Huu ndio uhalisia, hakuna rais atakae maliza matatizo ya Tanzania

"Hata wewe ungepata nafasi ya kula ungekula tu, hahahahahh...!)"

Kauli ya kijinga kuhalalisha ufisadi 🚮
 

Matatizo ni sehemu ya maisha duniani. Hivyo matatizo ni endelevu! Hayaishi!
Matatizo hayahitaji ahadi hewa zisizotekelezeka! Wananchi wanapaswa kuona matatizo yakitatuliwa kwa usahihi na usawa kadri fursa zinavyopatikana!

Mifumo madhubuti inatakiwa kuhakikisha fursa ya kula inapopatikana inufaishe wananchi wengi, leo na miaka mingi ijayo.
Wananchi ndo walipa kodi, tozo na ushuru... Wasipoona usawa kwenye mgawanyo wa matumizi muhimu watahoji!
Wanapoona viongozi na wanasiasa wana maisha ya kifahari wakati wao hawajui atma yao lazima watahoji.

Viongozi na wanasiasa wakijisahau na kuendelea kutumia matatizo ya wananchi kama mtaji wa maendeleo yao binafsi, lazima wananchi wataamka usingizini.
 
Mkuu, ndio maana katika aya ya tatu kama sio ya nne, nimesema, kama tutapata kiongozi mwenye nia njema na taifa atatupunguzia matatizo ila sio kuyamaliza, hata huko china, amerika na kwengineko bado wanachangamoto zao ingawa wapo juu kiuchumi.
 
Matatizo hayawezi kuisha lakini mkipata rais mwenye akili huwa analunguza kwa kiasi kikubwa tofauti na hawa waimba taarabu za mwanakwerekwe ambao wanaongeza matatizo juu ya matatizo
 
Tunapima kwa KPIs.

Sasa miaka zaidi ya 65 bado watu hawana maji ,umeme na barabara kwenye majiji maukbwa bado vumbi.

Nenda kwa Kagame ambao walitoka kwenye VITA uone jinsi walivyo ,utakuja kusema kwamba Rwanda ni ndogo ,haya Dar nayo ni NDOGO mbona ipo kama DAMPO? Mji wa Kigali hakuna Vumbi yaani ni Lami ,Garden ,pavements.
 
Sahihi ila sio Kwa kiwango kikubwa
 
Mkuu, ndio maana katika aya ya tatu kama sio ya nne, nimesema, kama tutapata kiongozi mwenye nia njema na taifa atatupunguzia matatizo ila sio kuyamaliza, hata huko china, amerika na kwengineko bado wanachangamoto zao ingawa wapo juu kiuchumi.
Inaonekana akili yako imeathirika na hii tabia iliyopandikizwa wakati wa Magufuli na hata sasa kuwa maendeleo yanaletwa na rais. Hii ndio inapelekea ww kusema hakuna rais atamaliza matatizo ya nchi hii.
 
Mkuu, #Tindo naheshimu mtu anaetumia akili yake kuchakata mambo, bila kufuata mkumbo, yani nani amesema nini.

Hivyo mawazo yako ninayahemu ila siyakubali, kwani yapo kinyume na kile ninachoamini.
 
Haueleweki kabisa
 
This is low mind.

Huoni kujilimbikizia pesa na kuliibia taifa kama sababu ya kukosa maendeleo ??..

Are you serious. Najua unatania tu. Mtu anaiba fedha zinazotosha kujenga madaraja 10 na shule 20 bado huoni shida ????? Duuuh.

Kama ndiyo hivi waacheni waendelee kujibebea.
 
Matatizo hayamalizwi Kwa siku moja au mwaka mmoja ila CCM hata miaka 1000 hawawezi kumaliza tatizo la matundu ya choo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…