Huu Mwenge usiwe unakimbizwa Dar es Salaam, unatuchosha na kutupotezea muda

Sio mchezo jana tumekaa Darajani Masaa mawili na Dakika 25.

Unafika kwa muhindi analeta shida balaa wakati yeye anaishi nyumba hiyo hiyo
 
Mtanzania na muda wapi na wapi bana. Mambo chungu nzima ya kipuuzi wabongo wanafanya ya kupoteza muda ije kuwa hii ya mwenge wa masaa mawili.
 
Mtanzania na muda wapi na wapi bana. Mambo chungu nzima ya kipuuzi wabongo wanafanya ya kupoteza muda ije kuwa hii ya mwenge wa masaa mawili.
Siku ukifanya kazi na muhindi utanielewa mkuu. Kwenye ishu ya muda.
 
Mwaka aliokufa Mwenge haukukimbizwa sababu ya covid...mwaka aliokufa na mwaka WA nyuma yake na kweli hakutoboa
Hauna manufaa yeyote zaidi ya hasara
Watoto wa zinaa tu ndio wanajaa mitaani na uvujishaji wa hela, ndio watu wanapopiga hapo
Baada ya covid wangeachana nao tu
 
Tafuta nchi ya kuhamia, mwenge ni tunu ya Taifa. Nna wasiwasi na uraia wako
 
We mshamba umetoka mkoani kwako leo unaiona Dsm ni kwenu na minyodo ya kipuuzi. Dar ina wenyewe we wakuja tu. Rudi kwenu we bwege
 
Ila Njerere au basi!
Enzi hizo primary tunaimba mwenge ooooh mwenge!!! Mbioo mbiooo mwenge tunaukimbiza!!! Mbio mbio hadi makao makuu mbio mbiooo!!
 
Hakuna kitu kama hiki. Mnaoshiriki na kuamini haya mambo ni mnaamini katika ushirikina na ibada za wengine msizozijua.

Kwa hiyo tusipokimbiza mwenge ndio uhuru utaondoka tutarudi kutawaliwa? Ni uhuru gani ambao tunao ikiwa bajeti yetu tu ni tegemezi kwa kiwango kikubwa kwa hao waliowahi kututawala?
 
Mwenge bdo upo sana tu hata miaka 100 ijayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…