Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Hoja zako nyingi ninazielewa na kuzikubali, mkataba una matatizo mengi, ukisoma hiyo article utaona kabisa mkakati wa UAE wa ku monopolize biashara ya logistics/ bandari, na sisi tunawapa monopoly ya bandari zote, that is a single point of failure.Ndugu mimi ni muumuni wa uchumi huru, serikali za kiafrika zimefeli kuendesha hata mashirika muhimu kwa usalama (mfano nishati). Africa ya kusini wanahangaika na shirika lao (kwangu mimi ni uafrika ndio tatizo). Kuleta muwekezaji bandari ili kuongeza tija kwa nchi hapo hakuna tatizo. Tatizo ni lilelile la muda wote kuwa wawekezaji wa nje ndio jibu letu ( kwa mfano umeona mwenyewe UAE wanatumia kimkakati DPW!) Hiyo mikakati kwa kawaida ni kwa usalama na faida yao kwanza!.
Kama DPW inatumiwa kimkakati, kwanini sasa tuseme wamekuja tu kuongeza tija kwetu? Vipi mikakati hiyo ya UAE ikiwa ni hatari kwetu ( kupoka uhuru wetu?) Kwanini utata huu (ambao hata wewe umewanukuu TLS) usitatuliwe kwanza na mengine mengi yanayopigiwa kelele na wenye nchi (kama KWELI ni wenye NCHI) yasitatuliwe?
Nchi imegawanyika katika hili (na historia ya nyuma ni mwalimu mzuri), kwanini tuende tu na migawanyiko hii? Kumbe Zanzibar ilikosea ila kosa hilo lilikuwa linawapa faida Zanzibar ila hatari kwa muungano! Vipi ikiwa DPW wamekosea ila kosa hilo linawapa faida wao wenyewe na UAE na hatari kwetu, unadhani UAE watakuja ku- claim? (Kumbe ndo ile maana ya hata uhusiano wa kidiplomasia ukiharibika baina ya nchi huu MKATABA hauvunjiki!)..maana siku tukijajua tuliingizwa chaka kuwa Dubai ni nchi na tukaanza kupishana na UAE, mkataba utaendelea kutudunda tu!
Makubaliano hayana clear end date, Tanganyika Law Society wamechambua vizuri sana, kifungu kwa kifungu.
Mkataba una matatizo mengi sana tunayoweza kuzungumza.
Lakini, hii point ya kwamba Dubai hawana nguvu ya kusaini intergovernment agreement ni very weak na a big distraction, kwa sababu tushaona UAE inafanya kazi kimkakati na Dubai/ DPW, sasa utafikiri watakosa kuidhinisha? Hawawezi.
So, tuongelee mapungufu ya IGA na jinsi ya kujiondoa katika IGA hii.
Habari za kusema Dubai haina nguvu za kusaini mkataba ni distraction tu.