Black Label
JF-Expert Member
- Aug 18, 2021
- 432
- 553
Kwa nini hakuna accountanility kwenye sadaka: Kujua nini kimepatikana na kimetumika vipi kama CAG wanavyofanya?Sasa usipotoa sadaka, Mapadre wetu na Watawa wataishi vipi? Na wakati wamejitolea maisha yao yote hapa duniani kulitumikia Kanisa la Mungu?
Marekebisho ya nyumba ya Mungu yatafanywa na nani, kama siyo sisi waumini?
Huduma mbalimbali kwenye nyumba zetu za ibada zitalipwa na nani, ka siyo sisi waumini? Mfano ununuzi wa vifaa vya kuendeshea misa, malipo ya wahudumu mbalimbali, nk!!
By the way, hiyo sadaka na zaka huwa tunatoa kwa hiyari. Na hatutoi huku tukiwa tumesimamiwa na mtutu wa bunduki.
Au unataka uniambie na nyinyi msikitini kwenu huwa hamtoi sadaka na zaka?
Kitendo cha kutumia sadaka kwenda kujenga hoteli binafsi ya askofu hakiingii akilini na kinanipa mimi muumini haki ya kusita au kukataa kutoa sadaka kwa huyo askofu. Badala yake nikatoa sadaka kwa njia nyingine!!!