uran
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 10,392
- 15,948
- Thread starter
- #101
Sio mchezo jana tumekaa Darajani Masaa mawili na Dakika 25.Leo unakuja bunju yani hii nchi haki Afrika **** shida. Barabra ya mabwepande mbovu kwa miaka mingi. Ila kisa leo mwenge unapita wamepitisha grader wakamwaga na kokoto hapo ili mwenge upite vzuri na baada ya siku kadhaa itarudi kuwa vile vile. Mimi leo nilikuwa nna safari ya kwenda down town ila siendi maana najua nitakuwa stcuk kwenye folen kuanzia bunju hadi mwenge huko.
Mimi sielewi haya masuala ya kutengeneza barabara kiongozi akiwa anapita. Kuna siku rais nadhani ilikuwa feb alienda mtembelea mzee Makamba. Ile barabara ya kuelekea mtaani kwake mbovu sana miaka na miaka. Ila siki 2 kabla likapitishwa gereda ikachongwa na kumwaga kifusi. Mabanda ya wauza mboga mboga yakaondolewa. Boda bida wakaambiwa waondoke pale kituoni wakae mbali. Lakini hawakusema kuwa atapita rais. Ila mimi nikabaki najiuliza baada ya kupita rais wanajaribu kumficha umasikini walionao anaowatawala hadi wanabomoa mabanda yao au maana sielewi. Barabara yenyewe baada ya mwez ikarudi katika hali yake na kwa makamba hata hakukaa zaidi ya dakika 30
Unafika kwa muhindi analeta shida balaa wakati yeye anaishi nyumba hiyo hiyo