Huu ndio Mtihani kwa ACT-Wazalendo: Kukubali maridhiano na kuunda Serikali

Huu ndio Mtihani kwa ACT-Wazalendo: Kukubali maridhiano na kuunda Serikali

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Tafsiri kupitia tamko la Rais mteule wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, baada ya kutangazwa mshindi, inaweza kujenga taswira kuwa kiongozi huyo anaweza kuwa na dhamira ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Hata hivyo, mtihani upo kwa mpinzani wake, Maalim Seif Sharif Hamad na chama chake cha ACT-Wazalendo kutoa uamuzi ndani ya siku saba baada ya Rais kuapishwa.

Akizungumza baada ya kutangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kuwa Rais mteule wa Zanzibar, Dk Mwinyi alisema ataendeleza maridhiano yaliyopo kikatiba

Alisema atadumisha amani iliyopo kwa kushirikiana na wapinzani kwa sababu wao ni nyenzo muhimu katika kukuza demokrasia nchini.

“Nipo tayari kuyaendeleza maridhiano yaliyopo katika katiba yetu, kwani Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofauti zetu, nitashirikiana nanyi kujenga Zanzibar mpya,” alisema Dkt. Mwinyi

Akiwa ameshinda kwa zaidi ya asilimia 76.2 alisema kuwa amepokea ushindi kwa mikono miwili na akaahidi kuijenga Zanzibar kwa ushirikiano na Wazanzibari wote bila kujali itikadi

Hata hivyo, kwa mwongozo wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, ACT-Wazalendo wanapaswa kuketi na Dk Mwinyi ndani ya siku saba kisha kumpa jina la mtu wanayempendekeza kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, vilevile kufanya mashauriano kuhusu muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Kauli hiyo ya Dk Mwinyi, pamoja na ile nyingine kwamba “Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofauti za kisiasa”, inaweza kujenga picha ya utayari wake wa kushirikiana na wapinzani wake kuunda Serikali

Mtihani ni Seif ambaye awali alitangaza hatamtambua aliyetangazwa kama Rais wa Zanzibar, vilevile uchaguzi uliompa ushindi

Seif alisema uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 27 na 28, haukuwa uchaguzi, bali zoezi la kijeshi. “Uchaguzi ulitekwa na vyombo vya dola. Ikiwa kulikuwa hakuna uchaguzi vipi nitamkubali aliyetangazwa?, hakuwekwa madarakani na wananchi kama Katiba inavyotaka. Amewekwa madarakani isivyo halali,”alisema

Pamoja na msimamo wake huo, bado Seif jana alipozungumza na Mwananchi kwa simu kuhusiana na msimamo wake juu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alirejesha mpira kwa chama chake kwamba ndicho kitakachokuwa na uamuzi wa mwisho

“Kwanza itategemea huyo aliyetangazwa! Akiamua kuunda GNU na kutaka kutushirikisha sisi itategemea maamuzi ya Chama. Si maamuzi yangu,” alisema

Kauli hiyo ya Seif, imeshabihiana na ile ya Mkuu wa Itikadi na Uenezi wa ACT-Wazalendo, Salim Bimani aliyesema: “Chama kitakaa na kutoa tamko la pamoja kuhusu vurugu zote hizi za uchaguzi. Kwa sasa hatuwezi kuzungumzia ushiriki wetu kwenye hiyo Serikali ya Umoja wa Kitaifa”

Kwa mujibu wa Ibara ya 39 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, uteuzi wa Makamu wa Kwanza wa Rais kutoka chama kilichoshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa Rais, si hiari kwa Rais aliyeshinda, bali ni lazima pale mshindi wa pili anapopata kura za urais asilimia 10 au zaidi

Katika matokeo ya urais Zanzibar yaliyotangazwa Oktoba 29, mwaka huu na Jaji Hamid, Seif aliyegombea urais kupitia ACT-Wazalendo, amepata asilimia 19.87, ambayo ni karibu mara mbili ya asilimia zinazohitajika ili chama kilichoshika nafasi ya pili kitoe Makamu wa Kwanza wa Rais na kushiriki kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Ibara hiyo inaeleza bila kutaja idadi, kuwa endapo mshindi wa kiti cha urais hakuwa na mpinzani, basi Makamu wa Kwanza wa Rais atapatikana kupitia chama kitakachoshika nafasi ya pili kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi

