Huu ni mwaka wangu wa mwisho kuajiriwa

Watu wengi wanasahau asilimia kubwa ya walioajiriwa kuna muda watastaafu na itawalazimu kujitegemea/kujiajiri..Ukiacha wanasiasa wachache na makundi mengine machache yenye uhakika wa kiuchumi kwa vizazi vyao,wengi ni pangu pakavu..Ajira ikakata/kuisha ndio watu tunashtuka na kuwekeza kwa kupanic/ kuingia kwenye "quick rich schemes" .
Ni vizuri kuanza mapema shughuli za ujasiriamali (side hustles) zinatujenga baada ya muda..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Nae akishindwa hiyo biashara?
Mana kufungua biashara ni rahisi ila kuifanya ibaki na ikupe faida hiko ni kitu kingine tofauti kabisa!
Ni biashara ambayo tumewahi kuifanya kipindi cha nyuma na tuna uzoefu nayo mkuu...inshort ni biashara ya mbao,milango,madirisha,mabati na kuni (Used)
 
Tunasahau kuna kufukuzwa kazi..
Kudos mkuu.
 
Safi sana, nakuunga mkono. Kapige kazi tena mbili tu, wife mfungulie duka la kawaida maenneo ya kijiji fulani kilichochangamka ambacho ni senta ya vijiji vingine kununua bidhaa au mahitaji. Spea za pikipiki kama kuna soko itapendeza unaweka fundi mlangoni kwako. Halafu zama huko Morogoro sijui Ifakara au Malinyi kapige kazi za kiume kama ulivyosema kilimo na ufugaji wa kuku hutojutia.
 
Nitafanya hivyo mkuu,shukrani sana.
 
Hakuna kitu cha namna hii aisee. Wangaoi washafanya hivyo wakaishia kulia.
Cha msingi ni sacrifice. Ila jua hizo pesa zitaisha na utachalala mtaani baada ya hapo ndio utaanza kupanda taratibu.
Kama wife wako anaweza pata ajira mtafutie kisha wewe ndo uache itakusaidia wakati ukiwa down tena sana. Ukisema umpe 2m na hana experience yoyote itamuia ngumu. Nilipita katika stage hiyo kitambo, hizo pesa unaziona nyingi ila sio nyingi ukiingia mtaani.

Hasara ya kuacha kazi na kujikita katika ujasiriamali

1.hutakuwa na cash ya kwenda bar na kuspend kama waajiliwa
2.utapunguza matumizi yasiyo ya lazima
3.marafiki watakukimbia hiyo sio shida jiunganishe na marafiki ambao ni wajasiriamali huwa wanasaidiana sana temana na waajiliwa kuspend nao muda mrefu utakuwa frustrated sababu watakuwa na cash ya kuspend hata laki bar wakati wewe unataka buku 10 ya matumizi yako

4.Kuza biashara yako taratibu EPUKA madeni katika kukuza biashara

Faida

1. Unawahi mtaani mapema kujifunza namna ya kuishi bila mshahara tofauti na yule mtu atakayestaafu ama akafukuzwa kazi.
2. Unakomaa mapema katika ujasiriamali japo hadi kuja kustabilize yaweza chukua hadi miaka 3-5


Pia note. Usikatike sana kiuno kabla biashara yako haujaijua na kujua cashflow usije ukajikuta una mahitaji ya mtoto na wakati umefilisika haujasimamisha biashara
 
Mkuu hakuna uwezekano ukafanya uwekezaji mahali huku ukiendelea na kazi nyingine?
Hata Mimi namshauri afanye uwekezaji huku akiendelea na kazi nyingine ujasiria Mali ni kujitoa.Wapo watu WANGA miradi inawaingizia fedha nyingi lakini bado wanapiga job.
 
2003 Mimi Niko la tatu
..shkamo baba..
 
Labda niseme tu kila kitu ni mazoea kilimo ni kizuri ila pia biashara ni nzuri zaidi.
 
