Huu mchezo wa kula nyama mwisho ameuanzisha nani kwani?

Huu mchezo wa kula nyama mwisho ameuanzisha nani kwani?

lwambof07

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2016
Posts
4,643
Reaction score
5,335
Hellow JF

Kuna haka katamaduni unakuta mfano mpo kwenye sherehe wageni waalikwa mumeenda kuchukua msosi buffet ya maana kabisa sahani imejaaa kwenye kula sasa ataanza na aina nyingine nyingine nyama hata ikisogea ule upande anaomega itarudishwa juu au pemben ya sahani.

Lengo likiwa ni kuila ya mwisho kabisa baada ya vingine kuliwa hii sio kwenye sherehe tu hata majumban pia mwendo ni ule ule ,mimi mwenyewe hata kama nitakula katikati ya msosi au mwanzoni lazima kuna kamoja katapigwa stop kuliwa mwishon.

Huu mchezo ameuanzisha nani kwani??[emoji848][emoji848]na kimeshakuwa kiutamaduni tayari labda mkiwa mnakula kwenye sahani moja sinia hapo nyama itapigwa mapema maana ukizubaa huikutiiiView attachment 2091579
FB_IMG_1642847988327.jpg
FB_IMG_1642847836827.jpg
FB_IMG_1642847826709.jpg
FB_IMG_1642847797148.jpg
FB_IMG_1642847860523.jpg


FB_IMG_1642847988327.jpg

View attachment 2092776
 
Unafanya wanaosubiria mshahara wajiume ulimi Kuna watu Kama nawaona jinsi walivyo na hamu ya kutafuna kuku leo Kama kikitoka au kitimoto
 
Huo mchezo niliuacha tangu nikiwa sekondari badaaa ya kumuangalia mtu akila na kuona kuwa ni jambo la ajabu sana kwa mtu ambaye anajitambua akikuona anaweza kukuona wa ajabu tu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Wewe utakuwa unakula nyama za mawazo,mimi huwa nashangaa sana watu wanaokula nyama mwisho,utaratibu wangu ni tonge nyama mpaka chakula kiishe,kama umeweza kula chakula chote bila nyama manake unaweza kuishi kwa mchuzi tu.
 
Wewe utakuwa unakula nyama za mawazo,mimi huwa nashangaa sana watu wanaokula nyama mwisho,utaratibu wangu ni tonge nyama mpaka chakula kiishe,kama umeweza kula chakula chote bila nyama manake unaweza kuishi kwa mchuzi tu.
Hongera yako yaan haijalishi kuna nyama kiasi gan mkuu ukiwa hata kwenye sherehe wewe chunguza utaona wadau
 
Kwetu sisi ni mwendo wa tonge nyama tonge nyama
 
Back
Top Bottom