Jameni, tukifumze kupenda basi, mbona tunaponda sana??
Stars kufanya vizuri ni LAZIMA tuipende? ndio timu yetu.
Naona Adidas wametubwaga, Kuna brand kibao kama puma, new Balance, n.k, wote wakatae kudhamini?
Hata mimi sielewi. Sijui ndio mambo ya Simba na Yanga kwenye timu ya taifa? TFF imejaa watu wa mizaha sana
Iam sorry to say,'' Jezi hazivutii, na wala hazichezi na watazianzia kwa waarabu wakipigwa bao 5-1. Mimi ni mtanzania lakini kwa stars hii. YATOSHA!
Hiyo rangi nyeupe imetokea wapi?
Watumie rangi za bendera. Ndio alama ya taifa hiyo
Wameamua kuwafurahisha Simba, majanga matupu!
Ikumbukwe Malinzi ni shabiki wa timu ya wananchi au wazee wa kimataifa tangu kitambo, sasa inakuaje amfurahishe mnyama?
Kiukweli JEZI za Taifa zinatakiwa ziwe na color ya bendera ya TAIFA.
TUSIPOTOSHE UKWELI.
MATAIFA YOTE NATIONAL TEAM IS A symbol of NATION,period.
Bora hata bukta zingekuwa nyeusi
uzi unatakiwa kuwa na rangi ya taifa tu, nyeupe ya nini??
Mkuu, hao wanakuja timu ikiwa na mafanikio. Hawafanyi udhamini bora udhamini tu. CHAN tupo hoi, Mataifa ya Afrika hoi bin taabani, kombe la dunia ndio usiseme. Sasa huo udhamini utawapa faida gani?
Heri washonewe vitenge maana kwenye mpira hawana faida,sometimes ikifikaga swala la timu la taifa mpaka natamani kukana utanzania
Hahahahahaaaa...kweli jf kiboko
Hiyo rangi nyeupe msingi wake au insipration yake ni nini?
Kuna mataifa wanatumia rangi za bendera ya taifa husika. Wengine hutafuta rangi zenye maana fulani kwa nchi zao hata kama hazipo kwenye bendera. Sisi msingi wetu ni nini?
Msingi wa rangi nyeupe ni kuwafurahisha mikia full stop!
Mkuu, hao wanakuja timu ikiwa na mafanikio. Hawafanyi udhamini bora udhamini tu. CHAN tupo hoi, Mataifa ya Afrika hoi bin taabani, kombe la dunia ndio usiseme. Sasa huo udhamini utawapa faida gani?