Kila jambo lina wakati wake, kwa mfano
Kiranga alisema ameacha nikajiuliza wanawezaje hawa?! Lakini mwisho wa siku niliacha kwa siku moja tu tena jana yake nilikuwa nduki mama kawa. Uongo mbaya nilipata sana tabu ya usingizi kwa siku5 mfululizo ila saivi aah.
Mkuu,
Nashukuru sana kuweza kuonesha nimeacha na jambo hilo kukupa challenge mpaka na wewe ukaacha.
Mara nyingine huwa nafikiri sana kama kusema haya mambo inaweza kuwa kujitapa, au kujionesha kwa watu, lakini nikifikiria watu kama wewe, watu ambao wanaweza kuwa inspired na mtu kusema mambo fulani ya maisha yake, naona tunahitaji kusema.
Mohammed Ali aliwahi kusema kuwa, kama kitu umekifanya kweli, ukisema umekifanya hujajitapa, umesema ukweli tu.
Mwaka huu nimefanya nini mpaka sasa?
Si makubwa sana, ila mchango kuchangizana. Na mimi nitakuwa mtovu wa uungwana kutajwa hapa kama mfano mzuri bila kuleta muendelezo wa habari zangu.
Pengine kuna wengine zitawa inspite zaidi.
Nachangia hivi.
Nimeacha kutumia social media platform moja iliyokuwa inanipotezea muda sana, na nimeweza kuongeza muda wa kusoma zaidi. Nimefikisha challenge yangu ya mwaka ya kusoma vitabu. Nimejiongeza kwenye suala la time management.
Nimerudi gym kwa kasi sana angalau dakika 90 siku tano kwa wiki.
Nimejifunza zaidi mambo ya AI na jinsi ya kutumia AI kufanya scripting kwa different languages.
Nimesaidia vijana kadhaa ada za shule/ vyuo na matumizi mengine ya wanafunzi.
Nimemsaidia kijana mmoja pesa ya nauli na gharama nyingine kwenda Afrika Kusini ambako alikwenda kuchukua visa ya kwenda kusoma kwa scholarship Kazakhstan. Nimemsaidia pia pesa yote ya nauli na ya kuanzia maisha Kazakhstan.
Nimemsaidia kijana mmoja mtaji wa biashara yake.
Nimejiongeza kwenye tax strategy kupunguza kodi na kuongeza ufanisi kwenye investments zangu.
Nimeongeza pesa kwenye trust fund ya familia.
Nimepunguza matumizi katika subscriptions ambazo sizitumii/sizihitaji.
Nimepunguza sana manunuzi ya vitu nisivyovihitaji.
Nimempa dogo mmoja anayeanza kazi gari aweze kuanza vizuri maisha bila ya kuwa na pressure ya kununua gari.
Nimesaidia wazee fulani wa familia kupata bima ya afya.
Nimejitolea muda kufundisha jamii kuhusu ubaya wa datacenters na kujenga movement iliyofanikiwa kuzuia datacenters zisijengwe karibu na ninapoishi.
Nimeanza kazi kufanya institutional coordination kibiashara kati ya taasisi za US/Canada na Tanzania.
Nimeanza kumtayarisha mtoto anayefanya mitihani ya form four Tanzania mwaka huu kupata nafasi ya kusoma chuo chake anachotaka, MIT.
NB: Kutoa ni moyo, usambe utajiri. Kuna mengi nimetoa kwa kujinyima mwenyewe, si kwa sababu ni tajiri kihivyo.