Mdogo wangu kwanza nakupa hongera kwa kuwa na wazo la ujasiliamali. Hongera sana

Pamoja na yote uliyoyaongea mimi naomba nikupe ushauri na naomba uufanyie kazi kikamilifu kwa kuwa mie nina uzoefu wa yote mawili unayoyapitia na kutaka kuyafanya yaani kufanya kazi na kufanya ujasiliamali.

Naanza kuwa ujumbe ambao niliusoma humu jana na kuuandika katika DIARY yangu nanukuu "Imenichukua miaka 30 kufika hapa nilipo, japo vijana wanatamani yote haya ndani ya usiku mmoja" - Aliko Dangote. Mwisho wa kunukuu

Wewe hauna mtaji hata kidogo (kwa mujibu wa maelezo yako) ila kuna hela za mafao ya kujitoa unazitegemea. Hapo ni tatizo kubwa sana. Fao la kujitoa halitoki kirahisi kama unavyofikiri mdogo wangu. Kuna watu nawajua wanasotea hilo fao toka JPM alivyoingia madarakani mpk leo hii na hawajafanikiwa kulipata. Una mfano mmoja tu wa huyo mtu hujui alikuwa na connection gani mpaka akapata hizo hela. Unaweza kukaa hata miaka mitatu unazungushwa tu. Hata wastaafu ambao wana haki kisheria nao wamekuwa wanapata shida kupata mafao yao wengine miaka miwili au zaidi sembuse wewe.

Kwenye hilo nashauri usiache kazi mpaka uhakikishe umepata mtaji wa kutosha wa kuanza hizo biashara nje ya mafao ya kujitoa unayoyafikiria. Simple logic chukulia umeacha kazi na mafao yakachelewa kwa miaka miwili, utaweza ku-survive?

Biashara inataka mipango (planning) na mipango hiyo ni kuanzia kutafuta mtaji, jinsi ya kuiendesha, mauzo unayoyategemea, faida utakayopata, gharama za uendeshaji pamoja na life span ambayo uwekezaji wako utakulipa (Business Proposal).

Usiache hiyo nia yako ya kufanya ujasiliamali ila jipange vizuri kabla hujaingia huko maana ni kugumu kuliko wengi wanavyodhani.

Mimi ni mwajiriwa wa Serikali ingawa nina cheo na elimu kubwa sana pia ni mjasiliamali mkubwa wa ufugaji kuku wa nyama, samaki pamoja na kumiliki mashamba makubwa Morogoro na Mkuranga. Pamoja na ujasiliamali sijawahi kuwaza kuacha kazi hata siku moja.

Mtumie sana mkeo kwa sababu nadhani kwa maelezo yako hana shughuli ya kuingiza kipato. Mtumie kwenye biashara unayofikira kuifanya ili yeye aianze kwa udogo na kadri siku zinavyoenda itakuwa na utapata uzoefu kupitia yeye ili baadae ukishaona mbivu na mbichi unaweza kufanya maamuzi ya kuacha kazi au lah. Mtaji ambao unaufikiria ni mdogo sana kwa jinsi ulivyojieleza. Ufugaji unahitaji mtaji kama mabanda, mifugo yenyewe, malisho, vifaa vya kulishia na utafutaji masoko. Nashauri usiingie kichwa kichwa ukakwama baadae ila usiliache hilo wazo lifanyie kazi na chukua muda kuanzia chini upande mpaka juu.

Jiwekee mipango na usikurupuke nenda taratibu kwani mafanikia yanakuja kwa mipango na yanachukua muda sana kuiva. Ndio sababu iliyonifanya nianze na ujumbe wa Dangote pale juu. Najua kama kijana una kiu ya mafanikio ila mafanikuwa hayaji ndani ya usiku mmoja mafanikia ni process tena ndefu mno.

Kama una swali au unahitaji ufafanunuzi usisite kuuliza kwani nina uzoefu kwenye yale unayoyawaza.
Nina mengi ya kueleza ila muda ndio tatizo nina kazi nyingi ila nina uhakika nimesema mengi ya msingi
 
una mawazo km yangu mkuu kila kheriii
 
kwa point hii sina cha kuongezea umemaliza kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…