Huu Moto wa Katiba Mpya naona umekolea sana nchi nzima

Huu Moto wa Katiba Mpya naona umekolea sana nchi nzima

Cathelin

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
2,071
Reaction score
3,995
Kwanza inabidi tukubali kuwa CCM walifanya kosa kubwa saana la kuiba uchaguzi kishamba last year. Kupitia wizi ule ndo maana wazo la katiba liliibuka na kwa hali ilivyo sioni wa kuuzima huu Moto .

Freeman Mbowe baada ya kuanza makongamano, serikali ikaona solution ni kumpa bogus terrorism charges, wakiamini watakuwa wamauzima Moto wa katiba, lakini toka Mbowe awekwe ndani naona hoja ya katiba ime-gain momentum, mfano sahivi haiwezi pita siku mbili bila magazeti makubwa kuandika Mambo ya katiba mpya Tena front page.

CCM na ACT wameamua wajikoshe kwa kuja na tume huru, unadhani ni kwanini? Ni kujaribu kuzima Moto wa katiba mpya, mitandaoni pote ni katiba,katiba,katiba.

Ujio wa Lissu mwaka huu nao utakoleza Moto kwenye madai ya katiba, Sasa ni serikali ijipange ama kumuacha Lissu aendelee na Moto wa katiba, au wamuweke ndani na kumpa kesi Kama Mbowe(hapa nadhani haiwezekani serikali haiwezi kufanya kosa Mara mbili).

Vyovyote itakavyo kuwa upuuzi wa Magufuli last year ndo umeibua huu Moto wa katiba, na huu Moto utasubiri ata miaka 2,4,10 Ila katiba itaandikwa tu.
 
Ninavyoona Lissu akituaa tuu, watamfanyia kama Mbowe,
Bado h aitakuwa dawa ya kuizuia kupatikana katiba ya wananchi, yenye maoni ya wananchi kweli kweli na sii yenye maino na maslahi ya Wana ccm pekee kama walivyojaribu kufanya .
 
Haiwezekani mtu akope trillion 8 halafu anajiamulia tu kuzipeleka Zanzibar bila ruhusa ya bunge na hakuna wa kumuuliza wala kumfanya kitu chochote ili kumuwajibisha, sasa ni katiba gani hiyo?!
Hii Katiba ya kijinga iliyopo ilivyoamua Rais asishtakiwe kwa chochote atakachofanya akiwa madarakani pale ndio ilijishusha ikamuweka Rais juu yake, ndio maana kila siku wanavunja sheria sababu wanajua wanalindwa na sheria pia.
 
Kwanza inabidi tukubali kuwa CCM walifanya kosa kubwa saana la kuiba uchaguzi kishamba last year. Kupitia wizi ule ndo maana wazo la katiba liliibuka na kwa hali ilivyo sioni wa kuuzima huu Moto...
Hakuna cha Katiba mpya itakayopatikana.
 
Haiwezekani mtu akope trillion 8 halafu anajiamulia tu kuzipeleka Zanzibar bila ruhusa ya bunge na hakuna wa kumuuliza wala kumfanya kitu chochote ili kumuwajibisha, sasa ni katiba gani hiyo?!
Ndo tuungane kuleta katiba mkuu
 
Hii Katiba ya kijinga iliyopo ilivyoamua Rais asishtakiwe kwa chochote atachofanya akiwa madarakani pale ndio ilijishusha ikamuweka Rais juu yake, ndio maana kila siku wanavunja sheria sababu wanajua wanalindwa na sheria pia.
Katiba ya kishenzi kabisa
 
Nauliza tu!
Tunataka Katiba Mpya au Mkutano wa Katiba??
Ref; Hivi leo Bunge Hili Tulilo nalo wakikaa na na kukokotwa wakatupa Katiba Mpya!;
Tunadai nini??
 
Back
Top Bottom