Huu Moto wa Katiba Mpya naona umekolea sana nchi nzima

Huu Moto wa Katiba Mpya naona umekolea sana nchi nzima

Mkuu hebu jiulize awali dogo tu: Ni nini kilichomuibua Ndugai huko aliko na kuanzia harakati za kutaka kutenganisha Mhimili wa Bunge na ule Uliojichimbia chini zaidi??? Ukipata jibu jiulize tena, je hatima ya sakata lile ni nn kitatokea??
Ndo vizuri
 
Hv mbna yule kubwa la maadui alifanya alivyojickia na kudai yy hapangiw
Haiwezekani mtu akope trillion 8 halafu anajiamulia tu kuzipeleka Zanzibar bila ruhusa ya bunge na hakuna wa kumuuliza wala kumfanya kitu chochote ili kumuwajibisha, sasa ni katiba gani hiyo?!
 
Haiwezekani mtu akope trillion 8 halafu anajiamulia tu kuzipeleka Zanzibar bila ruhusa ya bunge na hakuna wa kumuuliza wala kumfanya kitu chochote ili kumuwajibisha, sasa ni katiba gani hiyo?!

Kuna trillion 8 imekopwa nje na ile 1.3 ya Uviko?
 
Bunge linanguvu kuliko rais, lilipiga kura imeisha hiyo
Huna unachokijua,Rais ndio kila kitu Tzn hapa,Tunisia Rais alifutilia mbali Bunge na Waziri Mkuu Kisha anaongoza Nchi Kwa executive order shida ni spika na pm walikuwa hawaelewani.

Hadi saizi yupo,inategemea vyombo vya Dola vimeegemea wapi na Kwa kwetu viko na amir jeshi mkuu wao kwa hiyo hakuna wa kuleta fyoko.

Enzi za Nyerere watu walitaka kupindua Muungano wakatokomezwa achilia mbali walioharibu mara kadhaa kumpindua.

Point ya msingi nani ataanzisha hayo unayotaka yatokee? Wabunge wengi wako na Samia kawapa mapesa kibao majimboni sijui wewe unasemaje hapo.
 
Shida ni kwamba kila mtu ana ya kwake anayotaka yawe kwenye katiba hiki kinapelekea kuwa na "Constitution Hijack" na hii inafanya jamii kubwa ya watanzania kutojua nini kilichopo kwenye katiba na kwanini tuibadilishe.

Wapo ambao hata mchakato wa katiba mpya ukiletwa watateka Yaliyomo iwe imejaa ya kwao na kuwa blind watanzania walio wengi.

Iwapo wanasiasa ndio wenye nguvu ya kuingiza ya kwao katika katiba basi hiyo katiba mpya ni heri isiwepo, ila kama hoja za wananchi ndio kipaumbele basi iwepo.

Maana kunaweza kukawa na kupigia kura kablasha ambalo watu wachache wameandaa kwa vikao vya kukaa kumbi za hoteli za miji mikubwa badala ya kuwa na vikao vya chini ya mwembe vijijini ambako watanzania wengi wapo.
 
Kosa lilianza 2014 baada ya 'wajanja' kumpanga JK na kuvuruga ule mchakato kupitia lile Bunge la Katiba.
Nakumbuka kuna siku nilishindaa njaa ili kuwasubiri wajumbe wa Tume ya Katiba ili nitoe maoni.
Huu upuuzi wa kudharau maoni ya wananchi umekuwa kansa, ndio maana hata sanduku la kura haliheshmiki.
Katiba yenye kulinda haki na mali za raia, udhibiti thabiti wa viongozi na vyombo kama polisi, serikali tatu, n.k
 
Ivi Ni Kwanini Ccm Wanaogopa Katiba Mpya Ilihari Wao Ni Viongozi Pendwa Wa Wanyonge[emoji848]

Wapi CCM kasema anaogopa. Kwani katiba mpya Ni swala la katiba mpya au swala Ni content ya Katiba. Shida ya watu kama wewe Ni kuandika na kupiga kelele wakati hujui nini hasa unachohitaji katika maisha yako Siasa za Africa kutokana na kuendeshwa na mabeberu hasa kiuchumi hazijaweza kunufaisha mataifa moja moja. Ni pale tu Africa ingekubali kuteseka kwa muda na kuungana kibiashara nk. Ndo ukombozi wetu utapatikana. Otherwise ni katiba iwe mpya au ya zamani wananchi tunataka maendeleo na Sisi wenyewe tuna role kubwa sana ya kuplay.

Tz Sasa inahizaji kuangalia Elimu na mitaala na wanafunzi wanapaswa kufundishwa kuwa analytical sio kukariri tu kwa ajili ya mitihani.

Afya. Dawa zinanuniliwa Lakini Sisi madaktari na manurse wengine ccm au CHadema au Act kiitikadi wanaiba na tunawaona Mashujaa wakijenga majumba haraka kwa kuuza dawa na vifaa tiba. Hii hahitaji katiba mpya. Unahitaji wewe na mimi tubadilke. Rais hawezi Control mawazo yangu mimi kama daktari au nurse.

Kilimo Pia. Maamuzi magumu. Nk.

