Huu ni mwezi wa mwisho bila mimba ndoa haipo tena,.nisaidieni jaman!.

Huu ni mwezi wa mwisho bila mimba ndoa haipo tena,.nisaidieni jaman!.

Gambaz

Member
Joined
Oct 9, 2011
Posts
75
Reaction score
2
Heshima kwenu waungana,
Jaman mwenzenu nina tatizo maana mke wangu anataka kuondoka endapo mwez huu hatapata ujauzito maana limekuwa ni ombi lake la muda mrefu,ni kwamba mimi na yeye haituishi pamoja sababu ya majukum ya kikaz hvyo tuna siku maalum tu za kukutana,sasa naomba ushaur lini ni siku nzuri ya kumpa mimba endapo:
Mwez wa1 aliona hedhi tarehe 20
Mwezi wa pili tarh 19,mnishaur lini nkakutane nae kutimiza lengo letu la kupata mimba?
 
nakushauri ndug nenda kwa daktar kupata maelekezo zaid
 
Nyie hamna mapenzi ya ukweli, mmefanya juhudi gani kwa pamoja?
Mkae chini muongee
 
mmmh huyo ni mke au hawara?anaondoka mwenyewe bila kufukuzwa? au keshapata mwingine? pole sana
 
ndugu yangu sipati picha ya aina ya ndoa uliyonayo! kwa nini usitafute namna ya kuishi pamoja na mke wako? hizo ndoa za mwanaume anaishi kule na mke huko hazifai hata kidogo kwani ndio mwanzo wa vishawishi na magonjwa ya zinaa. ipo hatari pia ya kulea watoto wasiokuwa wako! anyway it is my little advice...
 
tunaweza kukupa tarehe lakini je ulihakiki kuwa mbegu zako zina virutubisho?
 
Kuna watakao mawasiliano ya shemeji ili wamsihi atunze ndoa yenu
 
Hebu fanya hv kama mzunguko wake ni cku 28-30.Bac hesabu tangu tarehe ya kwanza kupata hedhi yake ambapo yai hutengenezwa kuanzia cku ya 11-14 ambapo huwa tayari kuru2bishwa hvyo kutaneni ndani ya hzo cku namaanisha cku ya 11 na hasa ya 14.Kama wote mko salama kwa uwezo wa Mungu mtapata mtoto.Note: INABIDI WOTE MSIWE NA STRESS M2LIZE AKILI.Ni hayo 2.
 
Nyie mna siku maalumu ya kukutana, ukipewa siku maalumu unaweza kuvunja mwiko wa tarehe zenu za kukutana, anyway pima uzito kazi na ndoa ni kipi muhimu, au singizia unaumwa rudi kwa mkeo kaa naye kwa mwezi mmoja na nusu kitaeleweka tu
 
Ungechukua likizo na kuenda kwa daktari. Hakikisha unachukua likizo wakati anaanza siku zake. Atapewa dawa za kunywa siku ya kwanza ya hedhi, around siku ya tisa ataanza kufanyiwa 'follicular study' kuangalia upevukaji wa mayai yake. Katika kipindi hichi chote hakikisha mnakutana walau mara moja kila baada ya siku moja (unaruka siku moja). Daktari atawashauri baada ya hapo.

Kuhusu kuondoka, kama anataka kuondoka muache tu. Kwenye habari ya kupata mtoto mpaji ni Mungu really. Hakuna daktari anaejua process inayotokea hadi mimba kujishika kwenye kizazi japo inajulikana yai linapevushwaje. Hii ni alongside kuanza kwa uchungu wa kujifungua (ndo.maana tunabakia kuambiwa wiki mbili kabla ama baada ya tarehe tarajiwa!) Muambie asikutishie, mnahitaji kukaa pamoja na kuangalia mfanye yaliyo ndani ya uwezo wenu.

Kila la kheri.
 
King'asti asante sana kwa ushaur wako na kunipa moyo,asante na ubarikiwe
 
Kwa kuongezea sio kila mwanamke anayeona siku zake ana uwezo wa kubeba mimba/kuzaa. Lakini pia sio kila mwanaume mwenye uwezo wa kumkojolea mwanamke ana uwezo wa kumpa mimba.

Hapa utapewa nadharia ya kalenda,lakini ukumbuke kuna mambo mengi sana yanayosababisha mimba itungwe na kukua.Hivyo basi nakushauri,kabla ya kwenda kwa daktari muulize mwenzio kama kigezo kudumu kwa ndoa yenu ni mimba au mapenzi.Vipi ikiwa akashika mimba halafu kwa bahati mbaya(hatuombei) ikaharibika,atalaumiwa nani?

Mwisho, muulize kiapo chenu siku ya ndoa,yeye alikuahidi nini?
 
Huyo mkeo hajatulia kabisaa. Atasemaje anaondoka wakati bado hamjapata muda mzuri wa to make pregnancy??? Ila kukaa mbali,ni tatizo maana timing yaweza kuwa ngumu. Fuata shauri hizo walizokupa wadau. Pole sana mkuu.
 
Back
Top Bottom