Huu ndio mtiririko wa utajiri wa waumini wa dini 4 zinazoamini Biblia. Wa mwisho watakushtua.

Huu ndio mtiririko wa utajiri wa waumini wa dini 4 zinazoamini Biblia. Wa mwisho watakushtua.

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
1: Uyahudi (Judaism).
Hawa ndio wanaoongoza kwa utajiri kwani wao wanaamini torah (vitabu vitano vya Musa) vina sheria 613 ambazo ni code za utajiri ukizitumia maishani. Pia wanaamini TANAKH (Yoshua hadi malaki) pamoja na vitabu vyao vinavyotafsiri maandiko hayo kuna siri kubwa za utajiri. Waumini wanazitumia kutajirika. Wao mtu masikini ni sawa na mtu aliyekufa.

2: Mainstream Protestantism (Ulokole wa msimamo wa wastani).
Hawa pia kwa sababu wanahamasishana sana injili ya utajirisho. Wanaamini pamoja na yote Mungu kawabariki hapahapa duniani.

3: UKATORIKI
Hawa kwa sababu tayari wanabase ya miaka zaidi ya 2000. Na dini yao imejifungamanisha na kaisali hivyo ni rahisi kupata koneksheni. Lakini wanashika nafasi hii ya tatu kwa sababu bado wanaathiriwa na nadharia za Kigiriki ambazo ziliingizwa kanisani ambazo zinaamini vitu vinavyoonekana ni vya kuharibika. Wapo wanaoamini katika umasikini ndio ukiroho, ndio maana wengine wanatembea hadi peku wakati Yesu alivaa kobazi muda wote.

4: Wamwisho ni Waprotestant wa msimamo mkali ( wasabato, Jehovah witness na wababtist etc).
Hawa mambo yao mengi wameyahamishia katika ulimwengu ujao, chochote kuhusu huu ulimwengi wanaona kama ni anasa. Hakuna uhamaishwaji wa mistari ya biblia inayohusu uwekezaji, kufanya mambo makubwa kiuchumi maana hata hivyo Yesu alimjibu Petro atabarikiwa hapa duniani na mbinguni zaidi. Ujio wa Yesu haraka usiojulikana siku umewachanganya wasijue wafanye nini. Hii hali ya kusita imewarudisha nyuma. Pia wamehusisha utajiri wa mali na ufreemason au ushetani na ukosefu wa uadilifu bila kujua Mungu wao ni Mungu wa mabilionea Ibrahim, Isaka na Yakobo.

Kabla hujaanza harakati za kujikwamua kiuchumi, anza kuangalia mindset ulizowekewa kupitia dini na vifungu ulivyosomewa vya kukukatisha tamaa.

Karibu kwa maoni zaidi.

Ni mimi mzao wa Ibrahim
Mitale na midimu.
 
Mfano wa namba 2 ni madhehebu gani?
wapentekoste, kwa hapa nchni ni FPCT, TAG, EAGT, PEFA, FGBF, PAG, KLPT,CAG, usijumuishe mitume na manabii akina mwamposa, geor devie, mzee wa upako, gwajima, malisa na vijana wanaoinukia akina masanja na kapola hao wana falsafa zao za mahubiri na mafundisho ya utajirisho
 
utajiri wenu wooote ni wa muislamu mmoja tu baharesa simleti GSM simleti LAKE OIL simleti MO au OIL COM , pambaneni na mmoja tu wakristo woote na wanabii wote tajiri mmoja tu wa kiislamu anawatosha kenge nyinyi
Tunaongelea mambo ya kidunia wewe unaleta takwimu za uswahilini.
Hii naiwahusu waarabu mkuu. Hata hivyo wengi wanautajiri wa kurithi
 
Kuna dini hapo inawapofusha waumini sana ukiwaondoa Wajudaism
 
wapentekoste, kwa hapa nchni ni FPCT, TAG, EAGT, PEFA, FGBF, PAG, KLPT,CAG, usijumuishe mitume na manabii akina mwamposa, geor devie, mzee wa upako, gwajima, malisa na vijana wanaoinukia akina masanja na kapola hao wana falsafa zao za mahubiri na mafundisho ya utajirisho
Asante
 
utajiri wenu wooote ni wa muislamu mmoja tu baharesa simleti GSM simleti LAKE OIL simleti MO au OIL COM , pambaneni na mmoja tu wakristo woote na wanabii wote tajiri mmoja tu wa kiislamu anawatosha kenge nyinyi
sio kweli ni vile wachungaji wengi hawaweki wazi mapato yao ila nikwambie tu kuna maaskofu na mitume wana pesa kuliko mwananchi yoyote hapa Bongo, kaa kwa kutulia kabisa ndugu acha kukurupuka.
 
sio kweli ni vile wachungaji wengi hawaweki wazi mapato yao ila nikwambie tu kuna maaskofu na mitume wana pesa kuliko mwananchi yoyote hapa Bongo, kaa kwa kutulia kabisa ndugu acha kukurupuka.
Kwani Bakhresa kaweka wazi mapato yake wapi?

Huwezi kua na hela kumzidi Bakhresa halafu usijulikane,hata biashara zako zitakuonyesha tu.
 
Mungu Wa Ibrahim Isaka Na Yakobo Ni MUNGU wa masikini viwete,yatima na wajane sio Mungu Wa mabilionea hapo umekosea.
 
Back
Top Bottom