Plaintiff
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 307
- 216
Kitu cha kwanza cha msingi ambacho unatakiwa kujua ni kwamba, kuna mstari mwembamba sana unaotenganisha kati ya ibada ya Mungu na ibada ya sanamu(Shetani).
Hii ni kwa sababu hata yeye shetani hawezi kuja kuwatafuta watu kwa jinsi alivyo, atawatafuta watu kwa jinsi ya Mungu kiuhalisia watu wanakuwa wanamuabudu shetani.
Hivyo shetani anafanya kazi zake kupitia watu kama ambavyo Mungu anafanya kazi zake kupitia watu. Shetani anafanya kazi zake kupitia mafundisho ya uongo hata kama ni ndani ya Kanisa.
Hivyo nimejaribu kuanisha baadhi ya mambo ambayo ukiyafuata utakuwa unaishi ndani ya ukristo wa kweli na siyo kumtumikia shetani.
1. Kuzishika sheria zote za Mungu bila kuacha hata moja.
Kama zilivyoandikwa katika vitabu vya kutoka na kumbukumbu la torati 5 na Kutoka 20. Wala usiache amri yoyote kwa maana hakuna mahali popote kwenye Biblia kuanzia Mwanzo mpaka Ufunuo wa Yohana ambapo amri hizo zilibadilishwa.
Kinyume chake itakuwa ni kufuata mafundisho ya wanadamu.
Ukisoma Isaya 29:13 Inasema "Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;"
Na Injili ya Mathayo 15: 8-9 imeweka wazi juu ya watu wanaofundisha mafundisho ya wanadamu ya kwamba wanamuabudu Mungu Bure. "Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu."
Pia Yesu kristo aliweka wazi kwamba hakuja kutangua sheria ya Mungu(Torati) bali alikuja kuitimiliza, Mathayo 5:17 "Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza."
2. Kuziishi Amri hizo za Mungu,
Kumekuwa na changamoto kwamba hata wale wanaozishika amri za Munguimekuwa ni ngumu kuziishi, hivyo imekuwa ni kama vitu ambavyo mtu amevikariri kichwani mwake lakini havipo Moyoni kabisa. Na sehemu nyingi ukisoma kwenye Biblia, sehemu kubwa ya kuyaishi maisha ya kristo ambayo imehubiriwa ni upendo. Hasa kuwajali wale wenye uhitaji.
Angalia Luka 11:42 Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili.
Yakobo 1:27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
, Waefeso 4:28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.,
N. K.
3. Kutomuona kiongozi wa dini kama ndio kila kitu ndani ya kanisa.
Hiki kitu kimepelekea watu wengi sana kumuacha Mungu kwa sababu kwenda kwao kanisani ilikuwa ni Kumfuata kiongozi wa dini na siyo kumfuata Mungu. Wanasahau kwamba huyo kiongozi wa dini ni Binadamu na mbaya zaidi siku kiongozi huyo atakapoanguka katika dhambi ndio siku ya mshiriki huyo kuacha kwenda kanisani.
Mungu awabariki viongozi wa Dini wanaojishusha na kujiweka katika mizani sawa na watu wengine.
4. Kuacha kuhukumu na kunyooshea watu vidole.
Hii haina tofauti sana na point namba 3, labda tu niseme hakuna mzigo mkubwa utaubeba maishani mwako kama kushuhidia uovu wa mtu. Na usipokuwa makini, huo uovu wake unaweza kukuangusha kiimani hata wewe mwenyewe.
Mungu anatupa nafasi ya pili kila tunapokosea, hivyo wakati wewe unaendelea kumnyooshea mtu kidole, huenda mtu huyo alishayaweka mambo yake sawa na Mungu, We utaendelea kumnyooshea kidole au hata kuacha kwenda kwenye nyumba ya ibada.
Usitolewe kiimani na maovu ya watu ambao mnaabudu nao sehemu moja kwa sababu hata nao ni binadamu.
Haya ni baadhi tu sababu Muda umenibana ila yapo mengine. Nitaendelea kuandika kwa kadri nitakavyoweza.
Mungu awabariki.