Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,264
Wakuu kwema?
Kuna haka kamtindo kameingia na kanashamiri. Huu mtindo unafanywa na makampuni yanayoshughulika na miamala. Fikiria kampuni yoyote ambayo itakudai hela kupitia mitandao ya simu.
Sasa mashaka yangu yanakujaje? Unakuta unanunua huduma aidha ya maji, umeme, au kisimbuzi. Umeweka hela kisha unaambiwa utaunganishwa na huduma ndani ya saa 48. Hivi kiukweli kabisa bila kupepesa hisia, inawezekana vipi kumcheleweshea mteja huduma kwa saa 48? Yaani siku 2? Yani kwa kitendo tu cha kuminya kitufe kuruhusu huduma ndio inachukua siku 2?
Sasa nawaza tu kwa sauti. Inawezekana kuna dili za watu. Sijui ni zipi ila chale zangu zinaniongoza hivyo. Mfano huduma ya kisimbuzi kwa gharama ya tsh 7000 i alipiwa na wateja laki moja, kisha kila mteja anaambiwa utacheleweshewa huduma kwa saa 48. Yani 7000 x 100,000 = 700,000,000/-. Hizi mil 700 ndani ya saa 12 tu haujafanya biashara ya uchuuzi ambayo itakupa hata faida nusu ya hela yote?
Hakuna lisilowezekana. Watu wanabuni mbinu kila leo. Usione watu mjini wanaishi kama hawafi. Akili mtu wangu. Tunatumika sana kuinua wengine.