Huu Mkataba siyo Intergovernmental, Dubai siyo Nchi

Hoja zako nyingi ninazielewa na kuzikubali, mkataba una matatizo mengi, ukisoma hiyo article utaona kabisa mkakati wa UAE wa ku monopolize biashara ya logistics/ bandari, na sisi tunawapa monopoly ya bandari zote, that is a single point of failure.

Makubaliano hayana clear end date, Tanganyika Law Society wamechambua vizuri sana, kifungu kwa kifungu.

Mkataba una matatizo mengi sana tunayoweza kuzungumza.

Lakini, hii point ya kwamba Dubai hawana nguvu ya kusaini intergovernment agreement ni very weak na a big distraction, kwa sababu tushaona UAE inafanya kazi kimkakati na Dubai/ DPW, sasa utafikiri watakosa kuidhinisha? Hawawezi.

So, tuongelee mapungufu ya IGA na jinsi ya kujiondoa katika IGA hii.

Habari za kusema Dubai haina nguvu za kusaini mkataba ni distraction tu.
 
Mkuu,

I'm just seeing this unfinished business. Nilikuwa natafuta mitanange ambayo haijaisha bado.Huu mtanange haujaisha.

Hujui makubaliano ya Dubai na UAE yakoje, hujui kama ni ya siri au wazi, hujui business strategy na risk management approach yao ikoje, you are arguing from a position of ignorance. And by that I simply mean lack of information. Your whole argument is based on information you do not have, not information you have.

Yani ni hivi, kungekuwa na habari, au document inayoonesha UAE wanapinga hili suala na kusema kwamba Dubai haiwezi kuingia IGA, kwa sababu UAE haijaidhinisha, hapo ungekuwa na point.

Lakini, hakuna habari hiyo. Sasa kama UAE wenyewe wako poa na hawajaraise any issue, wewe nani uje u raise hii issue ya UAE? Nani kakuchagua wewe uwe wakili wa UAE?

Unaamini kabisa kwamba Dubai, na mtandao wao wote wa kimataifa, na huyo Emir wao kuwa Prime Minister wa UAE, na ma lawyers wao wote, wataenda kufanya rookie mistake hii na kuacha loophole ya kufanya mkataba uwe null and void on a small technicality kama hii?

Halafu kwa nini Watanzania wanashikia bango hili wakati this is a matter for Dubai and the UAE? Na mambo mengi hayawekwi wazi, hata haya makubaliano ya IGA tu hayakutoka kwa njia rasmi, yamevuja.

Unabishaje kuwa Dubai kimsingi haijapewa idhini wakati sisi tumeona document moja tu, documents ambazo hatujaona ni nyingi sana?
 
Nashjndwa kuelewa kabisa, kwanini Rais Samia analazimisha hii issue ya bandari..

Ana maslahi gani ?

Anatuonaje sisi watanganyika? Wapumbavu au?

Kwanini baada tuu ya Magufuli kufariki, wamasai loliondo waliondewa kwa nguvu kupisha waarabu?
 
Inabidi waje waeleze kwanza uhalali wake wa dubai-mkoa ndani ya UAE kuitwa ni IGA. Huwezi ingia mkataba na mkoa na nchi ukaitwa IGA.
Ingekua heri hata wangesaini na Dubai, ukweli ni kwamba mkataba ni IGA ila umesainiwa kati ya serikali ya Tanzania na DP world.. sijui tunaakili gani Watanzania.
 
Dubai is a state, na ina serikali yake Emirate with full powers na Mfalme ni absolute Monarchy, kila kitu kiko owned na Mfalme.
 
Wana Jamii Forums endelea kutuhabarisha na kutuelewesha.
 
DP world ndio tumesaini nao mkataba, hata sio serikali ya dubai
Mkuu umeisoma IGA? Page ya 4 mwanzo kabisa?

Umesoma ukurasa wa 34 kwenye saini?

Umesoma instruments of power pages 37 na 38?
 
Kwanini huu mkataba wanauita IGA wakati haukidhi matakwa ya kuitwa hivyo? Nasimama kuelimishwa.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani ili kitu kiitwe IGA inabidi kiweje kwa uelewa wako?

Unaposema mkataba haukidhi matakwa ya kuitwa IGA, unamaanisha matakwa gani?
 
Siku mkigombana na Rwanda kwa Mfano na hapo UAE au Dubai wakaamua kiwasaidia Rwanda still hamuwezi kuwafanya chochote. Inshort wanaweza hata kutumia hizo bandari zenu Kuingiza silaha kwa ajili ya adui yenu and you can't do shit about it.
 
