Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
- Thread starter
-
- #21
ππππsubiri muone!kitila waziri mkuu,lowasa makam wa rais!rais jiwe!!!mbona mashehe kazi mnayo!!
Naam, ukiwa kiongozi wa nchi 'home' ni nchi yako yote.
Naona umeandika kwa haraka haraka ukasahau matakwa ya katiba!subiri muone!kitila waziri mkuu,lowasa makam wa rais!rais jiwe!!!mbona mashehe kazi mnayo!!
Sikuuliza hilo la ushauri kuwa 'valid' lini au bado uko 'valid' leo. Tafadhali nielewe.
Labda nikupe 'hint' kidogo ndipo utaelewa.
Huyo aliyepewa ushauri huo hapo 1995, na yeye leo anatoa ushauri huo huo kwa mtu wake?
ππππ
Rais akitoka upande mmoja wa muungano basi makamu wake atatoka upande wa pili.
Ni kweli kabisa, hakuma linaloshindikana nchi hii.Tunaweza kumpatia uraia wa upande wa pili nani kakwambia hilo linashindikana.Ikiwa mbunge kajivua uanachama halafu anarejeshwa bungeni kwa nguvu huku akidai yeye mwenyewe alishaondoka nini kinashindikana.
Ni kweli kabisa, mwalimu alikua anaona mbali sana. Unaweza sikiliza hotuba yake ya mwaka 67 ukabaki mdomo wazi.Ila mwalimu bwana alikuwa ana bonge la maushauri sijui wengine wanakwama wapi
Nilimsikia mzee mmoja mstaafu eti anashauri kiongozi aliyepo aomgezewe zaidi ya miaka 10 wakati yeye miaka yake ilipoisha alitoka nduki Kali na sasa hivi anakula bata batani haguswi na yeyote
He was a real Genius and a Father of our NationKabla ya kuchukua fomu ya kugombea urais wa JMT, Ben Mkapa aliamua kwenda kumuomba ushauri/ridhaa Mwalimu Nyerere kwa kumwandikia ujumbe na kuutuma butiama, lakini pia baadae Mkapa alipokutana na Mwalimu kwenye vikao vya chama Dodoma alipata wasaa mzuri wa kumweleza kwanini ameamua kugombea.
Mwalimu alimwelewa Ben na kumpa ushirikiano wa kutosha, baada ya kupata ushindi na kuapishwa kuwa rais wa awamu ya tatu 23/11/1995, mzee Mkapa aliona ni busara aonane na Mwalimu ili apate kumshukuru na pengine apante nafasi ya kushauriwa mawili matatu na mwalimu.
Walipoonana Mwalimu alimpongeza Ben kwa ushindi wake, kisha baada ya hapo Ben akamshukuru Mwalimu na akamuuliza, "Mwalimu unaushauri wowote juu ya nani awepo na nani asiwepo kwenye baraza langu la mawaziri?"
Mwalimu alimjibu hivi, "Ben, hili ni baraza lako, sio langu. Serikali yako sio yangu. Kwahiyo nenda ukaiunde. Ushauri pekee ninaoweza kukupa ni huu, kwanza, lazima ukumbuke kuwa nchi yetu ina jamii/makabila mengi, kwahiyo hauwezi kulipuuzia hili moja kwa moja, lazima ujaribu kutengeneza uwiano. Pili, pia tuna dini mbalimbali, tunazo dini kubwa mbili, hauwezi kupuuzia huo ukweli. Mbali na hayo, ni serikali yako, baraza lako, nenda kaliunde."
Hizi zilikua ni hekima na busara za mwalimu mwaka 1995, akijaribu kumwonesha njia sahihi kijana wake. Ni matumaini yangu kuwa kila atakayepata nafasi ya kukalia kiti kilichowahi kukaliwa na Mwalimu ataiona thamani ya ushauri huu.
tangu lini jiwe likaheshimu katiba???Mhimili wa jiwe umejichimbia sana kuliko wowote ule!!
Ni kweli kabisa.Raisi pekee ambaye hakuliangalia hilo la mgao wa kijimbo na kidini ni hii Awamu ya Tano.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna kinachoshindikana kufanyika nchi hii mbele ya mwenyekiti wa ccm hata corona tumeweza kuimaliza kwa kutumia mbinu rahisi kabisa ya kupima mapapai,mbuzi & oil hata kama machadema hayakutaka tuimalizeTunaweza kumpatia uraia wa upande wa pili nani kakwambia hilo linashindikana.Ikiwa mbunge kajivua uanachama halafu anarejeshwa bungeni kwa nguvu huku akidai yeye mwenyewe alishaondoka nini kinashindikana.
Ndio maana tunataka DJ awe Kiongozi, baada ya uchaguzi wa 2020Kabla ya kuchukua fomu ya kugombea urais wa JMT, Ben Mkapa aliamua kwenda kumuomba ushauri/ridhaa Mwalimu Nyerere kwa kumwandikia ujumbe na kuutuma butiama, lakini pia baadae Mkapa alipokutana na Mwalimu kwenye vikao vya chama Dodoma alipata wasaa mzuri wa kumweleza kwanini ameamua kugombea.
Mwalimu alimwelewa Ben na kumpa ushirikiano wa kutosha, baada ya kupata ushindi na kuapishwa kuwa rais wa awamu ya tatu 23/11/1995, mzee Mkapa aliona ni busara aonane na Mwalimu ili apate kumshukuru na pengine apante nafasi ya kushauriwa mawili matatu na mwalimu.
Walipoonana Mwalimu alimpongeza Ben kwa ushindi wake, kisha baada ya hapo Ben akamshukuru Mwalimu na akamuuliza, "Mwalimu unaushauri wowote juu ya nani awepo na nani asiwepo kwenye baraza langu la mawaziri?"
Mwalimu alimjibu hivi, "Ben, hili ni baraza lako, sio langu. Serikali yako sio yangu. Kwahiyo nenda ukaiunde. Ushauri pekee ninaoweza kukupa ni huu, kwanza, lazima ukumbuke kuwa nchi yetu ina jamii/makabila mengi, kwahiyo hauwezi kulipuuzia hili moja kwa moja, lazima ujaribu kutengeneza uwiano. Pili, pia tuna dini mbalimbali, tunazo dini kubwa mbili, hauwezi kupuuzia huo ukweli. Mbali na hayo, ni serikali yako, baraza lako, nenda kaliunde."
Hizi zilikua ni hekima na busara za mwalimu mwaka 1995, akijaribu kumwonesha njia sahihi kijana wake. Ni matumaini yangu kuwa kila atakayepata nafasi ya kukalia kiti kilichowahi kukaliwa na Mwalimu ataiona thamani ya ushauri huu.
DJ ndio nani tena? Anauhusiano gani na ushauri maridhawa wa mwalimu?Ndio maana tunataka DJ awe Kiongozi, baada ya uchaguzi wa 2020
Wewe utakuwa sio mtanzania nini??? Hivyo hata joy usia wa Mwalimu utakuwa huelewi vizuriDJ ndio nani tena? Anauhusiano gani na ushauri maridhawa wa mwalimu?
Labda ni umri ndio unanitupa mkono, lakini enzi zetu DJ alikua ni 'Disc Jockey' na hakua na uhusiano wowote na mambo ya siasa za nchi.Wewe utakuwa sio mtanzania nini??? Hivyo hata joy usia wa Mwalimu utakuwa huelewi vizuri