Hadi sasa, kabla ya kupitisha majina ya viti maalumu, CCM ina viti 49 na ACT-Wazalendo kimoja
Kwa ufafanuzi huo wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, mantiki yake ni kuwa ACT-Wazalendo ndiyo wenye kutakiwa kutoa majibu ya mtihani wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ama wakubali au wakatae

Na kwa mujibu wa Katibu, wanapaswa kuwa na majibu ndani ya siku saba kutoka siku ambayo Dk Mwinyi ataapishwa.
Kingine kinachoweza kuwapa mtihani ACT-Wazalendo kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni idadi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi

Mpaka sasa wana mjumbe mmoja ambaye ndiye pekee ana sifa ya kuteuliwa kabla ya kungoja viti maalum au hisani ya uteuzi katika viti 10 vya Rais wa Zanzibar.



Source: citizen
 
Hoja nzuri sana hii.
Uchaguzi wa 2015, Maalim Seif akiwa CUF, walifanya ujinga kususia uchaguzi ule wa marudio, na matokeo ya uchaguzi huu ni kufidia makosa, sasa Maalim kupitia ACT, ameadhibiwa. Hata hivyo, kufanya kosa, si kosa, kosa ni kurudia kosa, Maalim Seif alifanya Kosa ile 2015, sasa 2020, asilirudie kosa!.
P
 
Mimi ningemshauri Maalim, kama atakubali kuingia kwenye serikali basi awe na demands ambazo huyi rais wa kulazimishwa azikubali. Kwanza kikosi cha mazombi kifutwe, pili wawajibishwe wote waliohusika katika kuruhusu silaha za moto kutumika na wauwaji wa raia wachukuliwe hatua, uchaguzi ngazi ya wawakilishi na wabunge urudiwe.

Vyenginevyo awaachie sirikali yao tu waendeshe watakavyo wenyewe, tofauti iliopo Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko Zanzibar yenyewe saiv.

Maalim akikubali ivi ivi bila demands basi ajue ameua upinzani 2025, na asitegemee kama kutakuwa na muamko wa watu mana hakuna jipya atakalowaambia wananchi wakatambua kuwa ni maneno tu.
 
Unafiki mtupu!Awaachie serikali yao.

Baada ya kutimiza walichotaka, ndio sasa wanajidai kutaka maridhiano wakati kuna madai kuwa watu wamepoteza Maisha kutokana na vurugu za uchaguzi.

Ni hivi, kinachafutwa sasa ni kushirikisha wapinzani ili kuihadaa dunia lengo likiwa ni kuwapoza wahisani ili waendelee kutoa mikopo na misaada..

Hata huku Bara, Mbowe,Lissu na Zitto, wanaaweza kualikwa Magogoni lengo likiwa ni kuonyesha wafadhili kuwa kuna maridhiano ili waendelee kutoa fedha.

Hivyo,msishangae hao niliowataja na wapinzani wengine wakaanza kushawishiwa kwa kupewa ubunge wa kuteuliwa ingawa naamini kamwe hawawezi kukubali.
 
Hoja nzuri sana hii.
Uchaguzi wa 2015, Maalim Seif akiwa CUF, walifanya ujinga kususia uchaguzi ule wa marudio, na matokeo ya uchaguzi huu ni kufidia makosa, sasa Maalim kupitia ACT, ameadhibiwa. Hata hivyo, kufanya kosa, si kosa, kosa ni kurudia kosa, Maalim Seif alifanya Kosa ile 2015, sasa 2020, asilirudie kosa!.
P
Maalimu akili zake hazipo tumboni we mzee, kama akili zako zilivyo. Maana wewe ungekuwa nafurusa kama ya maalimu ungewaza tumbo lako tu, huku maalimu anawawazia wazanzibar.
 
Hahaha ni ujinga kukubali kuwa mkia kila siku, kwani wakikataa watapungukiwa nini?!

Ningekuwa mshauri wao ningewashauri waachane na ujinga wa maridhiano, maana hakuna tofauti na kugeuzwa Colgate.

