa nini mambo ya Tanzania ndugu yangu? Kama ukiwa umeumia wanaweza hata kukudhuru zaidi ili wachukue mali zako unashangaa kwa marehemu kuibiwa?Mkuu,
Wow, mbona umenishitua unaposema jambo la kawaida kabisa. Yaani kwa Tanzania marehemu kuibiwa mpaka nguo alizovaa?
Kama una akili timamu hata wewe unaweza kumiliki silaha.Mkuu hiyo silaha yako unakodisha?
Double standard Government hizi ni mbinu za kutuondoa kwenye mijadala ya Kitaifa na kutulisha habari za kijinga, wakati haya ni matukio ya kila siku kwenye barabara zetu. Why Sharo is so special?
Mijadala ya kitaifa inafanyika wapi...miafrika bana. Huyu dogo kuibiwa vitu vyake baada ya ajali ni habari ya kijinga.
Rekebisha kichwa cha habari. Wizi umetokea baada ya ajali na si kabla ya ajali. Ina maana alikuwa anaendesha gari akiwa tayari alishaibiwa nguo.