Ungechukua likizo na kuenda kwa daktari. Hakikisha unachukua likizo wakati anaanza siku zake. Atapewa dawa za kunywa siku ya kwanza ya hedhi, around siku ya tisa ataanza kufanyiwa 'follicular study' kuangalia upevukaji wa mayai yake. Katika kipindi hichi chote hakikisha mnakutana walau mara moja kila baada ya siku moja (unaruka siku moja). Daktari atawashauri baada ya hapo.
Kuhusu kuondoka, kama anataka kuondoka muache tu. Kwenye habari ya kupata mtoto mpaji ni Mungu really. Hakuna daktari anaejua process inayotokea hadi mimba kujishika kwenye kizazi japo inajulikana yai linapevushwaje. Hii ni alongside kuanza kwa uchungu wa kujifungua (ndo.maana tunabakia kuambiwa wiki mbili kabla ama baada ya tarehe tarajiwa!) Muambie asikutishie, mnahitaji kukaa pamoja na kuangalia mfanye yaliyo ndani ya uwezo wenu.
Kila la kheri.