Maafisa Vipenyo waliopo ACT na Chadema wanaripoti kuwa ACT itasusia serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuwa hata ikiundwa Vingunge wote mbali ya Seif hawatoingia kwny Cabinet kwa kuwa sio Wawakilishi na pia Katiba haimlazimishi Rais Mwinyi kuteua Wajumbe wa baraza kutoka upande wa pili hivyo automayically kina Bimani, Jussa, Mazrui watakuwa nje ya viti vya Uteuzi
Upande wa Bara Chadema wamepanga kususia Bunge kwa kuwa Viongozi wakuu wote na Wajumbe wa Kamati kuu ya Chadema wamepoteza majimbo yao hivyo hata wakiruhusu wabunge wa viti maalum waende pamoja na wa kule Rukwa bado kwao binafsi hawatapata manufaa japo wanabishana kuwa kama watasusia ikitokea Serikal ikawanyima Ruzuku ambayo kwa sasa haitopungua 70 million kwa mwezi hali itakuwaje na huku hawana Ubunge?
Binafsi Halima Mdee anataka wasisusie kwa kuwa ana uhakika wa kupata Ubunge wa viti maalum hivyo atakuwa anatumikia kipindi cha nne mfululizo na kuwa Mbunge aliedumu bungeni muda mrefu zaid
ACT watafanya kosa kubwa kama watasusia Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Wao waombe kwa kuwa wana viti vichache basi Mwinyi ateue japo wabunge wanne au watano kutoka ACT ili wakina Jussa waweze kuingia serikalini.
Pi huku bara kama CHADEMA watamkataza mbunge wao wa Nkasi na pia wale wa viti maalum ambao wanaweza kufika hata kumi basi watakuwa wamejiua zaidi. Mimi nawashauri wale wabunge wa viti maalum watakaoteuliwa na yule wa Nkasi waende bungeni hata kama chama chao kitapinga, ikiwezekana bunge litunge sheria kuwalinda na ubunge wao dhidi ya ubabe wa viongozi wao.
Katika siasa inatakiwa utumie kila fursa unayoweza kuipata. Kule Israel, waarabu ambao wamekubalika kama raia wa Israel hugombania ubunge ma umoja wao unajulikana kama joint list bungeni, sio kwamba wanaikubali serikali ya Israel la hasha ila wanapigana toka ndani na ni chama cha tatu kwa ukubwa bungeni. Isingekuwa ni kuona aibu baadhi ya vyama vya waisrael vingewatumia kuiangusha serikali ila vinaogopa kuonekana vinashirikiana na adui.
Mfano mwingine, kule Kongo enzi hizo ikiitwa Zaire ya Mobutu, mahakama iliwahi kumhukumu mwanasiasa maarufu wa upinzani aliyeitwa Nguza Karl Bond adhabu ya kifo lakini baadae Mobutu alilazimika kumteua huyo huyo Nguza kuwa waziri mkuu wakati ule wa vuguvugu la upinzani wa vyama vingi linaanza na Nguza alikubali uteuzi huo akatolewa jela akawa waziri mkuu.
Hao wabunge japo wachache wanaweza kung'ara bungeni kwa hoja nzito kuliko chadema ilipokuwa na wabunge wengi. Hata hoja yao ya tume huru wanaweza kuipigania toka bungeni huku wemgine wakipigania huku nje.
Alternatively, kama Chadema wanasusia bunge basi wasusie na ruzuku wasichukue ili wasimamie kweli maneno yao.
Jambo moja wapinzani waelewe hakuna uchaguzi mwingine utakaofanyika hadi mwaka 2025 na jumuiya ya kumataifa haiwezi kushinikiza wala kufanikiwa kuilazimisha nchi huru nyingine kufanya uchaguzi. Pili Marekani sasa hivi sio dominant power duniani kuna China na Urusi ambazo zinaipinga Marekani katika medani mballi mbali za kimataifa.
Maridhiano ndio kitu pekee kitakachowawezasha wapinzani walau kuwa sehemu ya uendeshaji nchi lakini siasa za uanaharakati tena wa chuki dhidi ya serikali zitawaumiza wao zaidi. Hakuna mtu atakayeingia barabarani aache kwenda kutafuta riziki na pia ajiletee matatizo. Wakumbuke kuwa sisi wengine wapenda amani tunategemea tutumie barabara hizo hizo kupita kwenda kwenye shugjuli zetu hatuwezi kukubali tufe njaa kwa sababu barabara zinatumiwa kwa maandamano.
Duniani hapa hakuna mtu yeyote hata kama alikuwa rais mwanzoni anayeweza kupambama na serikali.