Process ya Katiba mpya Ni gharama sana. Mwaka huu kuna sensa. Hii ndo jambo MUHIMU. Ila ushamba na kutaka sifa kijinga ndo watu kama nyie mnatumika. Ukitaka kujua mwanasiasa Bora na kweli mwenye nia njema na Taifa Sio tumbo lake soma mahali kama ajenda ya sensa ya mwaka huu ameitaja na kuipongeza popote, ama kuongeza namna ya kuiboresha ili nasi Tuwe kama nchi za ulaya na marekani nk kuwa kila mtu anajulikana anakaa wapi, anafanya nini , nyumba nk. Hii ndo jambo muhimu sana Kwa mipango na maendeleo ya nchi hasa maskini.
 
Kosa lilianza 2014 baada ya 'wajanja' kumpanga JK na kuvuruga ule mchakato kupitia lile Bunge la Katiba.
Nakumbuka kuna siku nilishindaa njaa ili kuwasubiri wajumbe wa Tume ya Katiba ili nitoe maoni.
Huu upuuzi wa kudharau maoni ya wananchi umekuwa kansa, ndio maana hata sanduku la kura haliheshmiki.
Katiba yenye kulinda haki na mali za raia, udhibiti thabiti wa viongozi na vyombo kama polisi, serikali tatu, n.k
 
Kosa lilianza 2014 baada ya 'wajanja' kumpanga JK na kuvuruga ule mchakato kupitia lile Bunge la Katiba.
Nakumbuka kuna siku nilishindaa njaa ili kuwasubiri wajumbe wa Tume ya Katiba ili nitoe maoni.
Huu upuuzi wa kudharau maoni ya wananchi umekuwa kansa, ndio maana hata sanduku la kura haliheshmiki.
Katiba yenye kulinda haki na mali za raia, udhibiti thabiti wa viongozi na vyombo kama polisi, serikali tatu, n.k
Uwoga wa watanzania ndo unafanya watawala waamue watakalo
 
Katiba mpya ndio inahitajika lakini ndugu zangu hakikisheni hiyo katiba inakaliwa na watu wazuri alasivyo hutatatoka kwenye hili Lindi
Maana ya katiba nzuri ni kuzuia uharibifu wa nchi kwa kiwango kikubwa inapotekea watu wabaya wamekalia viti vya mamlaka.
 
Ivi Ni Kwanini Ccm Wanaogopa Katiba Mpya Ilihari Wao Ni Viongozi Pendwa Wa Wanyonge[emoji848]

Wanaujua ukweli lakini wao wameamua kuuishi uongo. Wako tayari kusimama kwenye uongo hata kama utawaletea msiba! Hilo ni sikio la kufa.

Na mashabiki wao kutwa kucha kazi ni kumtukuza kiongozi kwa msimamo usioyumba na uthubutu kwenye maamuzi potofu yanayoweza hata kusababisha maafa.
 
Kwanza inabidi tukubali kuwa CCM walifanya kosa kubwa saana la kuiba uchaguzi kishamba last year. Kupitia wizi ule ndo maana wazo la katiba liliibuka na kwa hali ilivyo sioni wa kuuzima huu Moto .

Freeman Mbowe baada ya kuanza makongamano, serikali ikaona solution ni kumpa bogus terrorism charges, wakiamini watakuwa wamauzima Moto wa katiba, lakini toka Mbowe awekwe ndani naona hoja ya katiba ime-gain momentum, mfano sahivi haiwezi pita siku mbili bila magazeti makubwa kuandika Mambo ya katiba mpya Tena front page.

CCM na ACT wameamua wajikoshe kwa kuja na tume huru, unadhani ni kwanini? Ni kujaribu kuzima Moto wa katiba mpya, mitandaoni pote ni katiba,katiba,katiba.

Ujio wa Lissu mwaka huu nao utakoleza Moto kwenye madai ya katiba, Sasa ni serikali ijipange ama kumuacha Lissu aendelee na Moto wa katiba, au wamuweke ndani na kumpa kesi Kama Mbowe(hapa nadhani haiwezekani serikali haiwezi kufanya kosa Mara mbili).

Vyovyote itakavyo kuwa upuuzi wa Magufuli last year ndo umeibua huu Moto wa katiba, na huu Moto utasubiri ata miaka 2,4,10 Ila katiba itaandikwa tu.
Mtu anayezungumzia katiba mpya namuona ana utoto tu! Hii inatokana na ukweli kuwa hii iliyopo inavunjwa kila mara, je hiyo mpya nani ataisimamia? Aidha kumbuka hakuna binadamu ambaye anaweza kuingiza kichwa chake katika mdomo wa mamba mwenye njaa. Samia leo hii asaini katiba itakayompeleka mahakamani kwa matendo yake baada ya kung’atuka? Mpuuzi kama Tundu Lissu ndiye ataamini katika katiba mpya
 
Kosa lilianza 2014 baada ya 'wajanja' kumpanga JK na kuvuruga ule mchakato kupitia lile Bunge la Katiba.
Nakumbuka kuna siku nilishindaa njaa ili kuwasubiri wajumbe wa Tume ya Katiba ili nitoe maoni.
Huu upuuzi wa kudharau maoni ya wananchi umekuwa kansa, ndio maana hata sanduku la kura haliheshmiki.
Katiba yenye kulinda haki na mali za raia, udhibiti thabiti wa viongozi na vyombo kama polisi, serikali tatu, n.k
Poleeee
 
Back
Top Bottom