Mdogo wangu kwanza nakupa hongera kwa kuwa na wazo la ujasiliamali. Hongera sana
Pamoja na yote uliyoyaongea mimi naomba nikupe ushauri na naomba uufanyie kazi kikamilifu kwa kuwa mie nina uzoefu wa yote mawili unayoyapitia na kutaka kuyafanya yaani kufanya kazi na kufanya ujasiliamali.
Naanza kuwa ujumbe ambao niliusoma humu jana na kuuandika katika DIARY yangu nanukuu "Imenichukua miaka 30 kufika hapa nilipo, japo vijana wanatamani yote haya ndani ya usiku mmoja" - Aliko Dangote. Mwisho wa kunukuu
Wewe hauna mtaji hata kidogo (kwa mujibu wa maelezo yako) ila kuna hela za mafao ya kujitoa unazitegemea. Hapo ni tatizo kubwa sana. Fao la kujitoa halitoki kirahisi kama unavyofikiri mdogo wangu. Kuna watu nawajua wanasotea hilo fao toka JPM alivyoingia madarakani mpk leo hii na hawajafanikiwa kulipata. Una mfano mmoja tu wa huyo mtu hujui alikuwa na connection gani mpaka akapata hizo hela. Unaweza kukaa hata miaka mitatu unazungushwa tu. Hata wastaafu ambao wana haki kisheria nao wamekuwa wanapata shida kupata mafao yao wengine miaka miwili au zaidi sembuse wewe.
Kwenye hilo nashauri usiache kazi mpaka uhakikishe umepata mtaji wa kutosha wa kuanza hizo biashara nje ya mafao ya kujitoa unayoyafikiria. Simple logic chukulia umeacha kazi na mafao yakachelewa kwa miaka miwili, utaweza ku-survive?
Biashara inataka mipango (planning) na mipango hiyo ni kuanzia kutafuta mtaji, jinsi ya kuiendesha, mauzo unayoyategemea, faida utakayopata, gharama za uendeshaji pamoja na life span ambayo uwekezaji wako utakulipa (Business Proposal).
Usiache hiyo nia yako ya kufanya ujasiliamali ila jipange vizuri kabla hujaingia huko maana ni kugumu kuliko wengi wanavyodhani.
Mimi ni mwajiriwa wa Serikali ingawa nina cheo na elimu kubwa sana pia ni mjasiliamali mkubwa wa ufugaji kuku wa nyama, samaki pamoja na kumiliki mashamba makubwa Morogoro na Mkuranga. Pamoja na ujasiliamali sijawahi kuwaza kuacha kazi hata siku moja.
Mtumie sana mkeo kwa sababu nadhani kwa maelezo yako hana shughuli ya kuingiza kipato. Mtumie kwenye biashara unayofikira kuifanya ili yeye aianze kwa udogo na kadri siku zinavyoenda itakuwa na utapata uzoefu kupitia yeye ili baadae ukishaona mbivu na mbichi unaweza kufanya maamuzi ya kuacha kazi au lah. Mtaji ambao unaufikiria ni mdogo sana kwa jinsi ulivyojieleza. Ufugaji unahitaji mtaji kama mabanda, mifugo yenyewe, malisho, vifaa vya kulishia na utafutaji masoko. Nashauri usiingie kichwa kichwa ukakwama baadae ila usiliache hilo wazo lifanyie kazi na chukua muda kuanzia chini upande mpaka juu.
Jiwekee mipango na usikurupuke nenda taratibu kwani mafanikia yanakuja kwa mipango na yanachukua muda sana kuiva. Ndio sababu iliyonifanya nianze na ujumbe wa Dangote pale juu. Najua kama kijana una kiu ya mafanikio ila mafanikuwa hayaji ndani ya usiku mmoja mafanikia ni process tena ndefu mno.
Kama una swali au unahitaji ufafanunuzi usisite kuuliza kwani nina uzoefu kwenye yale unayoyawaza.
Nina mengi ya kueleza ila muda ndio tatizo nina kazi nyingi ila nina uhakika nimesema mengi ya msingi