Huu ni mgao wa umeme au mabwawa yamekauka?

Huu ni mgao wa umeme au mabwawa yamekauka?

Tunahitaji majibu yanayoeleweka kama kuna ukame, maji hakuna ya kuendesha mitambo inayozalisha umeme au ni sarakasi za kiutendaji. Mh Makamba tafadhali njoo na taarifa kamili.

Hali hii ya joto bila umeme wala maji mtaleta magonjwa ya mlipuko na ustaarabu wetu sisi waswahili huwa unaishia kuvaa nguo na si vyooni.

Hivi Bi mkubwa Kashaenda Afdb Abidjan au Johansburg kwenye mkutano wa wawekezaji. Maana angekuwa mwendazake saa hizi tungesikia jipu la nishati limeshatumbuliwa na ameshatoa maelezao ya kutosha tuu. This is very unacceptable wakubwa msikae kwenye ma air conditioned offices mkatulia huku wananchi tunataabika.
 
Wananchi wa nchi , tupo kwenye shida saaana.
Makato ya miamala, kukatwa kodi katika luku, Mara luku token hazipatikani, sasa maji hakuna na umeme hakuna.

Na ada zitapandishwa, mafuta ya kupikia juu, diesel petrol juu.

Unajua mtu mmoja aliniiambia hakuna nchi nzuri kuitawala kama Tz , watu wake wanasahau haraka na killa tabu kwao sawa.

Naaamini ni kweli. Tusubirie mengine zaidi ya haya.
 
Mbona umeme wa Zanzibar haukatiki kwani hautoki bara?
 
Babu tulia....CCM tushagota...ok ni maji ya bahari gani yalishawahi kutumika kwa domestic use hapa duniani ? Kwa technologia ipi?

Ruvu imekauka na sasa tunataka rufiji nayo ikauke pia..

Eti mazingira - maweee
 
Dunia nzima inasema.maji ya mwenyezi Mungu tuliyopewa bure tuyatunze .... hili nakubali kwa mto Ruvu.

Haya mto Ruvu kau, maji dar mgawo...hivi sasa tupo Rufiji tunahangaika na technologia ya mwaka 1900 ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji wakati tuna gesi na urani kibao.

CCM mawazo yake huwa ni backwards..
Norway wanatumia sana umeme wa maji pamoja na kuwa na hazina kubwa ya mafuta na gesi asilia. Mbona tunataka kulishana matango pori, vipi? Kinachoendelea huko ni dhana ya energy mix. Kwa kuwa uchumi wetu bado mdogo, ni vizuri kwenda hatua moja baada ya nyingine vinginevyo " mtaka vyote kwa pupa..... "
 
Mkuu hizi ni hujuma...

Ni hujuma tuu..

Na makamba ameletwa hapo kimkakati.

Subiri.. Tutaelewana baadayee..
Lile dude nalo limekalia kulembua tu utafikri limewekewamo! Kazi kweli kweli!
 
Hawataki kutangaza ila naamini kuna mgao, umeme umekatika tangu asubuhi ndio umerudishwa sasa hivi, kama ni hujuma za makusudi walaaniwe wote wanaofanya huu mchezo wa kihuni, wapo wanaojitafutia riziki zao kwa kutumia umeme wanapowakatia bila taarifa siku nzima wanataka wakale wapi?
Mkuu, hata kwa hili humkumbuki JPM aliposema mtamkumbuka kwa mema?
 
Dar es salaam hakuna umeme maeneo ya Chanika tangu jana na leo siku nzima hakukuwepo umeme hadi hivi niandikapo.

Je, ni halali Tanesco kupokea pesa kutoka kwa wateja wake halafu wagome kutoa huduma?

Je kama Kuna matatizo ya kiufundi hivi si busara kuwataarifu wateja wanaotegemea umeme wa Tanesco kuendesha biashara zao juu ya katizo la umeme ?

Je tujipange sasa kutegemea umeme wa gesi kama alivyolisha matango pori na Waziri wa nishati?

Du ... Maswali ni mengi tu, Ila giza totoro kama enzi za ujima wakati Chief Hangaya akiendelea kupinga mwingi.
tupo tunafanya maintanance tulieni. 😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳
 
Dar es salaam hakuna umeme maeneo ya Chanika tangu jana na leo siku nzima hakukuwepo umeme hadi hivi niandikapo.

Je, ni halali Tanesco kupokea pesa kutoka kwa wateja wake halafu wagome kutoa huduma?

Je kama Kuna matatizo ya kiufundi hivi si busara kuwataarifu wateja wanaotegemea umeme wa Tanesco kuendesha biashara zao juu ya katizo la umeme ?

Je tujipange sasa kutegemea umeme wa gesi kama alivyolisha matango pori na Waziri wa nishati?

Du ... Maswali ni mengi tu, Ila giza totoro kama enzi za ujima wakati Chief Hangaya akiendelea kupinga mwingi.
Huwezi kutegemea umeme wa gesi pekee tunahitaji energy mix iwapo kuna nia njema ya kutatua matatizo ya nchi hii vinginevyo ni hujuma tu zinafanyika kwa sasa. Serikali ifuatilie kwa karibu na waziri awjibike haraka na bodi yake. Uchumi utaanguka haraka sana. Kalemani arudishwe kurekebisha mambo.
 
Wanasema hakuna shida ya maji wala umeme ,ukiwa na hela hauwezi kufeel kama kuna mgao wa maji wala umeme.

Umeset Generator Auto Mode kwenye ChangeOverSwitch -Umeme ukikatika Generator inapick load then Una reservoir yenye capacity ya litre elfu 50 sasa sijui kama utafeel migao yao.
Siyo wote wana uwezo wa generator. Poor opinion.
 
Mkuu hizi ni hujuma...

Ni hujuma tuu..

Na makamba ameletwa hapo kimkakati.

Subiri.. Tutaelewana baadayee..
Wengine wanasema vijana wa Kalemani ndiyo wanafanya hiyo hujuma kumkomoa Makamba. Hii vita ya madaraka huko CCM inatuumiza sisi walipa tozo,hakika wapiganapo tembo ziumiazo nyasi

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Thread hizi huwaoni nyumbu kama MMAWIA,ERTHROYTE,SALARY SLIP n.k wakichangia,wanaona watasifu legacy,wanasahau nao wanaishi wakati wa sasa
 
Back
Top Bottom