Mliishi bila kuwepo huko serikalini, mtaishi bila kuwepo huko serikalini.

Wameshinda wao waachieni watawale!
 
Hoja nzuri sana hii.
Uchaguzi wa 2015, Maalim Seif akiwa CUF, walifanya ujinga kususia uchaguzi ule wa marudio, na matokeo ya uchaguzi huu ni kufidia makosa, sasa Maalim kupitia ACT, ameadhibiwa. Hata hivyo, kufanya kosa, si kosa, kosa ni kurudia kosa, Maalim Seif alifanya Kosa ile 2015, sasa 2020, asilirudie kosa!.
P
Wewe uwa unajifanya una mawazo mazuri lakini umejaa pumba
 
Maalim akikubali ivi ivi bila demands basi ajue ameua upinzani 2025, na asitegemee kama kutakuwa na muamko wa watu mana hakuna jipya atakalowaambia wananchi wakatambua kuwa ni maneno tu.
Na ujue kaamua kustaafu siasa kwa aibu. Kwasabb kwa vyovyote vile Maalim hawezi kugombea tena urais kutokana na umri kumtupa mkono. Aweke masharti yenye maslahi kwa chama chake na nchi kwa ujumla yakikubaliwa akubali kuwa makamu wa kwanza.
 
Maalim analaana ya usaliti aliyoipata tangia akiwa CCM na serikali ya mapinduzi Zanzibar.
ni bora asuse kuliko akikubali anaweza kuwagawa wazanzibar na kuleta tafrani kwa mihemko yake ya kisiasa na chuki zake za kunyimwa Urais.
 
Ningekuwa mimi Mwinyi wala nisingekubali, yaani nishinde kwa > 75% halafu mtu aniambie tugawane madaraka? Huu ni ujinga mtu aliyepata 10% ya kura hana uwezo wowote wala hastahili hata kusikilizwa, akafanye homework yake next time aje vizuri, ...
 
Maafisa Vipenyo waliopo ACT na Chadema wanaripoti kuwa ACT itasusia serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuwa hata ikiundwa Vingunge wote mbali ya Seif hawatoingia kwny Cabinet kwa kuwa sio Wawakilishi na pia Katiba haimlazimishi Rais Mwinyi kuteua Wajumbe wa baraza kutoka upande wa pili hivyo automayically kina Bimani, Jussa, Mazrui watakuwa nje ya viti vya Uteuzi

Upande wa Bara Chadema wamepanga kususia Bunge kwa kuwa Viongozi wakuu wote na Wajumbe wa Kamati kuu ya Chadema wamepoteza majimbo yao hivyo hata wakiruhusu wabunge wa viti maalum waende pamoja na wa kule Rukwa bado kwao binafsi hawatapata manufaa japo wanabishana kuwa kama watasusia ikitokea Serikal ikawanyima Ruzuku ambayo kwa sasa haitopungua 70 million kwa mwezi hali itakuwaje na huku hawana Ubunge?

Binafsi Halima Mdee anataka wasisusie kwa kuwa ana uhakika wa kupata Ubunge wa viti maalum hivyo atakuwa anatumikia kipindi cha nne mfululizo na kuwa Mbunge aliedumu bungeni muda mrefu zaid
 
Sio kuolewa mkuu, sema ubakwe then uambiwe uje kuwa house girl wa mbakaji. Kama sio kutaka jamaa aendelee kukubaka free tu ni nini.

Makamu wa kwanza wa Rais katika katiba ya Zenji ni usanii mtupu, jamaa hana power kabisa.
Hahaha CCM ni wajanja sana walahy
Watu wengi wanadhani Maalim alikataa kujiunga nao kwasababu tu ya kugoma

Ukweli ni kwamba alishakaa ile ofisi akaona ni usanii mtupu mafaili yote yanaishia Ofisi ya makamu was pili(De facto Waziri Kiongozi sasa)

Unapewa kila kitu na serikali gari,ulinzi,ofisi na nyumba ila mpaka ziara akianza kuzunguka mikoani RCs,DCs wala vyombo vya dola hawampi ushirikiano kuratibu anaratibiwa na wenyeji kutoka CUF

Zinakua kama ziara za kuongea na wanachama akaona ukhanithi huo
 
Back
Top Bottom