Huu mstari wa Biblia Umeniacha mdomo wazi

Huu mstari wa Biblia Umeniacha mdomo wazi

excel

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
22,463
Reaction score
17,954
Je, Hii Nchi ya Tiro Bado Ipo?
Kama Haipo, Je Huu ukahaba Tiro alishaufanya?


FB_IMG_1748626683540.jpg

========
Isaya 23:15-18
[15]Basi, itakuwa katika siku ile, Tiro utasahauliwa miaka sabini, kadiri ya siku za mfalme mmoja; hata mwisho wa miaka sabini, Tiro utakuwa kama vile ulivyo wimbo wa kahaba.

And it shall come to pass in that day, that Tyre shall be forgotten seventy years, according to the days of one king: after the end of seventy years shall Tyre sing as an harlot.

[16]Twaa kinubi, tembea mjini,
Ewe kahaba uliyesahauliwa;
Piga vizuri, imba nyimbo nyingi,
Upate kukumbukwa tena.

Take an harp, go about the city, thou harlot that hast been forgotten; make sweet melody, sing many songs, that thou mayest be remembered.

[17]Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia.

And it shall come to pass after the end of seventy years, that the LORD will visit Tyre, and she shall turn to her hire, and shall commit fornication with all the kingdoms of the world upon the face of the earth.

[18]Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.

And her merchandise and her hire shall be holiness to the LORD: it shall not be treasured nor laid up; for her merchandise shall be for them that dwell before the LORD, to eat sufficiently, and for durable clothing.
 

Attachments

  • 1748673431871.png
    1748673431871.png
    373.4 KB · Views: 36
06249DBB-1703-488E-A09F-BAFEEFE6BA16.jpeg
Watakuambia uwe na roho mtakatifu ndo uweze kuelewa!
Shida ni kwamba watu weng wakristo au waislam wanachukuaga mstar mmoja wa Biblia.
Ila ukitaka kuelewa maana soma mistar mitatu juu na mitatu chini,
Mstar unaousoma uwe wa katkat.

Huo mstar huyo atakayerud ni Tiro,
(Nchi ya Tiro kurud kama awali baada ya miaka 70 - maana mstar wa 15 umesema itasahauliwa)

Ukisoma mstar unaofuata chini 18 utaelewa.

Pia anzia hapo juu kuna nyimbo imekuwa quoted ya kahaba.
Vyote vinahusu Tiro.

Nadhan umeelewa sasa!.
 
Je, Hii Nchi ya Tiro Bado Ipo?
Kama Haipo, Je Huu ukahaba BWANA alishaufanya?


View attachment 3351267
Isaya 23:17 inaeleza jinsi baada ya kipindi cha maangamizi au adhabu, mji wa Tiro utarejeshwa katika shughuli zake za zamani za kibiashara, lakini bado kwa njia zisizompendeza Mungu. Ni onyo kuhusu kurejea kwenye tabia mbaya hata baada ya kupata rehema.
 
Tatizo mmeshikilia ukahaba na maana yenu moja mnayoipenda.... mbona kata mnaweza kuinyambulisha
 
Je, Hii Nchi ya Tiro Bado Ipo?
Kama Haipo, Je Huu ukahaba BWANA alishaufanya?


View attachment 3351267
Kwanza Soma hapo chini
Isaiah:23

[Isaya 23:17] Yes, after seventy years, the Lord will revive Tyre, but she will be no different than she was before; she will return again to all her evil ways around the world.

Holy Bible (TLB) The Living Bible

Kazi ya Bwana nikuirudishia hadhi yake Tiro. Lakini baada ya kurudishiwa hadhi yake, Tiro haitakuwa tofauti na awali, itazirudia njia zake mbaya, kufanya ukahaba na mataifa mengine.

Badala ya kuandamana na Bwana wake, (hapa sio bwana kama wanawake waswahili wa mtaani muitavyo, hapa ni LORD yaani mtawala) ambaye ni Mungu, yeye Tiro ataandama na njia zake za awali ili kujipatia ujira wake.

Usisome BIBLIA ukiwa na wenge lako kichwani. Unasoma Biblia unawaza ngono unategemea nini?😎
 
Back
Top Bottom