Quran 22:7
Na kwamba hakika Saa itakuja hapana shaka kwa hilo, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini.
Allah atakuja kufufu waliokufa lakini pia kumbuka hii imekuja kuandikwa miaka 600 baada ya Yesu.
Tukienda kwenye Biblia yetu mnayosema ime chakachuliwa japo Quran haiwaungi mkono,tena ni mafundisho makongwe kuliko yenu.
Yohana 5:21
Kama vile Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo Mwana huwapa uzima wale awapendao.
Hapa Yesu anasema kama Mungu baba anavyo wafufua wafu basi hata mwana (Yesu) pia anawafufua wale anaowapenda.
Yohana 5:25
Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.
Anaye fufua wafu siku ya mwisho ni nani? Yesu.
Atawaita na sauti yake wataisikia na kufufuka.
Haya ni maneno ya Yesu miaka 600 kabla ya Mohamed ambayo amekopi na kuyaweka kwenye Quran 22:7. Usirudie tena kuuliza kama Yesu ni Mungu chief.
Kosa la Biblia kuhusu mwisho wa nyakati
Soma hii kutoka biblia
Mathayo 24
1Yesu akatoka Hekaluni, akaenda zake, wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya Hekalu.
2Yesu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambia, halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.
3Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakamwuliza, "Tuambie mambo haya yatatukia lini?" na ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?
4Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni mtu asiwadanganye.
5Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye Kristo; na watawadanganya wengi.
6Mtasikia juu ya vita na fununu za vita, angalieni msifadhaike;
7Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme;
8Haya yote ndiyo mwanzo wa utungu.
9Ndipo watawasaliti ninyi mpate dhiki, na kuwaua, nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
10Ndipo watu wengi watajikwaa na kusalitiana na kuchukiana.
11Na manabii wengi wa uongo watatokea na kuwapotosha wengi.
12Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.
13Lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka.
14Na hii Habari Njema ya Ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
15Basi, mtakapoliona chukizo la uharibifu, lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu, (asomaye na afahamu).
16Wakati huo walioko Uyahudi na wakimbilie milimani.
17Yeye aliye juu ya paa asishuke kuchukua kitu katika nyumba yake.
18Wala aliye shambani asirudi nyuma kuchukua nguo zake.
19Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha siku hizo!
20Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya Sabato.
21Kwa maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hadi sasa, wala haitakuwapo kamwe.
22Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote;
23Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule; usiamini.
24Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
25Tazameni, nimekwisha kuwaambieni.
26Kwa hiyo wakiwaambia, Tazama, yuko nyikani; msitoke nje; tazama, yumo katika vyumba vya siri; usiamini.
27Kwa maana kama vile umeme utokeavyo mashariki na kumulika hata magharibi; ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
28Kwa maana popote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.
29Mara baada ya dhiki ya siku hizo, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka kutoka mbinguni, na nguvu za mbingu zitatikisika.
30Ndipo itakapotokea ishara ya Mwana wa Adamu mbinguni;
31Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya wateule wake kutoka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu hadi mwisho huu.
32Basi jifunzeni mfano kwa mtini; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
33Vivyo hivyo nanyi, myaonapo hayo yote, tambueni kwamba yu karibu, milangoni.
34Amin, nawaambieni, kizazi hiki hakitapita mpaka mambo haya yote yatimie.
35Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
36Lakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, hata Baba yangu peke yake.
Baada ya kusoma Mathayo sura ya 24 msomaji ataona jinsi biblia inavyosema: Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie.
Hii ingemaanisha kwamba unabii wa mwisho wa wakati (ujio wake wa pili wa Yesu na maangamizi ya kifo kuwa hai) unapaswa kutokea katika karne ya kwanza (wakati wa kizazi ambacho Yesu alizungumza nacho katika Biblia),