Huu mwaka 2026 ni kama umekwisha umefanya nini cha maana ukikitazama unajivunia?

Mkuu,

Nashukuru sana kuweza kuonesha nimeacha na jambo hilo kukupa challenge mpaka na wewe ukaacha.

Mara nyingine huwa nafikiri sana kama kusema haya mambo inaweza kuwa kujitapa, au kujionesha kwa watu, lakini nikifikiria watu kama wewe, watu ambao wanaweza kuwa inspired na mtu kusema mambo fulani ya maisha yake, naona tunahitaji kusema.

Mohammed Ali aliwahi kusema kuwa, kama kitu umekifanya kweli, ukisema umekifanya hujajitapa, umesema ukweli tu.

Mwaka huu nimefanya nini mpaka sasa?

Si makubwa sana, ila mchango kuchangizana. Na mimi nitakuwa mtovu wa uungwana kutajwa hapa kama mfano mzuri bila kuleta muendelezo wa habari zangu.

Pengine kuna wengine zitawa inspite zaidi.

Nachangia hivi.

Nimeacha kutumia social media platform moja iliyokuwa inanipotezea muda sana, na nimeweza kuongeza muda wa kusoma zaidi. Nimefikisha challenge yangu ya mwaka ya kusoma vitabu. Nimejiongeza kwenye suala la time management.

Nimerudi gym kwa kasi sana angalau dakika 90 siku tano kwa wiki.

Nimejifunza zaidi mambo ya AI na jinsi ya kutumia AI kufanya scripting kwa different languages.

Nimesaidia vijana kadhaa ada za shule/ vyuo na matumizi mengine ya wanafunzi.

Nimemsaidia kijana mmoja pesa ya nauli na gharama nyingine kwenda Afrika Kusini ambako alikwenda kuchukua visa ya kwenda kusoma kwa scholarship Kazakhstan. Nimemsaidia pia pesa yote ya nauli na ya kuanzia maisha Kazakhstan.

Nimemsaidia kijana mmoja mtaji wa biashara yake.

Nimejiongeza kwenye tax strategy kupunguza kodi na kuongeza ufanisi kwenye investments zangu.

Nimeongeza pesa kwenye trust fund ya familia.

Nimepunguza matumizi katika subscriptions ambazo sizitumii/sizihitaji.

Nimepunguza sana manunuzi ya vitu nisivyovihitaji.

Nimempa dogo mmoja anayeanza kazi gari aweze kuanza vizuri maisha bila ya kuwa na pressure ya kununua gari.

Nimesaidia wazee fulani wa familia kupata bima ya afya.

Nimejitolea muda kufundisha jamii kuhusu ubaya wa datacenters na kujenga movement iliyofanikiwa kuzuia datacenters zisijengwe karibu na ninapoishi.

Nimeanza kazi kufanya institutional coordination kibiashara kati ya taasisi za US/Canada na Tanzania.

Nimeanza kumtayarisha mtoto anayefanya mitihani ya form four Tanzania mwaka huu kupata nafasi ya kusoma chuo chake anachotaka, MIT.

NB: Kutoa ni moyo, usambe utajiri. Kuna mengi nimetoa kwa kujinyima mwenyewe, si kwa sababu ni tajiri kihivyo.
 
Zimebaki siku chache sana mwaka 2026 uishe je umefanya nini cha maana ukikitazama unajivunia na kufurahia?

mimi binafsi plan zangu zimetimia kwa at least 30%

View attachment 3691545

#Welcome 2027
kwa sisi wakulima hodari na watumishi wachapakazi wa wananchi,

kwakweli tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu, kutujaalia na kutufanikisha yale yote ambayo tulipanga kuyafanya mwaka huu 2026. Mathalani, tulilima kwa mashaka kidogo, lakini mavuno tumepata vizuri sana kwakweli, mifugo imezaliana na kuongezeka vizuri, bei na masoko ya mazao ya kilimo na mifumo ni nzuri sana, wengi tumefurahi katika eneo hilo.

Kwa neema na Baraka za Mungu,
ni wazi tutamaliza mwaka huu na kutimiza malengo yote mengine vizuri, na pengine kuanza mwaka mpya 2027 vizuri zaidi.🐒
 
Mkuu ukisikia mtu kuoa kibabe ndio mimi. Sikutaka mambo mengi... Nilituma mshenga, nikalipa mahari, nikafunga ndoa bila harusi nikamwambia nyakuja kufanya party baadae bila kuchangisha fedha. Hiyo party nayo imeyeyuka.
Hicho ulichokifanya siyo kibabe!! Ndivyo inavyotakiwa!!! Ndoa ni kati yako wewe na mke wako!!! Ndoa siyo kitu cha kuwafurahisha wasiohusika!! Maisha ni kati ya wewe na mkeo!!

Bahati nzuri mimi nilifanya hivyo mwaka 1998!!!
 
nimekuwa inspired
 
Hakuna chochote nilichofanya natumia huu muda uliobaki kulipa Madeni tu nianze mwaka mwimgine nikiwa SiNA MADENi
 
Namshukuru Mungu kwa afya njema tu, ila ni mwaka ambao sitokuja kuusahau😭😭 nna machungu mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…