Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Hapa pamenichanganyaHivyo Rwanda walitegemea kupata support tena ya Angola, lakini ambacho walisahau ni kwamba maadam maslahi ya Angola yaani waasi wa UNITA walikua hawana support tena ya DRC hawakuwa na haja ya kumtoa Kabila na ndio hapa vita ikapata sura mpya kabisa iliobadili historia.
Mnamo August 22 majeshi ya Angola, Zimbabwe na Namibia yaliingia kwenye uwanja wa vita kupitia kusini mwa Kinshasa hivyo majeshi ya watutsi 800 (yaliyoongezwa nguvu na askari 2000 wa zamani wa Mobutu ) wakazingirwa katikati ya Kinshasa.
Vita ikachachamaa na Zimbabwe walitumia ndege za kivita huku Angola ikiingiza vifaru na mizinga mizito (Heavy Altirelly) huku askari wa Rwanda wakiwa na silaha nyepesi bila msaada wa ndege au vifaru. Hivyo wakawa hawana namna zaidi ya kusurrender.
Gen. James kabarebe hakuwa tayari kusurrender ingawa alikua amezingirwa katikati akiwa hana pa kutoka. Akaja na uamuzi mzito wa kuvamia Angola kwa nyuma ili wapate nafasi ya kupumua na kurudi kwao kishujaa kuliko kupata aibu ya kushindwa vita.
Mnamo mwezi september 1998, Makomandoo wa kitutsi (Rwanda, UG na Burundi) walivamia Eneo la Zombo de maquela huko Angola ambapo walisambaratisha majeshi ya Angola ya eneo hilo na kuteka uwanja wa ndege wa jeshi.
Walipodhani wamepata mwanya wa kutorokea, changamoto ilioonekana ni kwamba uwanja ulikua mdogo sana kwa ndege kubwa kutua hivyo alihitaji walau wiki 3 wapanue uwanja ndio askari watoroshwe.
Wakiwa Angola walipanua uwanja wa ndege na kufanikiwa kuondoka
Je wakati huo Congo kulikuwa na majeshi gani