Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Ni mara kadhaa nimekuwa nikitumia mfumo huu wa ardhi kufanya maombi mara kadhaa bila mafanikio, kuomba upimaji, kuomba hati miliki, n.k.
Unaanza vizuri ila uwezi kumaliza mchakato wowote wa maombi ya aina yoyote bila kukutana na error au failure. Error codes zimejaa katika mfumo mzima, si Web version au Mobile Application.
Nimefanya maombi ya Kuomba kupimiwa ardhi, picha linaanza kuweka wahusika tu napewa errors code, mara ukitoka ukirudi unaanza upya, nimepambana hivyo hivyo nikafika kwenye ku-attache Documents... kuna sehemu ya ku-generate "Land Services Application Form" hili ujaze kisha uweke tena. Hapo kwenye ku-generate ukibonyeza inaandika "Failure", uwezi kuendelea na mchakato.
Hii changamoto ya errors kwenye system nimeiona karibia kwenye maombi mengi ya mfumo huu, nimejaribu kusoma comments katika kurasa za wizara ya ardhi nimegundua changamoto hii wanayo watu wengi, kiasi kwangu watu wanaka tamaa na kuachana na mfumo huu wakisubiri neema ya bwana. Mfumo ni mzuri ila sio rafiki kutokana na errors kibao.
Simu zenyewe hazipatikani, huduma kwa wateja rating yake ni sufuri, ukienda ofisi za ardhi hawakusaidii chochote zaidi ya kukwambia pambana na mfumo.
Ebu Waziri wa Ardhi na menejimenti ya ardhi kwa ujumla Wizara ya Ardhi mkaliangalie hili, watu wanakwamishwa na huu mfumo kufanya maombi mbalimbali kama vile ya upimiwaji, hati miliki n.k... Matapeli wanatumia ubovu huu wa mfumo kuwapiga pesa wananchi.