Tushirikiane watanganyika kukataa wazanzibar kuuza bandari zetu.
Kama mkataba ni kwa manufaa kwanini bandari za Zanzibar hazijajumuishwa kwenye mkataba sijui makubaliano haya??
Hakuna mkataba usiokua na ukomo huo ni uuzaji.
Ukisoma wameuza hadi Anga [emoji23][emoji23] ndio maana ya territory
 
Can Dubai on its own enter the intergovernmental agreement ?
Ndio maana yule mburushi akasema Mahakama zetu hazina meno Mahakama na watendaji wake ni vibaraka wa Serikali mbele ya Serikali Mahakama hazina la kusema akitolea mfano Mahakama ya Kisutu ikiwa ni mfano hai wa Mahakama zote, ina maana wanasheria wetu wa ndani hawajaliona hilo au majaji na mahakimu hawajiliona hilo au wanalinda vibarua vyao walivyopewa na Serikali hawataki kutenda kinyume na Serikali hata km wanaona Serikali inakosea au inatenda kinyume na sheria ? Kongole nampa yule mama jaji jina lake limenitoka

404: Page Not Found
 
Kazi kweli kweli...
 
Ndio shida ya kuongozwa na mtu mwenye elimu ya kuungaunga! Masijala na mambo gani sijui!
Sasa mkataba ataweza kuusoma na kuelewa kweli!?
Tatizo sio yeye SSH tatizo ni wasaidizi wake wakiwemo wanasheria wa Serikali kuna mwanasheria Mkuu wa Serikali inamaana unataka kusema kabla haujasainiwa hawakushirikishwa na yeye mwanasheria Mkuu ameukingia kifua huo MKATABA bila kuelewa kua Dubai sio Nchi ni MJI haiwezi kua IGA km Nchi 1 inaingia MKATABA na MJI mmoja wa Dubai inamaana mwanasheria Mkuu wa Serikali hakuona hayo mapungufu ya mkataba ?

404: Page Not Found
 
Kitanzania washauri ndio wanashauriwa na rais, halafu kauli ya rais haipingwi.
 
Kitanzania washauri ndio wanashauriwa na rais, halafu kauli ya rais haipingwi.
Kwa hio unataka kusema walimwambia huu mkataba mbovu alafu yeye saa100 akakomaa kusema niacheni najua ninachokifanya msinipangie cha kufanya mimi ndio rais ? Ndio unamaanisha hivyo ?

404: Page Not Found
 
Kwa hio unataka kusema walimwambia huu mkataba mbovu alafu yeye saa100 akakomaa kusema niacheni najua ninachokifanya msinipangie cha kufanya mimi ndio rais ? Ndio unamaanisha hivyo ?

404: Page Not Found
Samia watu wa Usalama wa Taifa wamemuendea wakamwambia Mama mwanao anaonekana ana hela nyingi sana, hili kinaweza kuleta matatizo.

Akawajibu, sasa mnataka nifanye nini? Nimkamate mwanangu?

Watu wa Usalama wakanywea.

Sasa hapo utawalaumu watu wa Usalama?

Huu mkataba umekuwa firced top down, ndiyo maana haujabadilishwa hata nukta.

Hao wanasheria wote wa serikali na maofisa waandamuzi wamepewa amri wapitishe kila kitu kama kilivyo, na hakuna mwenye uthabiti wa kujiuzulu na kusema madudu.
 
In theory serikali ya Dubai haiwezi kusaini mkataba wa IGA na nchi ya kigeni bila idhini ya serikali ya UAE (ibara ya 120 ya katiba ya UAE), na mahusiano ya kidiplomasia hapa ni kati ya Tanzania na UAE. Serikali ya UAE itakuwa imeidhinisha mkataba, sema mkataba uko vague ingekuwa vizuri mahusiano ya kidiplomasia yakatajwa kuwa ni kati ya Tanzania na UAE. Peter Madeleka ameongelea hili sana, nafikiri na analysis ya TLS imegusia if I am not mistaken.

Serikali ya UAE ime devolve powers zake kwa serikali ya Dubai.

Zaidi ya hapo, hii ni clause standard katika mikataba mikubwa ya kimataifa. Mantiki yake ni kwamba, muwekezaji aweze kuwekeza fedha nyingi kwenye mradi bila kuogopa matatizo ya kidiplomasia kumuingilia katika uwekezaji wake.

Otherwise, ukitaka kuvunja mkataba unatangaza mgogoro wa kidiplomasia na UAE, unafukuza balozi, unasema mkataba umevunjika kwa kuwa mahusiano ya kidiplomasia yamekwisha, which is pretty ridiculous.
 
Kwa hio mzigo huu unamuhusu yeye mwenyewe sio wanasheria wa Serikali, aliwahi kusomea Sheria kwani ?

404: Page Not Found
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…